Mwalimu Nyerere Taifa linavuna ulichokipanda

Hii mada ndugu yangu ni kama umeniwahi tu.

Ukweli Nyerere ndie alieweka msingi mbovu sana wa Taifa hili na hata vyama vingi hakutaka viwepo kwenye utawala wake mpaka alipostaafu ndio akaunga mkono wazo hili mwaka 1992.

Mbaya zaidi,mwaka 1995 aliendelea kuwaaminisha wananchi kuwa CCM pekee ndio inafaa kuendelea kutawala nchii hii pale alipoamua kumpigia kampeni Mkapa.

Ni Nyerere huyu huyu alietuachia katiba hii mbovu inayotutesa.

Ni Nyerere huyu huyu aliehubiri amani kiasi kwamba sasa ni wimbo wa Taifa hata pale amani hiyo isipoendana na haki.
 
Suala la kutobadili katiba baada ya kuruhusu vyama vingi ni shida na itaendelea kuwa shida... mwalimu angeweza kutupa katiba mapema kabisa na haya mazingaombwe ya katiba yanayo endelea yasingekuwepo.... mengi mazuri alifanya mwalimu (rip) lakini hili la katiba aliliweka pembeni....na katiba itaendela kutafuna taifa.... amani bila haki ni bomu linalo subiri kulipuka....
 
Great Thinker ! na Mwenye ez Mungu anayaona haya yote na tunamini hakuna alie juu ya Mwenye ez Mungu ipo siku kama tupo hai tutashuhudia haki ikitendeka na hii mbegu aloipanda nyerere ikinyauka na kufa kabisa!
 
mungu ni muweza wa yoto! wapi alipo firauni?

jk na mkapa ni muda tu ukifika kitaeleweka
 
mungu ni muweza wa yoto! wapi alipo firauni?

jk na mkapa ni muda tu ukifika kitaeleweka
Udongo alioutumia yeye ulikuwa na rutuba ikaanza kupunga kidogo kidogo na sasa hivi ni dhahiri udongo ule haufai ndo maana wanatumia kila mbinu angalau hata utoe rutuba lakini hauwezi kuwa na rutuba
 
Makosa tufanye sie ya kushindwa kuondoa watawala, halafi tuanze kuwalaumu marehemu. Hio sio sahihi hata kidogo.
 
Umesahau kiwango cha elimu. Tuna idadi kubwa ya watu wengi wanaoamini wakishahitimu la7 basi. Hawa watu ni mizigo katika mageuzi.

Mwalimu alivifanya vyombo vya ulinzi kuwa kama vya kikoloni mfano jeshi la polisi na usalama wa taifa. Hivi vyombo vimetumika dhidi ya wana wa nchi bila huruma ili kulinda serikali dhalimu.

Mwalimu alipanda mbegu ya woga na kutokujiamini miongoni wa wananchi. Hata mwenye digree mbili bado utamkuta hawezi kuhoji au kutoa maoni yake kwa kujiamini. Hii dhambi itamtafuna Nyrere popote pale alipo. Huwezi kuwaweka wananchi mateka kama tunavyoshuhudia.

Hawa ni watoto wako, Wengine waliongoza kwenye uongozi wako, hawa wamejifunza toka kwako Mwalimu Nyerere mbegu hii uliasisi wewe kuanzia katiba, Muungano, chaguzi zote za ndani ya chama na taifa jumla katika uhai wako. Mwalimu Nyerere hawa hawajajilea Mwalimu Nyerere ni wewe ndo Ulimleta Mkapa ukamkataa kikwete wakati wengi walimtaka.

Mwalimu ni wewe huyo huyo Mkapa alikutoa machozi, Mwalimu yanayotokea Zanzibar ni Wewe ndo uliyaanza Mwalimu hakuna siku uliyowahi kufuata kile wananchi walikitaka hata kama cha kijinga wewe uliwapeleka ulivotaka na sio wao walivyotoka.

Mwalimu ni wewe wewe ulikataa sauti ya asilimia 80 ya watanzania waliotaka tuendelee na chama kimoja, mwalimu hukuwaambia ukweli kaka,baba,mama,bibi na babu yangu kuwa yale yalikuwa makubaliano ya mataifa ya kibeberu ili yatupe msaada Mwalimu ulijifanya eti hawa wachache maoni yao yanaweza kuwa ya msingi Mwalimu uliyakataa maoni ya wengi.

Mwalimu ulikuwa mshikaji mzuri wa biblia takatifu hivi Mwalimu hukuwahi kusoma kisa cha Mfalme sauli wa Israel? Mbona pamoja na MUNGU kuwaambia namna utawala wa Sauli kuwa ungewatesa,kuwadhulumu,kuwaua na kuwanyima haki zao bado wana wa Israel Wengi walitaka Mfalme huyo huyo mbona MUNGU aliwapatia mfalme sauli kwani mwalimu unafikiri hawapo wachache walio ogopa wa kamwambia MUNGU hatumtaki SAULI acha tuendelee na Manabii tu!!! Mwalimu hiki kisa hukukisoma kweli?? Au ulikosoma ukaelewa tofauti na mimimi nilivyoelewa?

Mwalimu huko ulipo Mbegu uliyoipanda imemea na kuzaa matunda na inakuwa kwa kasi.

Mwalimu Tatizo ni udongo huu wa sasa? ule ambao wewe ndo ulipandia mbegu hizi ulikuwa na rutuba kweli kweli tena haukuhitaji hata uongeze mbolea
Mwalimu kwa sasa hivi udongo umeanza kukosa rutuba na si muda mrefu mbegu zako zitasinyaa na kufa alafu zenyewe hizo hizo zitakuwa mbolea na kuleta mimea Mingine.

Mwalimu Taifa linavuna mbegu yako. mimi najua uliwasiliana na Mungu Juu ya Mbegu hii na atakuwa amekusamehe kabisa
 
Umesahau kiwango cha elimu. Tuna idadi kubwa ya watu wengi wanaoamini wakishahitimu la7 basi. Hawa watu ni mizigo katika mageuzi.

Mwalimu alivifanya vyombo vya ulinzi kuwa kama vya kikoloni mfano jeshi la polisi na usalama wa taifa. Hivi vyombo vimetumika dhidi ya wana wa nchi bila huruma ili kulinda serikali dhalimu.

Mwalimu alipanda mbegu ya woga na kutokujiamini miongoni wa wananchi. Hata mwenye digree mbili bado utamkuta hawezi kuhoji au kutoa maoni yake kwa kujiamini. Hii dhambi itamtafuna Nyrere popote pale alipo. Huwezi kuwaweka wananchi mateka kama tunavyoshuhudia.
kuna failure nyingi sana za mwalimu na failure zake zinaonekana kama hazina athari!!!! kwa wakati huo ilikuwa ni sahihi lakini vision yake haikupima kwa uyakinifu matokeo ya miaka mingi ambayo taifa linaishi ukilinganisha na maisha ya mwanadamu
 
Mengi mno
 
Mwaka 1995 yaliyotokea zanzibar Nyerere alikuwepo, je haya yanayotokea zanzibar leo yana tofauti gani na yale ya 1995? Je hatua za kutomtangaza mshindi zina tofauti?
 
Mwaka 1995 yaliyotokea zanzibar Nyerere alikuwepo, je haya yanayotokea zanzibar leo yana tofauti gani na yale ya 1995? Je hatua za kutomtangaza mshindi zina tofauti?
Kamakabuzi1995 yalitokea hawa wa leo walikuwa ndo damu changa yamoto kweli kweli wakawa wanaona baba alivyokuwa akiendesha mji!! na wao wakajua ndivyo inavyopaswa kuwa pindi watakapokuwa na wao ni wababa. sasa leo wanachokifanya hakijaibuka tu bali walipandikizwa haka ka tabia na baba yao na wao wanafanya vile vile.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom