Mwalimu Nyerere na ukabila

Namchukia sana mwalimu, kila nionapo picha yake, hasira unipanda misri ya cobra. Kwanza ndiye chanzo cha umasikini wa Tanzania kutokana na sera zake mbovu.
Umasikini huo ni wa watanzania wote au wako na familia/ukoo ndo unakufanya umchukie marehemu?

Unafahamu kuna watu wamezaliwa baada ya 1999 na wanapesa nzuri tu hapa TZ?

Unafahamu baada ya Mwalimu, kuna maraisi watano wame/wanaiongoza hii nchi?

Unafahamu kuwa Mwalimu alitawala miaka 24 ya mwanzo wa Tanganyika/Tanzania, miaka 36 ikiwa imetimia sasa tangu yeye atoke madarakani?

Miaka 24, akiwa na wasomi pengine wasiozidi 70, ni sawa na miaka 36, wasomi na teknolojia lukuki, na vichwa vitano kama maraisi, bado ulaumu sera za Mwalimu? Mmeshindwa vipi kuzibadili mkaendelea na mkaachana na umasikini? Singapore, Thailand, Malaysia mlikuwa nao sawa enzi za Mwalimu, imekuaje sasa?

Kama itasaidia kubadili sera za mwalimu na kufuta umasikini, huna budi KUZIDA CHUKI dhidi ya marehemu.
 
Hao wanaowwchukia Wahaya ni kina nani?
Maana unasema ndio Kabila linalochukiwa nchini
Mbona mimi nawajua wengi na siwachukii wala sioni wakibaguliwa?

Nyie ndio mnaoendekeza haya mambo
Kama unafanya mambo yako nani anakujali?
 
Wamissionari walijenga shule Bukoba katika harakati za kueneza dini. Hii ilipelekea Wahaya kuwa ni kabila lenye wasomi wengi kabla ya uhuru, sambamba na Wachaga na Wanyakyusa.

Kuna Wahaya walio anza harakati za kuupinga Ukoloni Zamani kabla ya Nyerere, tatizo ni ego hawakuwa tayari kuunganisha nguvu. Kutokana na kujiamini kwao waliweza kumkosoa Nyerere waziwazi na Nyerere hakuwa mtu akiykubali kukosolewa.
 
Hivi kuleta hoja dhidi ya aliyefariki nani wa kujibu hisia na sababu ya kilichotokea kwa uhalisia wake. Kifupi jipangeni huyo unae mpigia makelele keshapumzika
 
Huna uelewa wowote zaidi ya kukariri mambo.
 
Aliipandikiza kivipi, lini?
 
Kwa Sasa ni Lile lililodekezwa kuliko yote na likabweteka Hadi Sasa limeanza lialia linabaguliwa 🏋️
 
Mwalimu Nyerere watoto wake hawajui kuongea kizanaki. Truth is stranger than fiction.
 
Kila aliempinga alionja joto yajiwe

waulize kina bibi titi,kambona,edwin mtei na wengine weengi
Alimtumia kawawa kuua nguvu za kiuchumi za wachagga na wahaya Ili kuwainua wengine, athari zinaoneka leo
 
Wajinga walikuwa wengi isingekuwa Rahisi kutambua hila alizotumia
 
Watanzania muwaelewe wahaya ni watu wazuri ila egoism iko damuni kuiacha ni mgumu ni intrinsic na DNA, tofauti na wachaga
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…