Mwalimu Nyerere hakuwahi kuvaa vazi la CCM 'kijani na njano'?

Mmmmh hii imekaa kiutamu sana, mi naona tufunge safari kwenda Butiama tukamuulize Mama Maria atakuwa anajua siri hii lazima.
 
Nimeukuta mjadala huu mahala fulani, eti wadau nasikia enzi za uhai wa Hayati MWL. J. K. NYERERE hakuwahi kuvaa SARE YA CHAMA, CCM (kijani na njano) hata mara moja.

Je, jambo hili linaukweli ndani yake? Na kama ni kweli tunajifunza nini?

Ndio, na tunajifunza kuwa Nyerere alikuwa anajitambua kuwa yeye ni rais wa watanzania wote na sio rais wa ccm.
 
Niliwahi kuona mjadala humu JF kuwa mwalimu hakuwahi kuvaa kijani...nimeona hii picha sehemu..nikaamua kuiweka..humu
hapo ilikuwa mwaka 1985,mwalimu anang'atuka..

Je..hilo alilovaa ni sare ya chama?...au?
 

Attachments

  • NYerere .png
    NYerere .png
    119.4 KB · Views: 553
  • NYERERE KIJANI.png
    NYERERE KIJANI.png
    226.5 KB · Views: 240
Tofauti na huo mkutano uliona nyingine?

Je huwa aliwahi kuvaa na kushoboka nalo mtaani kama mazoba ya siku hizi?
 
hiyo kijani ya kujifichaficha.lakini hata hivyo hiyo picha umeitafuta kwa mda tofauti na wangekuambia tafuta picha ya kikwete alipo kuwa kavaa kijani.ungetuwekea hadi picha za wake wake na watoto.chiligate hadi kwenye harusi anavaa kijani na miwani tinted hata kama ni usiku wa giza.
 
Acheni Uzushi!!! Sasa kama hakuvaa ndio nini? Mtu akiwa na mke wake wanafungishwa ndoa kanisani au mbele ya Shekh ni lazima ambusu mbele ya watu ndio mjue kuwa anampenda anayemwo???!! Asipombusu basi hampendi?? Huo ni ushamba sana wa baadhi ya watu.
 
Wote chadema nyie na mnakuja na hoja za ajabu sana tena nyepesi nyepesi!!! Hilo ndio mnaona la kujadili!!! Great thinkers!!!! Au majungu tu!!?
 
Acheni Uzushi!!! Sasa kama hakuvaa ndio nini? Mtu akiwa na mke wake wanafungishwa ndoa kanisani au mbele ya Shekh ni lazima ambusu mbele ya watu ndio mjue kuwa anampenda anayemwo???!! Asipombusu basi hampendi?? Huo ni ushamba sana wa baadhi ya watu.

Ni wapi nyerere aliposema anaipenda CCM kama alivyompenda mkewe?. Nyerere aliisha wahi kutamka hadharani wakati akitaka jina la Malecela liondolewe kwenye orodha ya wagombea urais wa mwaka 1995 kwa kutishitia kurudisha kadi ya CCM na kusema 'CCM siyo baba wala mama'.

Mapenzi ya mtu kwa Chama yanatokana na imani yake kuhusu chama hicho. Nina hakika leo hii Nyerere angekuwa hai angeisha ikana hadharani CCM ya leo hii.
 
nimeukuta mjadala huu mahala fulani, eti wadau nasikia enzi za uhai wa hayati mwl. J. K. Nyerere hakuwahi kuvaa sare ya chama, ccm (kijani na njano) hata mara moja.

Je, jambo hili linaukweli ndani yake? Na kama ni kweli tunajifunza nini?

mada nyingine jamani...ujinga mtupu
 
Back
Top Bottom