Mwalimu Nyerere hakuwahi kuvaa vazi la CCM 'kijani na njano'?

Nadhani umenielewa vizuri kukujulisha kuwa CCM walitambulisha rasmi rangi za kijani mwaka 1985. Ni kweli kuwa Nyerere aliendelea na uenyekiti wa chama hadi mwaka 1987, lakini uelewe kuwa kipindi hicho vyombo vya habari kama TV havikuwepo kiasi cha kutotambua kuwa Nyerere amevaa nguo gani muda gani.

Huu sasa ndiyo unaitwa ubishi!!!!!!
 
Hakuna standards kabisa sas hivi......sasa hili jeshi gani la zambarau?

mgambo.JPG

Mkuu u made my day ahahahaha ahahahaha ahahaha!!!!!!!
 
Hakika labda picha hii anaoneka kuvishwa na msanii huyu
View attachment 38909
Hapa Msanii huyu kajaribu kumvisha Mwalimu Taswila hiyo uliomba kujua Mkuu.Mambo mengine yanatokea kwa sababu [It happen for a reason]

Huyu msanii ama alikuwa ameangalia movie ya AVATAR kabla ya kumchora Nyerere au kama alifanya hivyo kabla ya Movie hiyo kutoka anatakiwa kudai copy right kutoka kwa watayarishaji wa movie.
 
Huu sasa ndiyo unaitwa ubishi!!!!!!

Jamaa labda anaasili ya wakinga au waha.. Anataka kutuambia magazeti pia yalikuwa hayapo mmh mbona pc za magwanda zipo mim nazadhan watu wa maelezo watu saidie! Ila naweza kuanza kuamin kuwa Ticha alijua kuwa ndan ya CCM kumejaa, wanafiki, walafi, wezi, waasiojali kwao kazi yao kubwa ni kuhangaikia matumbo yao... Alijua kuwa hakuwa na mwanafunzi hata mmoja ndiyo maana wamebaki kuimba ujamaa huku kila siku wanaiba mali za wanyonge na kujitajirisha wao na watoto wao.
 
Nyerere alikuwa anavaa Kombati za Khaki, Ndiyo maana enzi zetu tulibatiza mgambo kuwa 'mgambo wa Nyerere'. Kuvaa kijani na njano leo hii unaonekana kama unajipendekeza kutaka ulaji fulani. We angalia watu wengi wanaovaa kijani wanavaa kulinda matumbo yao. Maana wataonekana si makada wazuri, na ukiangalia siasa za Gotcha za CCM lazima ujipendekeze. Kama si kwa maneno basi kwa mavazi ili uonekane mwenzao.

Nyerere alikuwa hana haja ya kujipendekeza kwani ilikuwa ni mwendawazimu pekee atakayeweza kutofautisha CCM na Mwalimu( I mean CCM ya Mwalimu, siyo CCM ya Wachumia tumbo ya leo). Ukiona chama cha siasa kinaanza kutumia nguvu nyingi kuhakikisha kinabaki madarakani ujue waliomo humo ni wachumia tumbo. Wangekuwa ni wajenga nchi wangeenda kwenye chama kinachokubalika na wananchi ili kupata nguvu ya pamoja toka kwa wananchi katika kujenga taifa.

nyerere hakuwa rais wa ccm,alikuwa wa watanzania,wenye chama na wasio na chama,thus why hakuona umuhimu wa kuvaa kijani kwa sana.
 
mchumia Juani ulia Kivulini, CCM wamechuma na Kuchuna wananchi wake tumebaki mifupa wao wakinenepeano hovyo mfano wa mwanakwaya Komba lakini waliokwenye mapambano ya kuondoa ukoloni mambo sasa wa wahindi na maakida wao kama EL na Chenga wakiwa wamevaa magwanda kwa ukombozi kamili.
 
mchumia Juani ulia Kivulini, Kivuli ni rangi ya Kijani ,CCM wamechuma na Kuchuna wananchi wake tumebaki mifupa wao wakinenepeano hovyo mfano wa mwanakwaya Komba lakini waliokwenye mapambano ya kuondoa ukoloni mambo sasa wa wahindi na maakida wao kama EL na Chenga wakiwa wamevaa magwanda kwa ukombozi kamili.
 
attachment.php

Nimekutana na hii kwenye makitaba yangu!
 

Attachments

  • Photo100101_299.jpg
    Photo100101_299.jpg
    335 KB · Views: 1,231
CCM wameanza kuitambulisha rangi za kijani na njano mwaka 1985 muda ambao Nyerere aling'atuka madarakani. Sasa ulitaka umuone wapi amevaa nguo za njano?

Lakini wakati huo alikuwa bado mwenyekiti wa CCM kama sikosei alimuachia Mzee Mwinyi uenyekiti mwaka 1987. Kwahiyo kama yalianzishwa mwaka 1985 kwanini hakuvaa huo ndio mjadala
 
Nadhani umenielewa vizuri kukujulisha kuwa CCM walitambulisha rasmi rangi za kijani mwaka 1985. Ni kweli kuwa Nyerere aliendelea na uenyekiti wa chama hadi mwaka 1987, lakini uelewe kuwa kipindi hicho vyombo vya habari kama TV havikuwepo kiasi cha kutotambua kuwa Nyerere amevaa nguo gani muda gani.

TVZ(visiwani) ilikuwepo tena ilikuwa ya rangi na picha za rangi zilikuwepo na kwa upande wa bara kulikuwa na taasisi ya vielelezo ambayo (makao makuu yake ndio ofisi za TBC sasa hivi) ilkuwa ina hifadhi picha za video za matukio ya chama na serikali kwa wakati huo ukiona tbc wanaonyesha picha za matukio ya zamani picha zake wamezitoa kwenye taasisi hiyo.
 
mavazi ya rangi ya njano na kijani yalivaliwa mioyoni mwa wakulima na wafanyakazi enzi za mwalimu ambao walikuwa na imani na chaqma na chama kilikuwa kwa ajili ya kuwatetea wanyonge. ila leo imani inalazimishwa kupitia mavazi ya nje ili kuwashawishi watu waendelee kuamini kuwa bado wapo wengi kwa kuona idadi ya watu wenye njano na kijani! hata hivyo wakati huu ukiona mtu ana vazi na nembo yoyote ya ccm ujue ameshapewa posho kwa ajili ya kuwa bango la chama.
 
Wana JF hata mimi kwa umri wangu huu takribani miaka 41 sikuwahi kumuona Mwl Nyerere amevaa hizo kijani wala Njano ambazo leo ni alama ya ufisadi,unafiki,kujipendekeza,uzandiki,ulafi,ubinafisi,wizi wa mchana,rushwa,kutokuwa na huruma na mwanadamu mwenzio,uongo pamoja na mengine yote maovu yanayotendeka kwa mgongo wa chama tawala chenye uzoefu wa ufisadi na kutunisha magamba.
Jamani mwenye hata picha moja isiyochezewa atuwekee tuione,au mwenye taarifa zaidi tuhabarishane.
 
Back
Top Bottom