Katika pitapita yangu maeneo ya katikati ya mji nilishtuka nilipokuta uzio uliokuwa umewekwa kwa ajili ya kuwezesha ujenzi wa jengo la Mfuko wa Mwalimu Nyerere ukiwa umeondolewa na eneo hilo likiwa limebaki na vichaka pamoja na lundo la kifusi.
Swali nililogubikwa nalo ni kama mradi huo umesitishwa ama ndiyo mwisho wa Mfuko wa Mwalimu Nyerere!!!
hivi hawa jamaa wa Nyere foundation wana chochote wanafanya au wanganga njaa tu. naomba kujua programs zao na jinsi zinavyoimplementiwa. sina hakika sana na kama kuna kitu wanafanya.
Sijawahi kuona hata kwenye TV kitu chochote kinachohusinana na mfuko huu. kama tunavyoona kwa Reginald Mengi.
Jengo lililotakiwa kujengwa ndani ya kiwanja hicho, lilizuiliwa na serikali, kwa maelezo kuwa, jengo lenyewe ni refu sana na liko karibu na ofisi ya rais (ikulu)