Mwalimu Nyerere ametukanwaje hasa?

Siko tayari kutukana, ila jua kua maneno aliyoyasema hakustahili kuyasema dhidi ya Nyerere.

ndugu bado upo zama zile za zidumu fikra za mwenyekiti!.kwa maelezo yako unaonekana mshabiki kama wale wasio na hoja kwenye bunge la katiba,wamebaki tu kusema mara ooh tumeoana sababu ya serikali mbili na muungano,nimezaa huku ilhal mimi ni wa upande ule,swali hakuna wazungu,waarabu,wachina nk waliooa au kuolewa hapa?,au nao nchi zao zimeungana na tz?.hebu jitafakari achana na siasa nyepesi.
 
Ndipo tunapokosa direction kama taifa iwapo sifa ya kisiasa ni kumwaga matusi tu.

Nyerere aliandika kitabu "tujisahihishe"
kwa mintaarafu wali/alikosea, tunapoyataja makosa yake hatumdhalilishi, wala hatujamtukana.

ikiwa unadhani Nyerere ametukanwa basi nakujulisha kuanzia sasa ujue Nyerere amejitukanisha.

Nyerere ametudanganya kuhusu UJAMAA NA KUJITEGEMEA.
Nyerere ametudanganya kuhusu AZIMIO LA ARUSHA.
 
kweli nimeamini watu wanafuata upepo ila sio uhalisia wa hoja, basi mpelekeni mahakamani kama alimtukana nyerere
 

Thibitisha pasipo shaka hapa jukwaani, ni kweli kwamba ktk maisha ya uongozi wa mwalimu hakuwahi kusema uongo?
 

kwa upande mwingine kumbe tafsiri ya msikilizaji inaweza kufanya hayo maneno kuwa matusi ama la,sasa basi ili kumuaminisha mwingine aamini unachoamini ni kumshawishi kwa hoja na mifano au nukuu toka ktk hayo maneno,tukirudi kwa lissu ninyi mnaoamini kuwa ametukana tunaomba nukuu ya yale unayoamin kuwa ni matusi ili tukikubaliana nanyi tuungane ktk kumkemea bwana lissu,lakini kinyume na hayo tutaendelea kuamini kuwa hizo ni siasa za majitaka ambazo hazina nafasi leo.
 
Siko tayari kutukana, ila jua kua maneno aliyoyasema hakustahili kuyasema dhidi ya Nyerere.

We naona hujailewa mada hebu ongelea ni maneno gani yaliyotolewa na tundu kumtukana nyerere na sio kubakia tu ati kamtukana..
 

Acha kwenda nje ya mada hebu ongelea maneno ya matusi yaliyotolewa na tundu na kwani nyerere hawezi kuwa mwongo au unadhani yale yote yaliyotolewa naye yalikuwa ya kweli.???
 
kama maneno gani kwa mfano hayakumstahili Baba wa Taifa na yalimstahili nani?
 
kwa mada hii,wanapropaganda wameshikwa pabaya.tajeni sasa.msikariri kama kasuku
 

Je ulimsikia Lisu kwa masikio yako?nirudi kwenye hoja yako, defamation unayosema ni Sawa. Lkn with evidence kwamba aliwahi kusema uongo bado mtu huyo atakuwa convicted?
Watu wengi tunaongozwa na mapenzi ya kumpenda Nyerere, hata mimi ni namkubali sana , lkn siamini hata kidogo kwamba hakuwahi kusema uongo,
 

Kwani MWONGO ni tusi???
 

TUNDU LISSU namfananisha na "tanganyika jeki"
sifa kuu ya hii jeki ni kuwa hunyanyua gari pamoja na mzigo wake.

JK alinyanyuliwa pamoja na mizigo ya majaji wake.
Nyerere kanyanyuliwa na mizigo ya uongo wake.

Jk aliteua baadhi ya majaji ambao hawakuwa na sifa za uteuzi ndio maana kuna baadhi ilibidi wajiunge open university kuchukua LLB ili wakidhi matakwa ya sheria waliyokwisha ikiuka. "tanganyika jeki imewanyanyua"

Huyu Nyerere sasa kanyanyuliwa juu zaidi muuone uongo wake, kwa kuthibitisha uongo wake jiulize,
uko wapi ujamaa na kujitegemea!!!!!
Liko wapi azimio la arusha!!!!!!

muungano nao magumashi.

Msipanick huu ni ukweli hamkuujua kabla.
 

Kama hakuwa mungu ni lazma akosolewe kwan nyerere jaman aliumbwa tofauti na binadamu wengne shida yote ya muungano tunaipata ni kwasababu waasisi wa muungano hawakuwa wazi
 
Hoja hapo ni kutaja hayo matusi kwani ccm mumezoea uzushi mpaka sasa muko makanisani kueneza kwamba serikali tatu jeshi litapindua nch basi bola tupinduliwe na jeshi kuliko kutawaliwa na ccm
 
Umenena mkuu, lakini umemsahau pia Lyatonga Augustine Mrema mzee wa Kiraracha ambaye aliimarisha usafi wa jiji la DSM na kuleta vivuli vya miti na pavements katikati ya jiji kwa amri ya siku 7, ingawa fadhila za JK zimemfanya aonekane kutikiswa siku hizi kimsimamo na kuegemea lolote la ccm hata bila kuchuja kama zamani. mnyonge myongeni lakini haki yake mpeni. Kaifanyia nji hii mambo mengi sana mazuri ambayo hapaswi kusubiri afe ndo tumsifu.
 
Haya Matusi kwa Nyerere hamuyaoni?muungano sasa umevurugwa Zanzibar imekuwa Nchi bila lidhaa ya Watanganyika, hili ni Tusi kubwa kwa Nyerere kwani Muungano aliotuachia ulikuwa ni kuelekea Kuwa na Serikali moja na Kuwa Taifa moja,Matusi yapo mengi sana ,huu Ufisadi ,rasilimali kutoroshewa nje ya Nchi,Uwekezaji wa kimagashi,Tamaduni zetu na Maadili kuporomoka kwa kasi Haya ni matusi kwa Nyerere , Siku hizi imekuwa ni Kawaida Vijana kuvaa Nguo chini ya makalio imekuwa kawaida hata wanawake wanavaa nguo za utata Hakuna wa kuthubutu kuwakemea , haya ni matusi makubwa kuliko hayo ya Lisu.
 
Nyerere Kama binadamu wengine alikuwa na Mapungufu yake japo si mengi sana kuliko Mazuri aliyofanya,tuendelee kumpongeza kwa Mazuri yake Pia isiwe dhambi kuyakosoa Mabaya kisha kumsamehe na kumwacha apumzike kwa Amani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…