Mwalimu Nyerere Aliiogopa CCM - Prof. Mbele

Mtumbatu

JF-Expert Member
Joined
Apr 27, 2012
Posts
363
Reaction score
171
Ingawa alikuwa mwanzilishi wa CCM, kwa nia njema ya kuendeleza mapinduzi katika nchi yetu, miaka ilivyozidi kwenda Mwalimu Nyerere alishuhudia jinsi CCM ilivyobadilika na kuwa mzigo kwake na pia tishio kwa usalama wa Taifa.

Mwaka 1993 Mwalimu alichapisha kitabu kiitwacho Uongozi Wetu na Hatima ya Tanzania (Harare: Zimbabwe Publishing House, 1993). Pamoja na mambo mengine katika kitabu hiki, Mwalimu alisema kuwa kuna kansa katika uongozi wa CCM. Nanukuu baadhi ya maneno yake:

Chama cha Mapinduzi, kwa sababu ya uzito wa historia yake, hadhi ya jina lake, mfumo wa wavu wake, mazoea ya watu, na ubovu wa Vyama vya Upinzani, kinaweza kuchaguliwa na Watanzania, pamoja na kansa ya uongozi wake. Au watu wanaweza wakachoka, wakasema, "potelea mbali:" wakachagua Chama cho chote, ilimradi tu watokane na kansa ya uongozi wa CCM. Hainifurahishi kuyasema haya, lakini uhai wa Nchi yetu unataka yasemwe. (Ukurasa 61)

Mwalimu hakuishia hapo, bali aliongezea namna hii:

Nilisema awali kwamba kansa ya uongozi ndani ya Chama cha Mapinduzi isingekuwa ni jambo la kutisha sana kama tungekuwa tumeanza kuona Chama kizuri cha upinzani kinachoweza kuiongoza Nchi yetu badala ya CCM. Ubovu wa uongozi ndani ya CCM ndio uliofanya nikapendekeza tuanzishe mfumo wa Vyama Vingi.
Nilitumaini kuwa tunaweza kupata Chama kingine kizuri ambacho kingeweza kuiongoza Nchi yetu badala ya CCM; au ambacho kingekilazimisha Chama cha Mapinduzi kusafisha uongozi wake, kwa kuhofia kuwa bila kufanya hivyo kitashindwa katika uchaguzi ujao. Lakini bado sijakiona Chama makini cha upinzani; na wala dalili zo zote za kuondoa kansa ya uongozi ndani ya CCM. Bila upinzani mzuri wa nje, na bila demokrasia halisi ndani ya Chama cha Mapinduzi, Chama hiki kitazidi kudidimia chini ya uzito wa uongozi mbovu. Kwa hali yetu ya kisiasa ilivyo nchini hili si jambo la kutarajia bila hofu na wasi wasi! (Ukurasa 66)

Source: wavuti.com - wavuti
 
Hofu ya Nyerere angekua hai leo ingekua imeondoka. Tayari kipo chama mbadala kwa ccm wakati ccm imekamilika kua chama cha kutetea wanyonyaji. Sera ya ujamaa na kujitegemea washaitupa iko kapuni.
 
Rais anaweza toka chama chochote lakini Rais bora atatoka Ccm- Mwl Nyerere haya maneno kayatamka 1995 wakati kitabu katunga 1993 ikimaanisha Chama kilishajirekebisha!
 
Wacha mzaha Songoro! Nyerere angefufuka leo aione ccm angekufa kwa uchungu.
 
Rais anaweza toka chama chochote lakini Rais bora atatoka Ccm- Mwl Nyerere haya maneno kayatamka 1995 wakati kitabu katunga 1993 ikimaanisha Chama kilishajirekebisha!

Mwalimu pia aliweka angalizo: Kama CCM kitashindwa kuhudumia maslahi ya Watanzania, watatafuta uongozi bora kutoka chama kingine.
 
Rais anaweza toka chama chochote lakini Rais bora atatoka Ccm- Mwl Nyerere haya maneno kayatamka 1995 wakati kitabu katunga 1993 ikimaanisha Chama kilishajirekebisha!

Hapana...hata mwalim alikua na hulka ya ombwe la uongoz,alikula matapishi yake..ndo maana ya neno siasi

Lkn turud ktk kitabu na mawazo yake,wazo la mwalim alikua anajua kbsa tanzania vyama vingi vimeanza 92,kwa maana yyte lazma wengi walikua ccm japo kinafki!!
Lkn kumbuka hata nyerere ni mwana wa adam,anakosea hivyo neno lake cyo biblia wala msaafu
 
Ingawa alikuwa mwanzilishi wa CCM, kwa nia njema ya kuendeleza mapinduzi katika nchi yetu, miaka ilivyozidi kwenda Mwalimu Nyerere alishuhudia jinsi CCM ilivyobadilika na kuwa mzigo kwake na pia tishio kwa usalama wa Taifa.

Mwaka 1993 Mwalimu alichapisha kitabu kiitwacho Uongozi Wetu na Hatima ya Tanzania (Harare: Zimbabwe Publishing House, 1993). Pamoja na mambo mengine katika kitabu hiki, Mwalimu alisema kuwa kuna kansa katika uongozi wa CCM. Nanukuu baadhi ya maneno yake:

Chama cha Mapinduzi, kwa sababu ya uzito wa historia yake, hadhi ya jina lake, mfumo wa wavu wake, mazoea ya watu, na ubovu wa Vyama vya Upinzani, kinaweza kuchaguliwa na Watanzania, pamoja na kansa ya uongozi wake. Au watu wanaweza wakachoka, wakasema, "potelea mbali:" wakachagua Chama cho chote, ilimradi tu watokane na kansa ya uongozi wa CCM. Hainifurahishi kuyasema haya, lakini uhai wa Nchi yetu unataka yasemwe.(Ukurasa 61)

Mwalimu hakuishia hapo, bali aliongezea namna hii:

Nilisema awali kwamba kansa ya uongozi ndani ya Chama cha Mapinduzi isingekuwa ni jambo la kutisha sana kama tungekuwa tumeanza kuona Chama kizuri cha upinzani kinachoweza kuiongoza Nchi yetu badala ya CCM. Ubovu wa uongozi ndani ya CCM ndio uliofanya nikapendekeza tuanzishe mfumo wa Vyama Vingi.
Nilitumaini kuwa tunaweza kupata Chama kingine kizuri ambacho kingeweza kuiongoza Nchi yetu badala ya CCM; au ambacho kingekilazimisha Chama cha Mapinduzi kusafisha uongozi wake, kwa kuhofia kuwa bila kufanya hivyo kitashindwa katika uchaguzi ujao. Lakini bado sijakiona Chama makini cha upinzani; na wala dalili zo zote za kuondoa kansa ya uongozi ndani ya CCM. Bila upinzani mzuri wa nje, na bila demokrasia halisi ndani ya Chama cha Mapinduzi, Chama hiki kitazidi kudidimia chini ya uzito wa uongozi mbovu. Kwa hali yetu ya kisiasa ilivyo nchini hili si jambo la kutarajia bila hofu na wasi wasi! (Ukurasa 66)

Source: wavuti.com - wavuti

maneno murua kwa Watanzania! yaani maneno yanayoishi haya!! CCM na vyama vya Upinzani ...you all serving this.....
 
Ubovu wa uongozi ndani ya CCM ndio uliofanya nikapendekeza tuanzishe mfumo wa Vyama Vingi.
aisee kweli Mwalimu aliona mbali, kumbe sababu kubwa na kuanzishwa vyama vingi ilikuwa ni hii, watu wengi pamoja na mimi hatukulijua hili.
 
Kwani ubovu wa ccm umekwisha? mii naona naona ndio kwanza unashika kasi ya ajabu.
 
Rais anaweza toka chama chochote lakini Rais bora atatoka Ccm- Mwl Nyerere haya maneno kayatamka 1995 wakati kitabu katunga 1993 ikimaanisha Chama kilishajirekebisha!

Weka uthibitisho hapa umenukuu kutoka wapi?sio kuja uozo wako hapa.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom