Mwalimu Mkuu wa shule ya Sekondari mbaroni akidaiwa kuomba rushwa ya ngono kwa Mwanafunzi

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,445
3,403
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Mkoa wa Dodoma, inamshikilia Mkuu wa Shule ya Sekondari Serengeti wilayani Serengeti mkoani Mara, Baraka Sabi kwa kosa la kutaka rushwa ya ngono kwa aliyekuwa mwanafunzi wa shule hiyo.

Mkuu wa Taasisi hiyo Mkoa wa Dodoma, Sosthenes Kibwengo leo Desemba 15, 2019 Jijini hapa amewaambia waandishi wa habari kuwa mtuhumiwa huyo alitaka rushwa ya ngono kama sharti la kumpatia mtoa taarifa cheti chake cha kuhitimu kidato cha sita.

Kibwengo amesema kuwa mtoa taarifa alikuwa akiwasiliana na mtuhumiwa ili kupata cheti hicho, ambapo mwalimu huyo alishauri aje na cheti hicho kwani ana safari ya kuja Dodoma kuhudhuria mkutano wa wakuu wa shule za sekondari ili kumpunguzia gharama za kusafiri hadi shuleni.

Amesema mtoa taarifa aliwaambia kuwa baada ya kufika ili kuchukua cheti chake mwalimu huyo alihitaji kupewa rushwa ya ngono ili atoe cheti ambapo mtoa taarifa aliomba udhuru na kuahidi kurejea siku uliyofuta.

"Desemba 12, 2019 tulipokea taarifa kutoka kwa msichana (jina limehifadhiwa) mkazi wa jiji la Dodoma ambaye alihitimu kidato cha sita katika shule hiyo mwaka 2016 na kwamba mtuhumiwa amemtaka kingono ili mpatie cheti kwa ajali ya maombi ya ajira baada ya kuhitimi chuo kikuu," amesema Kibwengo.

Amesema baada ya kupokea taarifa hiyo waliweka mtego na kufanikiwa kumkamata akiwa na mtoa taarifa kabla yakufanya tendo hilo.

Amesema Takukuru walifanikiwa kuchukua cheti hicho na uchunguzi wa awali unaendelea kwa mujibu wa sheria na hatua stahiki zitachukuliwa baada ya kukamilika.
 
Labda sababu huko mikoani mademu ni wa kubahatisha...huko mkoani hata ukitongoza demu wa mtu mwenye demu anaweza hata kukutoa roho...
 
Mambo za kulipizana visasi hayo. Hata hao Taakukuu nadhani ni wabaya sana. Kuaibshana namna hii hakufai kabisa. Lisichana lizima limeyaweka moyoni maviboko lililambishwa sekondari na mwalim leo limepata mwanya wa kumwadhibu mwalimu wa watu!!!
Dah! Madhambi mengine ya hovyo kabisa. Taakukuu nanyi fikirini kidogo. Rushwa ya ngono inakuwaje?? Yaani huyu teacher alimuahidi kumwibia cheti cha mwingine?? Kumuambia nakuja Dom kwenye kikao nitakuletea usiharibu nauli imekuwa noma??
Mwanamke huyu, nasema ni mchawi kabisa. Simjui huyo mwalimu ila nasema; Kaonewaaaaaa
 
TAKUKURU Mkoani Dodoma wanamshikilia Mkuu wa Shule ya Sekondari Serengeti iliyopo Serengeti Mkoani Mara, Baraka Sabi kwa tuhuma za kuomba rushwa ya ngono kwa Mwanafunzi aliyemaliza kidato cha sita katika shule hiyo ili ampatie cheti chake cha kuhitimu.

Kamanda Wa Takukuru Mkoa wa Dodoma Sosthenes Kibwengo amesema wamemkamata Mwalimu huyo kwa kushirikiana na mwanafunzi huyo Mkazi wa Dodoma ambaye alihitimu Serengeti Secondary Mwaka 2016 na alikuwa anataka cheti ili aombee kazi, ambapo waliweka mtego na kufanikiwa kumkamata Mwalimu huyo akiwa chumbani.

“Mwalimu Baraka alimwambia Mwanafunzi asipate shida ya kwenda Serengeti kwakuwa yeye ana safari ya kuja Dodoma kwenye Mkutano wa Wakuu wa Shule za Sekondari na atakuja na cheti hicho, ajabu Mwanafunzi amekifuata cheti akaombwa rushwa ya ngono, yule Msichana akajiongeza kwa kuomba udhuru na kuahidi kurejea kesho yake na akatupa taarifa”

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbinu za kupangua kesi kwako Mwalimu....
Komaa kwamba huyo denti ambaye amekwisha maliza six kwamba ulimtongoza....
ni mtu mzima huyo alafu ni raia tayari.....
uthibitisho ni hicho cheti....
na pili aliahidi kukupa tunda siku inayofatia ndio maana alikuja gest....
Hakuna kesi hapo.....
unless huyo dem angekuwa ni mwanafunzi wa secondary bado.
 
Back
Top Bottom