Mwalimu Mkuu kaeleza changamoto za shule, kapata misaada, kashushwa cheo

Kkimondoa

JF-Expert Member
May 31, 2014
4,453
4,933
Tanzania ni nchi ya ajabu sana tena sana, kuna Mkuu wa shule Iringa huko shule ya msingi Kibonzile( sina hakika na jina la shule na wilaya) kashushwa cheo kwa kosa la kuziongea changamoto za shuleni kwake.

Baada ya kuziongea wahisani wakajitokeza na kutoa misaada ya ukarabati.

Lakini katika hali ya kushangaza na ujinga wa baadhi ya viongozi tulio nao mwana mama huyo ameshushwa cheo eti amekiuka taratibu za utumishi na Afisa Elimu anajisifu kwa ujasiri kabisa, mbona swala la madawati liliongelewa kwa uwazi?

Mamlaka husika mmulikeni Afisa Elimu wa wilaya hiyo anayemuadhibu mwalimu kwa kuwa mkweli kueleza changamoto za shule yake ili ipate kurekebeshwa na kweli wahisani wamejitolea kusaidia shule hiyo.

HUU NI UNYANYASAJI AFISA ELIMU HUYO ANATUMIA VIBAYA MADARAKA YAKE.
 
mada yako nimeipenda ila jaribu kuedit baadhi ya maneno ili ikae vizuri.

kwa ufupi watawala wako hivyo. wanataka wao ndo waseme kujiletea misifa kibao. usishangae wakaja na kauli kuwa huyo mama anatumiwa na Msigwa (chadema). akiongea kitu Lissu hawawezi tekeleza kwa sababu ni mpinzani, lakini akiongea Diamond au Mrisho Mpoto au Shilawadu hao mpaka bosi utasikia kawaalika Ikulu.

wivu, visasi, kukomoana, ndo vimewajaa vichwani.
 
Mm huwa nikiona malalamiko ya walimu sipati huruma dhidi yao. Hawa ndiyo watu wanao ikumbatia ccm. Huwa wanatumika vibaya wakati wa uchaguzi.

Lkn pia kwa wingi wao ktk nchi hii miongoni mwa watumishi wa umma wangeweza kuishinikiza serikali kuboresha maslahi yao. Lkn kila siku wao ni kulialia tu.

Diwani, mkurugenzi na wakuu wa wilaya wakitaka kuonekana wanafanya kazi wanamnyanyasa mwalimu.

Tatizo kubwa walimu wengi walifeli, ndiyo maana hawajiamini. Sifa ya kuwa mwalimu lazima ufeli kwanza.
 
Huyo mwalimu wa S/m Kibonzelo ktk Manispaa ya Iringa ni SHUJA,MWADILIFU NA MZALENDO.Watanzania tuungane kupinga na kupiga vita watumisha wa umma ambao wanarudisha nyuma maendeleo.Huyo Afisa Elimu aliyemshusha cheo mama huyo AFUKUZWE KAZI MARA MOJA.Huyo mama arudishwe kwenye cheo chake cha mkuu wa shule mara moja. Maafisa elimu wengi ni FEKI.Wana wivu sana pale wanapoona mwalimu fulani anafanya vizuri. Kanuni gani za utumishi wa umma? Mimi ni mwanasheria na nimespecialize kwenye Labour Law. Hiyo kanuni haipo. Huyo afisaelimu ni MWONGO. Pili, kitendo hiki ni unyanyasaji dhidi ya wanawake. Ombi:Mhesh.Kabati tunakuamini.Fanya juu chini mama huyu urudi kwenye cheo chake.Huyu ni mama wa kuigwa.Mhesh.Simbachamwene na Jaffo wananchi tunaomba haki itendeke dhidi ya dhuruma na uonevu huu dhidi ya wanawake.
 
Mm huwa nikiona malalamiko ya walimu sipati huruma dhidi yao. Hawa ndiyo watu wanao ikumbatia ccm. Huwa wanatumika vibaya wakati wa uchaguzi.

Lkn pia kwa wingi wao ktk nchi hii miongoni mwa watumishi wa umma wangeweza kuishinikiza serikali kuboresha maslahi yao. Lkn kila siku wao ni kulialia tu.

Diwani, mkurugenzi na wakuu wa wilaya wakitaka kuonekana wanafanya kazi wanamnyanyasa mwalimu.

Tatizo kubwa walimu wengi walifeli, ndiyo maana hawajiamini. Sifa ya kuwa mwalimu lazima ufeli kwanza.
Ndio maana via vyako vya uzazi havifanyi kazi,,
Mwalimu ndo kakufikisha hapo ulipo hata kuweka tuvidole vyako hapo kwenye kasim kako ni mwalimu..
Kwa nini usipate laana???
Leo umejua kusoma,kuandika kisha unaropoka eti walimu walifeli.
Mfyuuu.....
 
Amemdhalilisha dereva wa LORI. Ni afadhali angekaa kimya huku watoto wakiendelea kuelimika katika mazingira magumu kuliko kuzitangaza shida zilizoko hapo shuleni na hivyo kumharibia sifa dereva wetu wa LORI.
 
Mkuu miafisa Elimu mingi ni mijitu isiyojielewa na watu wanaotoa vyeo kwa kujuana na rushwa.Katika mashule mengi vyeo vimetolewa bila kuzingatia elimu ya mtu bali kwa kujuana na rushwa.
Wengi hawana uelewa hata WA mambo ya msingi katika uendeshaji WA mashule.wengi wamewekwa baada ya kununua nafasi hizo.tshs 7000000 tayari unaukwaa uafisa elimu.wahusika wafanye uhakiki WA maafisa elimu kuangalia walifikaje katika nafasi hizo.Wengi hawana uelewa wanafanya kazi kwa maigizo ,hawana ubunifu...
 
aache kiherehere ,anahangaikia msaada kwani shule yake? kuna mtu kamuambia watawala wanataka watoto wapate elimu nzuri/ thubuutuuu,we fundisha hayo maandazi yakimaliza yakawe machangudoa na mapanya road,watoto wa watawala wako Canada,Uk na US wanapiga kitabu wakirudi huku wanakuja kuchukua nafasi za baba zao
 
Hii habari nimeisikia Radio Free Africa, Hiyo shule inaitwa Kigonzile ipo manispaa ya Iringa. Kitendo kilichofanywa na huyo afisa elimu siyo cha kiungwana tunatakiwa kupaza sauti kukilaani pia mamlaka za uteuzi zimchukulie hata Kali Huyo afisa.
 
Ndio maana via vyako vya uzazi havifanyi kazi,,
Mwalimu ndo kakufikisha hapo ulipo hata kuweka tuvidole vyako hapo kwenye kasim kako ni mwalimu..
Kwa nini usipate laana???
Leo umejua kusoma,kuandika kisha unaropoka eti walimu walifeli.
Mfyuuu.....
Mkuu mfumo wetu wa kuwapata walimu ndiyo uko hivyo mkuu. Tena kama walimu wa s/m ndiyo usiseme kabisa asilimia kubwa wana vyeti vya marehemu ama wamebashite.
 
Dereva wa Lori hataki msaada halafu wewe mwalimu unaomba msaada ujue kuwa hataki kulemba!!!kukaa kwenye Lori lazima uwe na roho ngumu hakuna cha mbavu za mbwa wala bumps vumilieni tu tutafika.
 
Taarifa hii imenisikitisha sana.
Kweli, huyo mwalimu amekuwa shujaa, hakika anastahili pongezi, heshima na kuthaminiwa sana na jamii, na nchi.

Mwalimu, huyo ni kiongozi, ni mahili, makini , mzalendo, mpambanaji, mmuwajibikaji yaani amesheheni sifa na vigezo vyote vya kuitwa Shujaaa. Ni mwanamke anastahili kupewa hata nafasi ya Uafisa Elimu hata ngazi ya Mkoa!!

Kwa sababu, viongozi wengi wa sekta hiyo ya elimu waliopo hawajielewi , hawaelewi wafanye nini , ni vilaza

Yaani, viongozi wengi wa sekta ya elimu ni tatizo sana.
 
Wa kuchunguzwa alifikaje pale si huyo afisa elimu tu Bali hata ule mtungi wa kusajili siasa!
 
Back
Top Bottom