Mwalimu kufungwa miaka 2i jela.

houseboy

Member
Joined
Jul 22, 2007
Posts
39
Reaction score
3
Jamani wanajamii naomba tujiunge pamoja kumsaidia Rachel,naona adhabu aliyopewa ni kubwa sana na ukizingatia kuna hadi mawaziri wana vyeti feki na wanapeta mtaani,sitetei makosa ya mwalimu lakini hii ni mbaya sana,invisible naomba ufatilie hili,Mwanakijiji kaanzi inabidi katembelee mahakamani hii noma tupu.FREE RACHEL.
 

Eleza vizuri kosa alilofanya hadi kufungwa jela kabla ya kuzungumzia kutetewa , isije kuwa ni yule mwalimu aliyembaka mwanafunzi kipofu halafu unataka wana JF wamtetee
 
No mchizi mwalimu Rachel kafoji vyeti,ni kweli katenda kosa ila miaka 21 ni adhabu kali sana.mbona wakina nanii wapo huru na mivyeti yao ya kuchonga?
 
No mchizi mwalimu Rachel kafoji vyeti,ni kweli katenda kosa ila miaka 21 ni adhabu kali sana.mbona wakina nanii wapo huru na mivyeti yao ya kuchonga?

wewe unahisi miaka mingapi ndio stahili kwa kosa hilo?
 
BigMgeni kosa kama ilo mi nadhani ni chini ya mwaka jela na kufukuzwa kazi.kwa maelezo zaidi nenda kwenye dailnews la leo .HELP TO FREE HER.
 
Kweli hiyo miaka mingi sana,angefungwa miaka isiyozidi miwili .Hapa wangeangalia unyeti wa kazi yenyewe aliyofojia vyeti kama ingegharimu maisha ya binadamu au la kama vile kufoji kazi ya udaktari,lakini pia bado kisingekuwa kifungo kirefu hivyo.Kuna hukumu kama hiyo ya jamaa mmoja aliyefoji vyeti vya chuo kikuu kwamba amehitimu shahada ya sheria,akapangiwa kazi ya uhakimu Arusha,jamaa walimfunga miaka miwili tu.hata yule daktari feki wa dodoma(a.k.a darasa la tatu) alifungwa miaka nadhani 3.Tatizo ni mahakimu wetu mara nyingi hukumu zao ni atakavyojisikia,na sikufuata vifungu vya sheria.
 
:A S 13: Katika watu wasio na mwono angavu ni huyo Mwalimu RECHO. Unafoji vyeti vya ualimu kazi ambayo hailipi
kila mtu anaikimbia then wewe unaikimbilia. My point is kazi ya elimu haina mshahara wa kutosha kusimama mahakamani
na mahakimu wetu hasa kwenye hizi mahakama zetu zilizo tawaliwa na harufu ya rushwa na ufisadi wa kutupa.
-Pole RACHEL Nasikitika kuipoteza kura yako.
 

Aliona ndiyo atayopata kazi haraka tofauti na kazi nyingine.Ila kwa kweli inabidi akate rufaa, adhabu aliyopewa ni kubwa kulingana na kosa lake
 
Mkuu tunarudi palepale tatizo ni chapaa. We mkopeshe 2ml uone kama kesho hajatoka.
 
According to The Penal Code (C.16. 2002 R.E)

sasa tuangalie ktk charge sheet yake amepigwa na kosa gani na mangapi?
nimemwaga hapo ili wenye kujua mwenendo wa ile kesi waverify kuona kama haki imetendeka au hakimu ameoverlook. Ryfaa ni haki ya kila mtu na mshtakiwa pia kama hajaridhika na hukumu dhidi yake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…