Mwalimu huyu wa St.Cornelius.. Mhhh!

Mwalimu huyu wa St.Cornelius.. Mhhh!

Tusker Bariiiidi

JF-Expert Member
Joined
Jul 3, 2007
Posts
5,554
Reaction score
2,160
Mwalimu huyu wa St.Cornelius aitwaye Baba G,ana matatizo gani? Kwanini anaonea watoto wetu namna hii yaaani anaudhi sana...anawapiga watoto wa wetu wa kike bila sababu... Kuna kipindi alishawahi kupigwa sana na mdada mmoja aliyebatizwa jina la "John Cenna" kisa akutaka binti yake aende kutibiwa...
 
Mwalimu huyu wa St.Cornelius aitwaye Gordian Bwemelo,ana matatizo gani? Kwanini anaonea watoto wetu namna hii yaaani anaudhi sana...anawapiga watoto wa wetu wa kike bila sababu... Kuna kipindi alishawahi kupigwa sana na mdada mmoja aliyebatizwa jina la "John Cenna" kisa akutaka binti yake aende kutibiwa...
Ingekuwa ni bila bold hiyo, ningesema huenda una mapenzi yaliyozidi kwa watoto!
Lakini kama huyo mwalimu anawabagua watoto wa kike na kuwatandika zaidi ya vile anavyofanya kwa wavulana, basi hapo kuna tatizo!
Kwani hanuendi kwenye mikutano ya wazazi mkampa live shida hiyo?
Kama kikweli anafanya hivyo ana malengo na madhumuni machafu!
 
Ulishafuatilia ukajua kwamba anawapiga bila sababu? Walimu tuna kazi kweli siku hizi. Hii mitoto tukiiacha inatudharau darasani, inakuwa mijinga, halafu wazazi mnatujia juu tena kwamba tumeshindwa malezi. Tukijaribu kuwarekebisha ili warudi kwenye mstari na penyewe mnatujia juu eti kwanini tunawapiga watoto wenu. Tukigeukia serikali japo ituboreshee hali zetu za kazi kwa sababu tunatumia muda wa ziada kuwarekebisha watoto wajinga, serikali inatujibu kwa kejeli. Kinachofuata tutakuwa tunaingia darasani kupiga story na watoto, hatufundishi wala nini ili japo wafeli tu tuone hii jeuri yenu ya kutulalamikia kila kunapokucha inaishia wapi?
Hebu waacheni walimu wafanye kazi zao kwa uhuru. Watu kama ninyi ndo mnaosababisha vibaka, majambazi na vyangudoa wanaongezeka mijini. Maana mnaingilia kazi za walimu ambao ndiyo wenye jukumu la kujenga na kulinda maadili ya watoto.
 
Paka Jimmy... Shule hiyo ni ya wanafunzi wa kike... Na pia kwenye vikao husika huwa haudhuriii... Nataka kumuamisha mdogo wangu...
 
Ulishafuatilia ukajua kwamba anawapiga bila sababu? Walimu tuna kazi kweli siku hizi. Hii mitoto tukiiacha inatudharau darasani, inakuwa mijinga, halafu wazazi mnatujia juu tena kwamba tumeshindwa malezi. Tukijaribu kuwarekebisha ili warudi kwenye mstari na penyewe mnatujia juu eti kwanini tunawapiga watoto wenu. Tukigeukia serikali japo ituboreshee hali zetu za kazi kwa sababu tunatumia muda wa ziada kuwarekebisha watoto wajinga, serikali inatujibu kwa kejeli. Kinachofuata tutakuwa tunaingia darasani kupiga story na watoto, hatufundishi wala nini ili japo wafeli tu tuone hii jeuri yenu ya kutulalamikia kila kunapokucha inaishia wapi?
Hebu waacheni walimu wafanye kazi zao kwa uhuru. Watu kama ninyi ndo mnaosababisha vibaka, majambazi na vyangudoa wanaongezeka mijini. Maana mnaingilia kazi za walimu ambao ndiyo wenye jukumu la kujenga na kulinda maadili ya watoto.

Huyu wa St.cornelius kazidi watoto wa kike anawapiga fimbo 13 "matakoni" huu ni unyama mkubwa sana...
 
Ameshawahi kukaribishwa Tusker baridiii. Pengine atatuliza munkali wake
 
Hebu waacheni walimu wafanye kazi zao kwa uhuru. Watu kama ninyi ndo mnaosababisha vibaka, majambazi na vyangudoa wanaongezeka mijini. Maana mnaingilia kazi za walimu ambao ndiyo wenye jukumu la kujenga na kulinda maadili ya watoto.

Sio kwa kuwatukana na kuwakanyaga SHINGO!!... Halafu Lukolo tunalipa mimilion ya kufa mtu... Lukolo ndo maana shule inakosa maadili... Kwann cio Canossa wala Green Acres?
 
Kuwaadhibu watoto kwa vipigo huchangia sana kudumaza watoto na kushusha viwango vya elimu. Upendo na adhabu mbadala vitafaa zaidi.
 
Mwalimu huyu wa St.Cornelius aitwaye Baba G,ana matatizo gani? Kwanini anaonea watoto wetu namna hii yaaani anaudhi sana...anawapiga watoto wa wetu wa kike bila sababu... Kuna kipindi alishawahi kupigwa sana na mdada mmoja aliyebatizwa jina la "John Cenna" kisa akutaka binti yake aende kutibiwa...

isije kuwa anatabia za wale maafande wa jkt wakitaka mtu/mtoto adhabu na vitisho kwa saana? by the way sheria ya kumwadhibu mtoto shuleni ina semaje? hususana mto wa kike vs mwl wa kiume?
 
Kuwaadhibu watoto kwa vipigo huchangia sana kudumaza watoto na kushusha viwango vya elimu. Upendo na adhabu mbadala vitafaa zaidi.

P upo juu... Wanadhani sisi tunachimba hela jamani... Jangwani,Zanaki etc kina Lukolo fanyeni hivyo...
 
isije kuwa anatabia za wale maafande wa jkt wakitaka mtu/mtoto adhabu na vitisho kwa saana? by the way sheria ya kumwadhibu mtoto shuleni ina semaje? hususana mto wa kike vs mwl wa kiume?

Kaka upo juu... Huyu jamaa hana maadili...
 
Fimbo ni mambo ya kizamani.. itafutwe adhabu mbadala.. sanasana kwa watoto wa kike.... mitoto wa kume bakora zibaki palepale
 
na nionavyo kama kweli mtoto amekuwa mtuku kweli kweli basi mzazi anatakiwa ataarifiwe, na ikiwezekana wapange na mwl njia za kumrekebisha iwe fimbo, kufanya homework/mazoezi kwa saana, nasa zikubaliwe na head wa shule , mwalimu wa nidhamu, mwalimu husika na mzazi pia pale panapo hitajika.
 
Sikiliza na upande wa pili mkuu hapo ndo utaweza kuamua vizuri kwamba anaonea au la!
 
Sio kwa kuwatukana na kuwakanyaga SHINGO!!... Halafu Lukolo tunalipa mimilion ya kufa mtu... Lukolo ndo maana shule inakosa maadili... Kwann cio Canossa wala Green Acres?
Watanzania tumezoea kulalamika kwa saaaana lakini hatutaki kuchukua hatua...Hili sio tatizo la kuleta hapa... Unachotakiwa kufuatilia huko shulenii.
 
Tuliosoma JKT kipindi kile,mademu nao bakora eti wanakataa mikononi kuonesha ni ngangali halafu anakuchukulia bakora bila KUFUTA wala nn tulikuwa tunaita KAMDINDISHIA teacher..ila hazikufundisha wala nn zaidi ya kuzoea mibakora na kuona ni vitu vya kawaidia tu JKT....huyo teacher awaachie JKT mibakora haina issue wala nn siku hizi...
 
Back
Top Bottom