Mwalimu Hamisi ana moyo sana?


Tumain

Tumain

JF-Expert Member
Joined
Jun 28, 2009
Messages
3,158
Likes
11
Points
0
Tumain

Tumain

JF-Expert Member
Joined Jun 28, 2009
3,158 11 0
MWONGOZO wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi unamtaka kila mwalimu kufundisha, kwa wiki vipindi, visivyozidi 28 na visivyopungua 24. Vipindi kwenye ratiba hujaa vizuri bila mgongano na wanafunzi hufaidi uwepo wa walimu.

Mwalimu yeyote anayekuwa na vipindi zaidi ya 28 huwa na mzigo mkubwa na ili kusiwe na mgongano na vipindi vya walimu wengine atalazimika kuwarundika wanafunzi wa madarasa mawili au zaidi katika darasa moja. Pia mwalimu anayekuwa na vipindi chini ya 24 hufikiriwa kuwa hatumiki ipasavyo.

Mwongozo huo unaweza kuwa unafanya kazi katika shule mbalimbali za msingi na sekondari lakini si katika shule ya msingi ya Saninga iliyoko kisiwa cha Saninga wilaya ya Rufiji mkoa wa Pwani ambako Omary Hamisi anafundisha.


Hamisi ndiye mwalimu pekee aliyeko shuleni hapo kwa hiyo anapaswa kulitendea haki kila darasa—kufundisha, kutoa kazi za kufanya nyumbani, kutoa majaribio, kusahihisha na kusimamisha shughuli nyingine kama usafi, michezo na shughuli nyingine za kujitegemea. Mwalimu Hamisi hakupenda kubaki pekee yake katika shule hiyo bali amejikuta akikimbiwa na walimu wengine waliopangwa kufundisha. Mazingira magumu ya kufanyia kazi yalioko katika eneo hilo la delta ndiyo chanzo hasa na ili aonekane anawatendea haki wanafunzi wote imemlazimu kufundisha madarasa yote peke yake.


"Nimekuwa katika wakati mgumu wa kufundisha hasa kipindi cha kwenda kwenye mishahara, kipindi cha kilimo na ninapougua kwani nalazimika kufunga shule kwa kipindi hicho," anasema Mwalimu Hamisi. Mwalimu Hamisi hawalaumu walimu wanaokimbia shule hiyo ila mazingira. "Mazingira ya walimu katika visiwa hivi hayamhamasishi mwalimu kufundisha labda serikali ione haja sasa ya kuongeza pesa za mishahara na marupurupu mengine kwa walimu wanaoletwa katika visiwa hivi," anaeleza.


Mwalimu huyo, ambaye anafundisha kuanzia darasa la kwanza hadi la saba, anasema, "Asikudanganye mtu, mazingira ya kazi ni magumu sana, ukweli nimeelemewa na mzigo wa vipindi kuanzia darasa la kwanza hadi la saba bila ya kupata msaada wowote hata kutoka katika shule jirani,"anasimulia.

Ni dhahiri pendekezo lake la kupata walimu wa msaada kutoka shule za jirani ni gumu pia kwani shule nyingine za jirani yaani visiwa vingine nako hali ni ngumu, kuna kilio kama chake.


Kwa mfano, shule za Ruma na Kiechuru zina walimu wawili wawili, Kiongoroni, Msala, Twasalie, Maparoni na Mbuchi zina walimu watatu watatu na zinazoonekana kuwa na nafuu ni Kiasi, Saalale, Nyamisati na Mchinga zenye walimu wane kila moja, Pombwe, Jaja na Kiomboni zenye walimu watano watano na yenye utajiri wa walimu ni Mfisini ambako wako sita. Lakini hakuna anayependa kwenda Saninga.


Baadhi ya walimu wanaopangwa kufundisha shule hiyo huripoti, lakini baada ya kujionea mazingira huondoka na wengine huamua kutoripoti kabisa pale anapoambiwa kituo chake cha kazi ni katika kisiwa hicho.

Halmashauri ya wilaya ya Rufiji, kwa ushirikiano na wananchi, Mwalimu Hamisi anasema imejitahidi kuboresha majengo ya shule na nyumba za walimu, lakini kinachowakimbiza ni mazingira iliko shule.


"Walimu tunaishii kwa shida sana. Nikiumwa au kupata dharura yoyote basi inabidi wanafunzi wabaki peke yao na shule inafungwa mpaka nitakaporudi," anasema mwalimu huyo huku aliyekuwa anajiandaa kwenda likizo nyumbani kwao Ikwiriri.

"Afadhali sana sasa nimetulia, lakini ungekuja hapa kati ya Januari 2009 na Septemba 2009, ungenionea huruma jinsi nilivyokuwa napata shida ya kuwafundisha watoto hawa.


Nikifundisha darasa hili wengine wanalazimika kubaki peke yao hasa madarasa makubwa," anaeleza Hamisi aliyehojiwa mwishoni mwa 2009. Wanaokimbia mazingira katika visiwa hivyo si walimu pekee bali hata watumishi wengine. Ukosefu wa huduma za usafiri, miundombinu mibovu, ugumu wa kupata mishahara, bidhaa na huduma nyingine kama za afya. "Kila kitu ukiwa huku ni shida, hata sehemu ya kununua vitu muhimu ni shida, bidhaa zinapatikana kwa gharama kubwa hivyo inabidi tugharamie kwa kukodi mtumbwi au boti.

"
Nasisitiza kwamba mazingira haya hayamhamasishi mwalimu yeyote awe wa kike au wa kiume kufundisha katika mazingira haya isipokuwa ni kwa yule mwenye roho ngumu kama mimi ndiye naweza kuishi katika mazingira magumu kama haya.

"Ndiyo maana naishauri serikali iangalie namna ya kuwapa motisha walimu wanaofundisha katika visiwa hivi na kuweka kipindi maalumu cha kukaa ili kumfanya mwalimu awe na moyo wa kufundisha.


"Serikali iangalie uwezekano wa kuongeza marupurupu kwa walimu wanaoishi kando kando ya miji na wale wanaofundisha katika mazingira magumu kama sisi kutuongezea fungu la pesa ili kujikimu na hali ngumu iliyoko katika visiwa."

Kwa mujibu wa mwalimu Hamisi, baadhi ya walimu huamua kugoma kuripoti kutokana na taarifa kwamba walimu wanaopangwa kufanya kazi visiwani humo husahauliwa kabisa hivyo hukaa bila kuhamishwa kwa muda mrefu.


Anasema mpango huo ni tatizo mojawapo kwani walimu katika maeneo haya wamekuwa wakisahaulika kabisa kiasi cha kukata tamaa kwani kama wapo wawwili wataendelea kuwa hivyo kwa muda mrefu na kama yuko mmoja basi ataendelea kukaa hivyo hivyo. Tatizo jingine analiliona Mwalimu Hamisi ni ugumu wa kupata maji safi kwa kuwa visima vilivyochimwa ni vifupi sana. "Ukitaka maji yaliyo salama ni lazima ununue dumu moja kwa Sh 700 hadi Sh1,000 kutoka katika kisiwa kingine kilicho mbali. Maji huletwa kwa mitumbwi ambayo wakati mwingine si salama,’’ anasema.


Alisema hata huduma ya afya bado ni tatizo kwa kuwa hospitali iko mbali sana na kisiwa hicho na upatikanaji wa dawa ni mgumu pia na hivyo humlazimu kutembea umbali wa siku nzima kufuata huduma ya matibabu.


Mwamko
Uhaba wa walimu unasababisha wanafunzi wengi kutokuwa na mwamko wa elimu. Baadhi huamua kuacha masomo na kujishughulisha na shughuli kama za uvuvi na kilimo. Wakati wa msimu wa kilimo baadhi ya wanafunzi huandamana na wazazi wao kwenda mashambani na wakati wa mavuno pia huenda kuwasaidia wazazi wao kuvuna. Mahudhurio ya wanafunzi katika misimu hiyo huwa madogo sana na ya kukatisha tamaa.


"Hali huwa mbaya zaidi inapofikia wakati wa kilimo kwa sababu wazazi huondoka na watoto hao na kwenda kwenye kilimo kwa takribani miezi sita na bado mwalimu ukienda kufuata mshahara, lazima ufunge shule hadi urudi ndipo ufungue shule. Pengine hutumia hata wiki mbili."
 
Tumain

Tumain

JF-Expert Member
Joined
Jun 28, 2009
Messages
3,158
Likes
11
Points
0
Tumain

Tumain

JF-Expert Member
Joined Jun 28, 2009
3,158 11 0
Duniani kuna watu wenye moyo hamisi una moyo mkubwa sana Mwenyezi Mungu akuongezee

Imagine kuwa mwalimu pekee kuanzia darasa la kwanza mpaka darasa la Saba?

Kufundisha kila somo kwa kila darasa?

Ni mwalimu mkuu, mwalimu wa nidhamu na mwalimu wa hesabu?

Mshahara unachelewa? agh!

Hamisi una moyo sana, JF we need to do something about this ?????...
 
Saint Ivuga

Saint Ivuga

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2008
Messages
45,379
Likes
31,608
Points
280
Saint Ivuga

Saint Ivuga

JF-Expert Member
Joined Aug 21, 2008
45,379 31,608 280
du. bado tuna safari ndefu. kuna wazazi ambao bado hawajui umuhimu wa elimu.ndio maana watu wa kaskazini wamejazana kwenye vitengo.
Nani tumlaum lakini..
 
M

mtatifikolo

Member
Joined
Feb 9, 2008
Messages
43
Likes
1
Points
0
M

mtatifikolo

Member
Joined Feb 9, 2008
43 1 0
I propose "Saidia shule ya msingi Saninga Fund"
 
Waberoya

Waberoya

Platinum Member
Joined
Aug 3, 2008
Messages
12,505
Likes
4,879
Points
280
Waberoya

Waberoya

Platinum Member
Joined Aug 3, 2008
12,505 4,879 280
wakuu mishahara yao ni sh, ngapi?
 
Lambardi

Lambardi

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2008
Messages
10,407
Likes
5,796
Points
280
Lambardi

Lambardi

JF-Expert Member
Joined Feb 7, 2008
10,407 5,796 280
Mishahara ya walimu haifiki 280,000 kwa sasa akijitahidi sana ndio hapo....
 
kilemi

kilemi

JF-Expert Member
Joined
Mar 13, 2009
Messages
524
Likes
6
Points
35
kilemi

kilemi

JF-Expert Member
Joined Mar 13, 2009
524 6 35
Mishahara ya walimu haifiki 280,000 kwa sasa akijitahidi sana ndio hapo....
Shahada(degree)= 310,000; stashahada(dip.)=280,000; Cheti(certificate)= 120,000= Yawezekana ndio mshahara wa mwl Hamisi kama hajapandishwa daraja!!
Pia hii mishahara ni Gross sallary (haijakatwa kodi)!
Wewe waweza? Naamini huwezi! Sasa tumlaumu nani matokeo ya mitihani yanapokuwa mabaya?
 
kisasangwe

kisasangwe

JF-Expert Member
Joined
Feb 16, 2010
Messages
294
Likes
2
Points
33
kisasangwe

kisasangwe

JF-Expert Member
Joined Feb 16, 2010
294 2 33
du. bado tuna safari ndefu. kuna wazazi ambao bado hawajui umuhimu wa elimu.ndio maana watu wa kaskazini wamejazana kwenye vitengo.
Nani tumlaum lakini..
hii safari naona twasafiria guta. wakati wenzetu wanapaa. jamani mwamko wa elimu uko wapi hata kwa wazazi wa eneo hili???

:eek:
 
Mazingira

Mazingira

JF-Expert Member
Joined
May 31, 2009
Messages
1,837
Likes
26
Points
135
Mazingira

Mazingira

JF-Expert Member
Joined May 31, 2009
1,837 26 135
Inabidi serikali iwe na mpango wa kutoa motisha kwa walimu kwenda kukaa sehemu kama hizi. Say mishahara yao iwe mara mbili ya kawaida. Maana hakuna mtu aliye tayari kwenda kwenye sehemu kama hizi ambazo hata huduma za jamii ni duni kupita kawaida. Vilevile serikali iwe na mikakati ya kuboresha huduma za jamii huko ili kuwavutia walimu. Vinginevyo watu wa maeneo hayo wataendelea kubaki nyumba mpaka YESU atakarudi mara ya pili.
 
Ngongo

Ngongo

JF-Expert Member
Joined
Sep 20, 2008
Messages
12,431
Likes
4,113
Points
280
Ngongo

Ngongo

JF-Expert Member
Joined Sep 20, 2008
12,431 4,113 280
Duh hii kali Mwl Hamis kweli ana moyo,mleta mada unaweza kupendekeza jinsi ya kumsaidia Mwl Hamis na shule anayofundisha.
 
R

Rwabugiri

JF-Expert Member
Joined
Jul 10, 2007
Messages
2,776
Likes
16
Points
135
R

Rwabugiri

JF-Expert Member
Joined Jul 10, 2007
2,776 16 135
hii safari naona twasafiria guta. wakati wenzetu wanapaa. jamani mwamko wa elimu uko wapi hata kwa wazazi wa eneo hili???

:eek:


Shhhhhhhhhhhhhhhhhhh! kisasangwe ndege yetu ya uchumi ina paa ama umesahau?
 
FirstLady1

FirstLady1

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2009
Messages
16,727
Likes
796
Points
280
FirstLady1

FirstLady1

JF-Expert Member
Joined Jul 29, 2009
16,727 796 280
Serikali hailioni hili swala mbona hatari sana
 
Tumain

Tumain

JF-Expert Member
Joined
Jun 28, 2009
Messages
3,158
Likes
11
Points
0
Tumain

Tumain

JF-Expert Member
Joined Jun 28, 2009
3,158 11 0
Duh hii kali Mwl Hamis kweli ana moyo,mleta mada unaweza kupendekeza jinsi ya kumsaidia Mwl Hamis na shule anayofundisha.
Ntamuandikia mod tuone itakuwaje!
 
Sajenti

Sajenti

JF-Expert Member
Joined
Apr 24, 2008
Messages
3,671
Likes
33
Points
0
Sajenti

Sajenti

JF-Expert Member
Joined Apr 24, 2008
3,671 33 0
Hili mbona liko wazi...kwa mtazamo wangu lazima lawama ziende kwa watawala wetu ambao walisoma katika mazingira mazuri hadi kufikia ngazi za juu kabisa lakini walipoingia madarakani wao wakawa wa kwanza kuvuruga mfumo wa utumishi hapa Tz. Uwezo wa kuboresha elimu Tz upo kabisa, kutoa mishahara mizuri na kuweka mazingira bora ya kazi uwezo upo. Tatizo nilionalo mimi ni akili na roho za ulafi za watawala wetu kutojali wengine na kudhani kuwa kwa kuwa wao wamefanikiwa ndio mwisho wa maisha.Ufisadi na ubadhirifu unaondelea kwa kweli ni matunda ya roho mbaya na akili za uchoyo za hao watawala...Imagine huyo mwalimu atakapopata tatizo kubwa kama binadamu kutakuwa na shule tena hapo???..........Napata hasira kabisa.
 
Masaki

Masaki

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2006
Messages
3,464
Likes
179
Points
160
Masaki

Masaki

JF-Expert Member
Joined Mar 7, 2006
3,464 179 160
Ntamuandikia mod tuone itakuwaje!
Anzisha hapa hapa kwa haraka haraka,

SAIDI MWALIMU HAMISI, SAIDI SANINGA SHULE YA MSINGI!

Kwa kuanzia tunaweza kupata mchango wa haraka haraka wa kumnunulia mwalimu Hamisi baiskeli. Maana nimesoma kwamba huwa anatembea kwa miguu umbali wa kutwa nzima kufuata huduma za afya na mshahara!

Baiskeli ni shilingi ngapi jamani?
 
Sikonge

Sikonge

JF-Expert Member
Joined
Jan 19, 2008
Messages
11,550
Likes
642
Points
280
Sikonge

Sikonge

JF-Expert Member
Joined Jan 19, 2008
11,550 642 280
Baiskeli sidhani kama itakuwa aghali kiasi hicho.

Mie naomba tulale na Waziri wa elimu ili huyu jamaa awe analipwa mishahara ya waalimu kama 4 kwa kuwa anafanya Overtime si ya kawaida.

Tusimpe samaki ila tufanye mpango awe na ndoano. So longer yuko peke yake basi ijumlishwe masaa anayofundisha na apewe hiyo overtime yake kila mwezi na nina imani itatosha anunue hata kipikipiki na helmet yake ......
 
RayB

RayB

JF-Expert Member
Joined
Nov 27, 2009
Messages
2,754
Likes
90
Points
145
RayB

RayB

JF-Expert Member
Joined Nov 27, 2009
2,754 90 145
na serikali inayojitamba ina achieve na kutekeleza ilani itakuwa na kazi gani?please give me a break

Halafu ziko nyinggi sio ya Hamisi tu, halafu hivi hata serikali inafahamu kuwa yupo huko? Alishawahi kutembelewa? Sasa huko ndo kwa kwenda sio uturuki kwenye PHD ya asante mkuu
 
Masaki

Masaki

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2006
Messages
3,464
Likes
179
Points
160
Masaki

Masaki

JF-Expert Member
Joined Mar 7, 2006
3,464 179 160
Baiskeli sidhani kama itakuwa aghali kiasi hicho.

Mie naomba tulale na Waziri wa elimu ili huyu jamaa awe analipwa mishahara ya waalimu kama 4 kwa kuwa anafanya Overtime si ya kawaida.

Tusimpe samaki ila tufanye mpango awe na ndoano. So longer yuko peke yake basi ijumlishwe masaa anayofundisha na apewe hiyo overtime yake kila mwezi na nina imani itatosha anunue hata kipikipiki na helmet yake ......
Wazo lako mkuu ni zuri, ila ni la kimapinduzi sana! Halitekelezeki kirahisi! Kama kuna watu waliosoma shule za bweni miaka ya 1980 na 1990 watakumbuka wanafunzi waliokuwa wanakuja shuleni kutokea vijijini kabisa! Wanasimulia vitu vingi ikiwemo kwamba hawajawahi kuona magari tangu wamezaliwa!

Baadhi yao leo ni wabunge ndani ya Bunge letu, na wengine ni maofisa wa ngazi za juu serikalini na kwenye mashirika binafsi. Ninachosema hapa;

1. Mwandishi anastahili pongezi kwa kwenda mbali zaidi ya kuandika habari za siasa za kila siku. Amekwenda kuandika habari inayoigusa jamii moja kwa moja!

2. Mwandishi wa habari hii atafarijika sana endapo Mwalimu Hamisi na shule ya Msingi kwa ujumla itapata ufumbuzi wa haraka wa matatizo iliyonayo.
3. Pia, itakuwa ni faraja kubwa kwa mwandishi endapo jamii itasaidia katika mipango ya muda mfupi kumhamasisha mwalimu Hamisi kuendelea na moyo huo.
Kwa mfano kumnunulia baiskeli.
4. Kwa kufanya hivyo, tutawasaidia watoto wa Kitanzania kupata japo hiyo Elimu kidogo toka kwa Mwalimu Hamisi na pengine wachache kati yao watafanikiwa kufaulu mitihani yao na kusonga mbele hata kufikia elimu ya juu!
5. Mambo kama haya jamii iyape kipaumbele kama ilivyokuwa kwenye majanga ya kitaifa kama ya mabomu ya Mbagala na mafuriko ya Kilosa!

Mabadiliko yanaanza na sisi wenyewe!

Naomba kuwasilisha!
 
Masaki

Masaki

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2006
Messages
3,464
Likes
179
Points
160
Masaki

Masaki

JF-Expert Member
Joined Mar 7, 2006
3,464 179 160
Halafu ziko nyinggi sio ya Hamisi tu, halafu hivi hata serikali inafahamu kuwa yupo huko? Alishawahi kutembelewa? Sasa huko ndo kwa kwenda sio uturuki kwenye PHD ya asante mkuu
Acha kumpigia mbuzi gitaa....Angalia jinsi ya kumsaidia Mwalimu Hamisi kwanza ili asivunjike moyo wa kusomesha Watazania wenzetu. Serikali yetu ni sikio la kufa, halisikii dawa!
 

Forum statistics

Threads 1,236,236
Members 475,029
Posts 29,250,891