Mwalimu akutwa na mwanafunzi chumbani

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Apr 29, 2016
20,744
25,445
GEITA: Mwalimu wa shule ya Sekondari ya Bugando Kata ya Nzera wilayani Geita mjini hapa, Noel Seleman anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kukutwa na denti wa kidato cha kwanza chumbani kwake.

Katika tukio hilo lililojiri hivi karibuni maeneo hayo, ticha huyo alidaiwa kuwa na uhusiano wenye shaka na mwanafunzi huyo mwenye umri wa miaka 17, uhusiano unaoelezwa kudumu kwa takriban mwaka mmoja sasa.

Akisimulia tukio hilo, baba mzazi wa mwanafunzi huyo, Francis Andrea alieleza kusikitishwa kusikitishwa na kitendo cha mwalimu huyo huku akiiomba Serikali imsaidie.

“Ni muda nilikuwa nikisikia kuwa mwanangu ana uhusiano na mwalimu.

“Siku ya tukio aliondoka nyumbani asubuhi, niliporudi nyumbani nikamuuliza mama yake, akaniambia alimtuma, lakini jambo la kushangaza tangu saa nne asubuhi hadi saa nane mchana alikuwa hajarejea nyumbani ndiyo nikachukua uamuzi wa kumwambia mdogo wake ambaye alikuwa naye kuwa dada yake yupo wapi.

“Mdogo wake alinipeleka na kunionesha kuwa yupo chumbani kwa mwalimu wake, nilikasirika sana na kama mzazi nilicharuka.

“Nilirudi nyumbani kwa hasira, nikawachukua vijana sita na wanawake wanne tukaenda kumkamata huyo mwalimu baada ya kumkuta ‘laivu’ na binti yangu chumbani.

“Baada ya kumkamata tulimwita balozi wa eneo hilo akashuhudia na kutusaidia kumfikisha Polisi,” alisema baba huyo kwa uchungu.

Kwa upande wake, mama wa mwanafunzi huyo, Joyce Katambi aliliambia Ijumaa Wikienda kuwa, mara kwa mara amekuwa akimkanya binti yake kujihusisha na mapenzi akiwa bado anasoma, lakini amekuwa hamsikilizi, hali ambayo ilimsababisha kujikuta akikutwa na mwalimu wake chumbani.

Balozi wa eneo hilo, Shaaban Majaliwa alisema walipozungumza na mwanafunzi huyo alikiri kuwa na uhusiano na mwalimu wake.

Kwa upande wake mwanafunzi huyo alipohojiwa na Ijumaa Wikienda alikanusha kuwa na uhusiano na ticha wake na kwamba alikwenda nyumbani kwake kumjulia hali baada ya kupata taarifa kuwa amepata ajali.

Kamanda wa Polisi Mkoani Geita, ACP Mponjoli Mwabulambo aliliambia gazeti hili kuwa, tukio hilo lilijiri Agosti 13, mwaka huu, majira ya saa nane mchana ambapo mtuhumiwa alitiwa mbaroni na upelelezi utakapokamilika atafikishwa mahakamani.

Chanzo:Globals Publishers
 
Bac huyo mzazi kaharibu ushahidi na kesi kaisha shindwa.

1. Alijibeba yeye na mashilawadu kwenda kuvamia mwalimu bila ya kuwa na muongozo kutoka serkal ya mtaa. Yan unaenda msearch mtu kwake bila RB or search warantee or balozi.

2. Mwanafunzi kasema hana mahusiano so kukutwa kwa mwalimu sio kosa kisheria anaweza kuwa alienda kufundishwa au kusalmia.

ELIMU ELIMU ELIMU.
Ni kweli walimu wanawakula wanafunzi wao ila inapokuja kwenye kuwakamata na kuwa na ushahidi wa kutosha ndipo shida ilipo.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hahaaa kesi hakuna hapo" Mtoto kesha mtetea mwalimu duuuhh""... mbona anaonyesha kuwa amekubuhu aisee""... hana hata hofu"" halafu mama yake pia inaonyeha kuwa siku nyingi anaujua mchezo mzima jinsi ulivyo " na huwenda ikawa anapewaga bakshishi na mtoto wake ili asimchongee kwa dingi"" Mama namtoto lao moja wallahi
 
Hako kadent ni kaninja...ndo basi tena kashajua dudu washa, katapata tabu sana
 
daaahh ila Kuwa mwalimu wa kiume sec. yataka moyo jinsi navyowaonga MA binti walivyonona vile'" daaahh nyie acheni tu
 
....unakutamwanafunzi ana sura angavu kuliko ya mke wa teacher...Pepooo kemeaaa
 
Back
Top Bottom