Mwalimu akutwa mtupu Shuleni Lindi

Candid Scope

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,879
1,250
UCHAWI UCHAWI UCHAWI
mbeyayetu.blogspot.com... Kenya akisindizwa na polisi kwenda kuondoa uchawi aliyomfanyia mtoto wa ...
swahilitime.blogspot.com


Nani kasema uchawi ni wa mwafrika tu? kwamujibu wa picha hiyo, ...kangevile.wordpress.com

Mwalimu akutwa mtupu Shuleni Lindi

MWALIMU Mkuu wa Shule ya Msingi Rutamba, Wilaya ya Lindi amekutwa akiwa na nguo za ndani pekee katika usingizi mzito kwenye kibao cha shule hiyo huku akiwa hajitambui kwa madai ya kilichomkutana kinahusishwa na imani za kishirikina.

Tukio hilo limetokea juzi usiku baada ya mkazi mmoja wa kijiji hicho, Juma Mbilemoto kumkuta mwalimu huyo akiwa kwenye kibao hicho wakati alipokuwa anamsindikiza nduguye,Aisha Mbilimoto aliyekuwa anasafiri kuelekea Dar es Salaam.

Akizungumzia tukio hilo, shuhuda huyo alisema alimkuta mwalimu huyo akiwa amelala chini ya kibao cha shule akiwa na nguo ya ndani tu (chupi)huku akikoroma kutokana na kuwa na usingizi mzito.Alisema awali hakumtambua mtu huyo lakini baada ya kumkaribia alimtambua kuwa alikuwa mwalimu mkuu wa shule hiyo na ndipo alipochukua jukumu la kumwamsha ili amvalishe kanga, lakini aliikataa na kuondoka kwenda nyumbani kwake akiwa kama alivyokutwa

Kwa upande wao walimu wa shule hiyo walisema kuwa, wamekosa molari wa kufanya kazi kutokana na kitendo alichofanyiwa mwalimu mwenzao.

Akizungumza kwa niaba ya walimu wenzake mwalimu wa taaluma wa shule hiyo, Francis Milanzi alisema walimu shuleni hapo wamekosa amani na kuwasababishia kuzihama nyumba zao kwa muda na badala yake kwenda kukesha kwenye ofisi za walimu tangu tukio hilo litokee.

Ofisa elimu wa Wilaya ya Lindi, Cosmas Magigi alisema amepokea taarifa za tukio hilo kwa huzuni na amewaomba walimu kuwa na subira wakati utaratibu wanalishughulikia suala hilo.

Magigi aliongeza kuwa ofisi yake itafanya utaratibu wa kumhamisha mwalimu huyo na kumtafutia shule nyingine huku akiwataka wakazi wa eneo hilo kujenga ushirikiano na watumishi ili waweze kutekeleza majukumu yao.

Hili ni tukio la pili kutokea katika halmashauri hiyo mwaka huu ambapo la kwanza lilitokea April katika Shule ya Sekondari Ruhokwe, mwalimu wa shule hiyo alilazwa kwenye kibao cha shule akiwa uchi wa mnyama.


 
  • Thanks
Reactions: kbm
Katavi

Katavi

Platinum Member
Aug 31, 2009
41,148
2,000
Duh...! Aletwe huku kwetu hakuna matukio hayo.
 
Candid Scope

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,879
1,250
Duh...! Aletwe huku kwetu hakuna matukio hayo.
Kule umachingani wengi wanaimbia, ni michezo ya kawaida kwao. Nilichoshangaa siku napita njia ya Tunduru-Masasi ilikuwa alfajiri nilishangaa kumwona mwalimu kavaa lubega akipuliza filimbi kuashira wanafunzi wakusanyike. Nilifikiri sana na kufunga break kidogo, nikajifanya niulizie umbali wa kutoka pale hadi Masasi, baadaya nikachomekea swali la kijanja na kanijibu yeye ni mwalimu wa zamu wiki ile na anawakusanya wanafunzi waanze usafi. Akajieleza zaidi kwamba ni mzaliwa wa pale na kwamba wengi hawakai muda mrefu wanakimbia kwa vile hawawezi kujishusha kwa kujilinganisha na wenyeji na mengi huwasibu. Nikamwuliza mbona hajavaa nguzo zinazotakiwa kama mwalimu, kaniambia anazo atakwenda kubadili baadaye atakapoingia darasani. Sikuona haja ya kumwuliza zaidi kwani taswira ya hali halisi ya maisha huko si ngeni kwangu kutokana na mizunguko yangu ya pande mbalimbali za Tanzania yetu ninayoipenda kwa moyo wote.
 
Bujibuji

Bujibuji

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
48,722
2,000
Hiyo ndio mikoa yenye waumini wengi wa ile dini ya maandamano, vurugu na uhalifu
 
Candid Scope

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,879
1,250
Mkuu kwenu unamaanisha mkoa wa KATAVI ilipo sumbawanga?
Nimewahi kuishi Mkoa wa Rukwa na kutembelea maeneo mbalimbali hadi huko Kirando, Kipili nk, nikapata kuelewa maana ya sumbuwanga (tupa uchawi) kwani sikushuhudia mambo ya uchawi huko kama nilivyoambiwa kabla sijaenda huko. Wafipa wakaribu, wastaarbu, wanaheshimiana na hulka ya maisha ya ujama wa kiafrika, kitu ambacho sijakishuhudia katika pande nyingine za Tanzania, kwani tanzania nimebakisha Kigoma tu, vinginevyo mikoa mengine huwezi nitolea uvivu. Wanaogopwa tu. Lakini huko Umachingani balaa, mwenyewe nimeshuhudia classmate wangu alivyoathirika. Sijajua tatizo ni nini huko.
 
U

usungilo

JF-Expert Member
Aug 9, 2012
527
250
Mkuu kwenu unamaanisha mkoa wa KATAVI ilipo sumbawanga?
mkuu sumbawanga ni sehemu nzuri ya kuishi ila ufanye mambo yako usianze kutafuta uchawi. Ni watu wakarimu sana na wanawapenda watumishi wanaowasaidia. Wengi wanaanzaga kurogana kutafuta vyeo hapo unakuwa umeingia anga za watu. Ukishautafuta uchawi inakulazimu ufanye wanayoyafanya wachawi. Lakini ukistik kwenye shughuli zako zisizohusisha uchawi utafanikiwa tu.
 
U

usungilo

JF-Expert Member
Aug 9, 2012
527
250
Nawamea huruma sana walimu wa vijijini wanaofanyiwa mambo haya, tena wanawake! Loh!
 
M

Morinyo

JF-Expert Member
Aug 26, 2011
2,747
2,000
Hii picha mbona kama vile ya siku nyingi.
 
asrams

asrams

JF-Expert Member
Sep 4, 2011
4,805
2,000
Labda alikua anawanga ili wanafunzi wake wafaulu mtihani


Sent from my Nokia 8310 using Tapatalk
 
mizambwa

mizambwa

JF-Expert Member
Oct 8, 2008
4,435
2,000
....................INANIUMA SANa
MIZAMBWA
 
mizambwa

mizambwa

JF-Expert Member
Oct 8, 2008
4,435
2,000
Hii picha mbona kama vile ya siku nyingi.
Mtoa mada sijui alikuwa na maana gani kuambatanisha hii picha ya mwanamke.

Kwani iliwekwa hapa na kuelezwa kuwa ni tukio lililotokea Mbeya, ni mwanafunzi wa Chuo fulani huko.MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
ITEGAMATWI

ITEGAMATWI

JF-Expert Member
Jan 26, 2012
4,740
2,000
Hiyo ndio mikoa yenye waumini wengi wa ile dini ya maandamano, vurugu na uhalifu


Acha udini juha wewe!! Mbeya wanapochuna ngozi na Shinyanga na Mwanza wanapoua albino utasemaje? Hili ni changamoto ya taifa inayotokana na ukosefu wa elimu wala dini haihusiki!!!
 
M

Morinyo

JF-Expert Member
Aug 26, 2011
2,747
2,000
Mtoa mada sijui alikuwa na maana gani kuambatanisha hii picha ya mwanamke.

Kwani iliwekwa hapa na kuelezwa kuwa ni tukio lililotokea Mbeya, ni mwanafunzi wa Chuo fulani huko.MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
Yawezekana habari hii haina ukweli ameamua kutumia picha za nyuma kutudanganya.
 
Gulaya

Gulaya

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
660
225
Mkuu hii habari na hiyo picha mbona vlishaletwa jamvini yapita wiki moja na ilikuwa ni habari ya mbeya na ikasemakana kua huyo dada pichani ni mwanachuo wa chuo gani cjui hapo mbeya..
 
Ndahani

Ndahani

JF-Expert Member
Jun 3, 2008
16,592
2,000
Duuh..mpaka head teacher anakuwa tishio kijijini, basi huko maendeleo bado sana.
 
Top Bottom