real G
JF-Expert Member
- Feb 7, 2013
- 5,227
- 5,292
Mwalimu wa shule ya msingi Lupapila iliyopo kata ya Subira Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma Christopher Ndimbo (29) amekutwa amefariki baada ya kukatwakatwa sehemu mbalimbali za mwili wake na kitu chenye ncha kali
Kamanda wa polisi mkoa wa Ruvuma Zuberi Mwombeji alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema mwalimu huyo aliuawa na watu wasiojulikana na pia walichukua pikipiki yake.
Kwa mujibu wa kamanda huyo, mwalimu huyo aliuawa Juni 14 mwaka huu na mwili wake uliokotwa kichakani na majeraha hayo.
Kamanda ameongezea Mwalimu huyo mara ya mwisho mwalimu huyo alionekana maeneo ya Uhuru Pub uwanja wa Maji akisubiria abiria na baada ya kumpata mteja aliondoka na kuelekea kusikojulikana.