King Tembo
Senior Member
- Aug 29, 2017
- 127
- 73
Daaah R. I. P teacher
Ni kweli unachosema shida watu wakishapendana hawaangalii kesho matokeo mabaya ya tabia zao wanaanza kubebesha wengine. Bila shaka wewe ni mtaalam wa saikolojiaMwl huyo inaonekana alikuw akisumbuliwa na ugonjwa wa akili, ugonjwa huu unasumbua baadhi ya watu na mtu anaweza akadhani yupo sawa tu, ila ukichunguza kwa undani utagundua kuwa ni mgonjwa sana, mfano, mtu aliye na sonona au mfadhaiko kupita kiasi kwa sababu ya jambo fulani anaweza fanya tendo la mauji kama hili, jinsi zote me na ke zinaweza fanya hili ingawa kwa wanawake wanaweza fikiria mara mbili kabla ya kujiua, kwa wanaume ni tofauti kwani wao wakiamua mara moja hujitoa uhai. Tujitahidi kuwasaidia watu wenye matatizo haya, ukiona mtu anajitenga na wenzake huku hapendi kabisa kuwa karibu na wenzake yupo kimya kimya tu iwe kazini, nyumbani au popote pale tuwasaidie watu hao. Unaweza washauri wamwone mnasihi au mtoa ushauri nasaha au daktari wa magonjwa ya akili. Pia walio katika ndoa msiwe chanzo cha kuwafanya wenzi wenu wapoteze furaha na amani ya moyo, hii itapelekea mtu kufanya maamuzi mabaya kwa sababu tu maisha yake na wewe anayaona ni taabu na kaisha gharamika sana kuwa na wewe kwa kila kitu halafu wewe unakuwa kikwazo kwake.
Natahadharisha, watu wenye magonjwa ya akili wao huona wapo sawa tu, ni wakali na wabishi inahitajika busara kuwasaidia.
Sio walimu wote tupo hivyo.Mpumbavu huyo
Walimu mna matatizo sana
Mwalimu wa Shule ya Sekondari ya Mtenga wilayani Nkasi, Leonard Mwipugi (29) amejiua kwa kujichinja koromeo akiwa nyumbani kwake.
Taarifa zilizotolewa na Mratibu wa Elimu Kata ya Mtenga, Hebron Mwafungo zimeeleza kuwa mwalimu huyo amekutwa akiwa amekufa baada ya kujichinja nyumbani kwake muda wa saa sita mchana leo Jumamosi.
Amesema kuwa mwalimu huyo alikwenda kazini kwake na saa 5 asubuhi alirejea nyumbani na hakumkuta mkewe na baada ya muda walipata taarifa kuwa mwalimu huyo amekutwa amekufa baada ya kujichinja koromeo chumbani kwake.
Amesema kuwa mwalimu huyo alikua akiishi na mdogo wake nyumbani hapo na alipofika alimtuma mdogo wake mbali kidogo ya nyumba hiyo na baada ya kurudi aliona damu na baada ya kuchungulia chumbani alikuta kaka yake amefariki dunia kwa kujichinja koromeo na kutoa taarifa kwenye uongozi wa kijiji hicho.
Li mgomba lote hlo mkuu, mchicha tuhh unakupeleka kukaba kiwanja.Siku zikifika hata mgomba ukikuangukia unakufa
Amechoka na msemo wa "pambana na hali yako"Jamaa alikuwa na roho ngumu, hivi maisha yalivyo matamu , unaanzaje kukatisha uhai wako kwa sababu za kipuuzi.
Mleta mada sijui alikuwa anakimbia. Kifupi ni kwamba chanzo ni mzozo Wa kifamilia ambapo mke Wa marehemu alikwenda kumshitaki mumewe polisi kwamba hatunzi familia, jambo hili lilimuudhi mwalimu na kuamua kujichinja koromeo huku akijitazama kwenye kioo. Mazishi yake ni Leo hapa Mafinga maana marehemu ni Mhehe.kwani ticha alivurugwa na nini hadi akaamua kuchukua maamuzi mkononi?
Wewe nae una akili za kimwalimu kuna vigezo gani vinataka mtu ajinyonge au kujiua?Acheni kashfa hizo za kuwatukana walimu akati ndo waliowatoa ujinga binafsi me naona Mwalimu alichukua uamzi huo kwa vigezo maalumu anavyojua yeye Mimi na wewe hatujui kilichomsibu
Mke wake alikuwa ameenda kwa mwalimu wa taluma kufundishwa reproduction jamaa ikamuuma kunoma akaamua kujichinja .kwani ticha alivurugwa na nini hadi akaamua kuchukua maamuzi mkononi?