Mwalimu ajichinja koromeo hadi kufa

Mwalimu ajichinja koromeo hadi kufa

Hivi punde

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2017
Posts
2,554
Reaction score
8,627
Mwalimu wa Shule ya Sekondari ya Mtenga wilayani Nkasi, Leonard Mwipugi (29) amejiua kwa kujichinja koromeo akiwa nyumbani kwake.

Taarifa zilizotolewa na Mratibu wa Elimu Kata ya Mtenga, Hebron Mwafungo zimeeleza kuwa mwalimu huyo amekutwa akiwa amekufa baada ya kujichinja nyumbani kwake muda wa saa sita mchana leo Jumamosi.

Amesema kuwa mwalimu huyo alikwenda kazini kwake na saa 5 asubuhi alirejea nyumbani na hakumkuta mkewe na baada ya muda walipata taarifa kuwa mwalimu huyo amekutwa amekufa baada ya kujichinja koromeo chumbani kwake.

Amesema kuwa mwalimu huyo alikua akiishi na mdogo wake nyumbani hapo na alipofika alimtuma mdogo wake mbali kidogo ya nyumba hiyo na baada ya kurudi aliona damu na baada ya kuchungulia chumbani alikuta kaka yake amefariki dunia kwa kujichinja koromeo na kutoa taarifa kwenye uongozi wa kijiji hicho.
 
kwani ticha alivurugwa na nini hadi akaamua kuchukua maamuzi mkononi?
 
R.I.P mwalimu...nafikiri ni stress zilkua znamsumbua.....kaz ya ualimu bhn.
 
Unamwonea wivu mwanamke tena umeoa single mama,,,wivu wa nn? Fukuza tu...lete mwengine
 
Rip mwalimu.
Poleni walimu Kwa maswahibu na manyanyaso mnayopata.
Hakuna anayetambua mchango wenu ni kukandamizwa tu ktk maslahi na haki zenu.
kifo kama hicho unalazimisha kihusishwe na changamoto za kazi ya ualimu? hebu kuweni waungwana
 
Back
Top Bottom