Mwalimu afunga ndoa na mwanafunzi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwalimu afunga ndoa na mwanafunzi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, May 31, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  May 31, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,612
  Trophy Points: 280
  WAKATI serikali ikiweka msisitizo katika kumkomboa mtoto wa kike kielimu, mwalimu mmoja wa hapa, Deogratius Peace, juzi alifanya kitu kilichowashitua wengi, baada ya kumuoa mwanafunzi wa kidato cha nne katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi na kupata cheti cha ndoa.

  Mwanafunzi aliyeolewa, Kabula Phares (20) au Amina Idd, ni mwanafunzi katika Shule ya Sekondari ya Kishamapanda Kata ya Nasa wilayani Magu, mkoani Mwanza.

  Peace ni Mwalimu katika Shule ya Sekondari Byuna, wilayani Magu. Habari za Mwalimu Peace mwenye umri wa miaka 29 kumuoa mwanafunzi, zimethibitishwa na Mkuu wa Wilaya hiyo, Baraka Konisaga.

  “Ni kweli amemuoa mwanafunzi, na hivi ninavyozungumza bado wako ndani (Polisi)…" “Huyu mwalimu amefanya kitendo cha aibu sana katika taaluma ya ualimu,” alisema Konisaga alipokuwa anathibitisha tukio hilo".

  Mbali ya wanandoa hao, Konisaga pia amethibitishwa kushikiliwa kwa baba mzazi wa `bibi harusi’ mwanafunzi, Idd Hamisi, ambaye ni dereva wa Kampuni ya Bia ya Serengeti jijini Mwanza, naye yuko mikononi mwa Polisi.

  “Tumewasiliana na Kamanda wa Mwanza ambako baba wa binti anafanya kazi, wanamshikilia na nimeshatuma vijana waende kumchukua ili aunganishwe na hawa wanandoa, tumhoji na kuweza kujua kama alibariki ndoa hii haramu,” alisisitiza Mkuu huyo wa Wilaya.

  Siku ya tukio, 'bibi harusi’ akiwa amefuatana na mama yake wa kambo, Suzana Idd, juzi majira ya saa tano za asubuhi alifika katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya na kuolewa na Peace ambaye mpambe wake ametajwa kuwa alikuwa Kabala Charles.

  Ndoa hiyo ilifungishwa na Katibu Tawala wa Wilaya ya Bariadi, Jackson Sima, ambaye inaelezwa licha ya kupata fununu za ndoa hiyo `haramu’, aliridhia kuendelea na taratibu za kuwaunganisha Mwalimu Peace na mwanafunzi wake.

  Lakini hafla fupi ya ndoa hiyo iliingia doa muda mfupi baada ya kukamilika kwa taratibu zote, baada ya maofisa wa Polisi wakiongozwa na Kaimu Mkuu wa Polisi wa Wilaya hiyo, aliyefahamika kwa jina moja la, Mbise, kuvamia ghafla na kuwaweka chini ya ulinzi wanandoa hao na kuwaongoza hadi kwa Mkuu wa Wilaya, kwa ajili ya mahojiano mafupi kuhusu kitendo cha mwalimu kufunga ndoa na mwanafunzi.

  Katika mahojiano hayo, ilibainika kuwa Mwalimu Peace alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanafunzi huyo wakati akiwa kwenye mazoezi ya kozi ya ualimu kwa kipindi cha miezi sita kwenye Shule ya Kishamapanda, wakati mwanafunzi huyo akiwa kidato cha pili.

  Kwa kwa sasa mwalimu huyo alikuwa amepata ajira kwenye Shule ya Sekondari ya Byuna iliyoko wilayani Bariadi na kwamba ameoa bila idhini ya wazazi wa mwanamke, baba Idd Hamisi na mama mzazi wa mwanafunzi huyo, Pendo Selemani anayeishi Dar es Salaam.

  Mama wa kambo wa mwanafunzi huyo, Suzana, alipotakiwa kuzungumzia ndoa hiyo alisema yeye alikuwa shahidi tu katika ndoa hakupata mahari wala mume wake hakupewa mahari na muoaji.

  Inadaiwa kuwa, mwanafunzi huyo alikuwa akiishi kwa bibi yake mzaa mama katika kijiji cha Nasa wilayani Magu, baada ya mama yake kutengana na mtoto wake na kuhamia jijini Dar es Salaam.

  Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Konisaga, akizungumzia kitendo cha mwalimu kumuoa mwanafunzi wake wa kidato cha nne, alisema ni cha aibu, udhalilishaji na kuifedhehesha taaluma ya ualimu kwa kuwa mwalimu ni mmoja wa walezi wa watoto wanapokuwa shuleni.

  Alisema, wakati serikali inapiga kelele za wanafunzi wa kike wasome na wale watoro warudi mashuleni mwalimu Peace ameamua kumuoa mwanafunzi wake ili awe mke wake wa ndani. “Sijawahi kuona mambo ya aibu na ajabu kama haya.

  Sitaki kusema zaidi, lakini hatima yao nadhani itakuwa kuishia mahakamani na kwa kuwa tuna uthibitisho wa hati, kazi inakuwa nyepesi…bila shaka Jumatatu kwa sababu tukio lenyewe limeangukia wikiendi,” alisema Konisaga aliyewahi pia kuwa Mkuu wa Wilaya ya Temeke, jijini Dar es Salaam.
  HabariLeo | Naali, Mgosi, Chuji wachomoza TASWA

  kweli mapenzi hayachagui huyu mwanafunzi huyu ni mwalim kasheshe kweli bongo yetu
   
 2. B

  Bull JF-Expert Member

  #2
  May 31, 2010
  Joined: Nov 4, 2008
  Messages: 984
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkuu Mi sioni tatizo liko wapi? kama bint anamiaka 20 huyu ni mature student kunaubaya gani kuolewa? kinacho nishangaza ni hawa police kuwa arrest wahusika, hivi sheria Tanzania kwetu imebadilika?
   
 3. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #3
  May 31, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Kwa hiyo Binti shule ndio basi tena
   
 4. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #4
  May 31, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  Samahani, mods unganishe hii thread tayari ipo nyingine
   
 5. Soulbrother

  Soulbrother JF-Expert Member

  #5
  May 31, 2010
  Joined: Apr 14, 2009
  Messages: 408
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Mwalimu huyo angesubiri hadi amalize shule... ana muda mfupi tu
   
 6. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #6
  May 31, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  Tatizo kubwa hapa nikuwa huyo mwalimu ana kosa gani wakati mkewe an miaka 20. huyo ni mtu mzima
   
 7. Shapu

  Shapu JF-Expert Member

  #7
  May 31, 2010
  Joined: Jan 17, 2008
  Messages: 1,918
  Likes Received: 234
  Trophy Points: 160
  mhh!
   
 8. M

  Mundu JF-Expert Member

  #8
  May 31, 2010
  Joined: Sep 26, 2008
  Messages: 2,719
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Hivi sheria ya ndoa imeweka umri gani kwa wanandoa? Huyo binti angekuwa labda na miaka 25 na yupo kidato cha nne, bado ingekuwa ni kinyume cha sheria? Au sheria inakataza kuoa wanafunzi hata kama watakuwa ni vikongwe? Tuwekani sawa hapa wanajamii.
   
 9. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #9
  May 31, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  Tanzania hakuna graduates au wanafunziwa university wenye 20 yrs mbona ni wengi tu na wengine wanaolewa mbona hawashikwi?
   
Loading...