Mwalimu adaiwa kulawiti wanafunzi sita | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwalimu adaiwa kulawiti wanafunzi sita

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Aug 19, 2011.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Aug 19, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  Fina Lyimo, Rombo
  MWALIMU wa Shule ya Msingi ya Kwamaksau iliyopo Useri, Wilaya ya Rombo, mkoani Kilimanjaro anatuhumiwa kuwalawiti wanafunzi sita wa kiume kwa nyakati tofauti baada ya kuwarubuni kwa kutumia vishawishi mbalimbali.

  Vishawishi hivyo ni pamoja na kuwapa fedha, kuwatafutia ada na wengine akiwapa chakula kingi cha mchana wawapo shuleni.Hata hivyo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Absolom Mwakyoma alisema uchunguzi wa awali wa polisi unaonyesha kuwa kitendo wanachodaiwa kufanyiwa wanafunzi hao si kulawitiwa bali kushikwashikwa korodani zao.

  “Tusiwe wepesi wa kuwalaumu polisi bila kuwa na uhakika na kile tunachowalaumu nacho, mimi nimefika mwenyewe shuleni hapo na nimezungumza na daktari aliyewafanyia uchunguzi na vipimo havionyeshi waliingiliwa,” alisema.

  Mwakyoma alifafanua kuwa tuhuma kuwa kila mara mtuhumiwa huyo anapofikishwa polisi huachiwa si sahihi kwani amekuwa akifikishwa mahakamani na anapopewa dhamana na mahakama, wananchi wanadhani ni uamuzi ya polisi.

  Mzazi wa mmoja wa mtoto wanaodaiwa kulawitiwa alidai mtoto wake ambaye yuko darasa la saba shuleni hapo alifika nyumbani na kumweleza kuwa mwalimu alimpa Sh500 na kumwingiza ‘stoo’ na kumfanyia kitendo hicho.

  Mzazi huyo, alidai mtoto wake alikuwa na rafiki yake ambapo wote walipewa Sh500 kwa ajili ya kufanyiwa kitendo hicho na kuwa mwalimu huyo alipomaliza kumfanyia mmoja alimchukua mwingine na kuanza kumfanyia.

  “Mtoto wangu alikuja nyumbani akiwa anachechemea huku akiwa hawezi kutembea vizuri na nilipomuuliza ndio akaanza kunielezea kilichomtokea na nikampeleka hospitali Ngoyoni ambapo alilazwe siku mbili kwa kuwa alikuwa amevimba sehemu za siri,” alidai baba huyo.

  Aidha alidai hali ya mtoto huyo bado ni mbaya kwa kuwa bado ana maumivu makali, ambayo yamesababishwa na kuvimba kwa sehemu za siri kutokana na kufanyiwa kitendo hicho kwa muda mrefu.

  Kwa mujibu wa mzazi huyo alidai kuwa mwalimu huyo aliwachukua wanafunzi wawili na kuwafanyia kitendo hicho kwa kuwapa kiasi cha Sh1,000 wote wawili na kwamba mtoto wake hali yake ni mbaya lakini mwenzeke anaendelea vizuri.

  Akizungumzia tukio hilo Mkuu wa Wilaya hiyo, Peter Toima alithibitisha kuripotiwa kwa matukio hayo na kwamba tukio hilo lilitokea Julai 27 mwaka huu ambapo mwalimu huyo alilawiti watoto wawili kwa wakati mmoja.

  Toima alisema kuwa mwalimu huyu alilawiti tena watoto wengi wawili mwezi Mei na wengine mwezi Aprili mwaka huu.

  Mkuu huyo alisema kitendo hicho kilisababisha wakazi wa eneo hilo kuandamana na kufika shuleni hapo ili kwa lengo la kutaka kumchoma moto ila polisi waliwahi na kumwokoa na kuweza kumpeleka katika kituo cha polisi.

  “Hili ni jambo la kusikitisha kwa kuwa mwalimu huyo amekuwa akihamishwa hamishwa shule kutokana na kitendo cha kulawiti watoto wa shule na huwa anawafanyia watoto wa madarasa mbalimbali,” alisema Toima

  Alisema wazazi hao waliandamana shuleni hapo Agosti 2, kwa lengo la kutaka kumchoma moto mwalimu huyo ila polisi waliwahi na kumwokoa mwalimu huyo na kwamba mwalimu anashikiliwa na polisi .

  Toima alizitaja shule za msingi ambazo mwalimu huyo amewahi kufundisha na kudaiwa kufanya matukio hayo kwa wanafunzi kuwa ni ni shule ya msingi Kimwingeni, Kiserini, Keni Mengeni na Ubetu.

  Mkuu huyo alisema mwalimu huyo akiwa anafundisha shule ya msingi alimlawiti mtoto mmoja ambaye alijulikana ambapo alikunywa sumu baada ya kufanyiwa kitendo hicho na mwalimu huyo na hivi sasa ni marehemu.

  Wazazi wa watoto hao wameiomba Serikali kumchukulia hatua kali mwalimu huyo na hata ikiwezekana kufukuzwa kazi hiyo kwa kuwa hafundishi bali anawaharibu watoto.

  Chanzo:Gazeti la Mwananchi
   
 2. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #2
  Aug 19, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  hivi hao wazazi kwa nini wasi arrange huyu mtu auwawe tu yaishe????????
   
 3. First Born

  First Born JF-Expert Member

  #3
  Aug 19, 2011
  Joined: Jul 11, 2011
  Messages: 5,315
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145
  Mbona maelezo ya polisi yanapingana na maelezo ya mkuu wa wilaya?
   
 4. H1N1

  H1N1 JF-Expert Member

  #4
  Aug 19, 2011
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 4,201
  Likes Received: 527
  Trophy Points: 280
  Hafai katika jamii,auliwe. Amejichukulia sheria mkononi wananchi amkeni kamateni sheria muulie mbali,ili mradi pawe na uthibitisho wa ushenzi huo
   
 5. D

  Dopas JF-Expert Member

  #5
  Aug 19, 2011
  Joined: Aug 14, 2010
  Messages: 1,151
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  huyo ni mgonjwa anayehitaji tiba. kufukuzwa kazi haitoshi, anahitaji kutibiwa kwani ataendeleza tabia yake hiyo kwingine. Labda kumfunga maisha anaweza kufunzwa
   
 6. C

  CUF Ngangari JF-Expert Member

  #6
  Aug 20, 2011
  Joined: Aug 11, 2011
  Messages: 273
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  huyo atafutiwe punda mumkamate punda amlawiti asikie maumivu yake labda anaweza akaacha.
   
 7. Mulhat Mpunga

  Mulhat Mpunga JF-Expert Member

  #7
  Aug 20, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 25,481
  Likes Received: 12,757
  Trophy Points: 280
  <br />
  <br />
  HATA KAMA YE ALISHIKA KORODANI ZA WATOTO ZA NINI KAMA C BAZAZI?! WAMBONYEZE NAYEYE ILI AJUE UTAMU WA KUKAWITIWA THEN PE LIFE SENTENCE PAMAV!
   
 8. Shinto

  Shinto JF-Expert Member

  #8
  Aug 20, 2011
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 1,781
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Huko Moshi kuna nini siku hizi? Mnamkumbuka yule Padri mwezi uliopita alilawiti na kumsokota uume mtoto wa seminary mpaka kumtoa damu?!
   
 9. M

  Madaraka Amani Member

  #9
  Aug 20, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 89
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Habari inasikitisha! Hivi kweli unaposoma habari hii kwa makini unagundua nini? Mimi nimeona rushwa.tena sio kwa mkuu wa polisi peke yake na hata daktari aliyeandika kuwa watoto wameshikwa kordani. Inatia huzini kuona watanzania hawathani utu wa mtu wanaendekeza rushwa wakati watoto ambao ndio nguvu kazi tunayotegemea inaharibiwa na wagonjwa wa akili kama mwalimu huyo. zamani ulikuwepo utaratibu wa mtu kustaafishwa kwa maslahi ya taifa. uamuzi huo unapofikiwa hatuhitaji mtu kutiwa hatiani na vyombo vya sheria mwalimu huyu hafai au jina lake halifai kuwa miongoni mwa watumishi wanowatumikia watanzania.
   
 10. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #10
  Aug 20, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,672
  Trophy Points: 280
  Kwa unataka kusemaje? inaonekana huyo mwalimu ni ndugu yako unataka kujenga hoja ya kumtetea.
  Dawa unachukuwa korodani zake then unapiga nyundo mpaka zinapasuka halafu unamwambie nenda
   
 11. J

  J 20A Senior Member

  #11
  Aug 20, 2011
  Joined: Apr 28, 2011
  Messages: 105
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Inasikitisha sana kuona kamanda wa polisi wa mkoa akitetea ushenzi kama huu huku watoto wetu wakiendelea kuharibiwa
   
 12. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #12
  Aug 20, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Kwa matukio yanavyojitokeza kwa sasa inaonyesha mwisho wa dunia ndo huo waja serikali ndo tegemeo letu katika hili
   
 13. Mshume Kiyate

  Mshume Kiyate JF-Expert Member

  #13
  Aug 20, 2011
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 6,774
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Watu kama hawa dawa yako ni hukumu ya kifo tu.
  Tena mnawatangazia wananchi kuwa siku ya Jumatatu uwanja wa Mnazi Mmoja ananyongwa hadharani
   
 14. Hassani

  Hassani JF-Expert Member

  #14
  Aug 21, 2011
  Joined: Jun 5, 2009
  Messages: 267
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 45
  Tatizo la kuwa na marais wanafiki,wanaogopa kutia saini za adhabu ya kifo ili wasionekani wauaji wakati wanatuua indirectly.
   
 15. Ndumbayeye

  Ndumbayeye JF-Expert Member

  #15
  Aug 21, 2011
  Joined: Jan 31, 2009
  Messages: 4,798
  Likes Received: 1,045
  Trophy Points: 280
  mzee umeshafika huko!
   
Loading...