Mwakyembe umetusaliti

Mwakyembe umetusaliti

masopakyindi

Platinum Member
Joined
Jul 5, 2011
Posts
18,590
Reaction score
14,498
Kitendo cha mhe. Mwakyembe kuingia kinyang'anyiro cha urais mnamo uchaguzi wa mwezi Oktoba kwa kweli hakieleweki.

Hakieleweki zaidi kwa wale wadau wa CCM toka mkoa wa Mbeya.

Kutoka mkoani mioyo yetu na support ni kwa mh. Mwandosya, na hili limekuwa likifahamika toka alipotangaza nia.

Siyo siri, ukiwalinganisha Mwandosya na Mwakyembe kwa kigezo cha urais, Mwakyembe bado sana.

Mwakyembe si presidential material- yet.

Si kwamba napinga demokrasia kwa kumnanga Mwakyembe kutotumia haki yake ya kimsingi, la hasha.

Ila najiuliza kwa nini amejitokeza dakika za majeruhi?

Nitakuwa wa kwanza kushangaa kama Mwakyembe atapitishwa kugombea urais na chama chake cha CCM.
JIBU ninalolipata ni moja tu.

Mwakyembe karubuniwa katika mkakati wa kumhujumu Mwandosya katka kinyang'anyiro hicho.
Simple, DIVIDE AND RULE.

Mwakyembe umeniondolea ile heshima ndogo niliyokuwa nayo kwako.
 
Kwa hiyo mmeshajipanga kimikoa na sio kumpata rais wa Watanzania wote???
 
Nasikitika sisi Morogoro atuna mtu.
 
Mwakyembe kasajiliwa dirisha dogo la Usajili. Kama Mengi na miela yote Rostam kamsainisha kwenye Team ushindi itakuwa huyo Mnyakusa
 
gawanyika,ukawa njia nyeupe ,haya ni mpango wa mungu......mwakyembe go go
 
Mimi nadhani ni mkakati wa Mwakyembe na Kaka yake Mwandosya kwa maana kwamba mwisho wa siku kundi lote la Mwakyembe litaenda kumuunga mkono Mwandosya.Tubamogele bosa bo babili. Wamethubutu na wanasonga mbele. Kyela na tukuyu oyeeeeeeee
 
Hebu tuondoleeni ukabira wenu hapa pumbavu wote.

Nchi hii hatuwezi kumpa Urais mchaga, muhaya na mnyakyusa, mnajidangany tu bado hatujasahau ukabila wa Kibona pale BOT.

Kibona alikuwa mndali wala si mnyakyusa!
 
Mwandosya kachoka amuachie tu Mwakyembe ikulu sio wodi ya wagonjwa
 
Mimi nadhani ni mkakati wa Mwakyembe na Kaka yake Mwandosya kwa maana kwamba mwisho wa siku kundi lote la Mwakyembe litaenda kumuunga mkono Mwandosya.Tubamogele bosa bo babili. Wamethubutu na wanasonga mbele. Kyela na tukuyu oyeeeeeeee

Nyie watu wakabila mno mnajulikana sana..kwa nini utuwekee kinyakyusa hapa.mimi sipendi hii tabia yenu kila mahala.
 
Namkumbuka Mwalimu Nyererr alituasa "Hatutamchagua mtu kwa sababu ya kabila lake", hakuishia hapo akaongeza pia "hatutamkataa mtu kwa sababu ya kabila lake".Pande zote mbili myaangalie haya.

Tuchague viongozi kwa sifa zao kama mahitaji ya taifa na uwezo wa binafsi kuyafanyia kazi mahitaji hayo.
 
jamani MIMI MTU WA HUKU KASKAZINI KIUKWELI DR MWAKYEMBE NI WA UKWELI HANA UTANI NA MTU NA UKWELI UNAJULIKANA JAMAA NI MCHAPA KAZI PROF MWANDOSYA AMEPOOZA SIYO KAMA SIKU ZA NYUMA SIJUI ANAUMWA BADO? ILA CCM WAKIMUWEKA DR MAENDELEO YATAONEKANA ANGALIA UCHUKUZI NDANI YA MIAKA MIWILI TU, NENDA EAST AFRICA RAIS KAGAME AMEKUWA NDUGU YETU BADALA YA ADUI HILI NI NDANI YA MIEZI MICHACHE TU MADAWA YA KULEVYA NDY USISEME WATU WALITAKA KUKIMBIA NCHI, USIMAMIZI WA MAZINGIRA WATU WALIKUWA WANAKOJOA NA KUJISAIDIA HOVYO NJIANI WAKISAFIRI HUYU BWANA ALIKOMAA MPAKA VYOO VIKANZA KUJENGWA HILI KWA SASA LIMEKUFA KAAA JAMANI PIGA UA DR MWAKYEMBE ANAFAA SANA KAMA KWELI TUNATAKA KUFIKIA KIPATO CHA KATI.
 
Mwl JK Nyerere "Hatutamchagua mtu kwa sababu ya kabila lake", hakuishia hapo akaongeza pia "hatutamkataa mtu kwa sababu ya kabila lake"

Tuchague viongozi kwa sifa zao

TUWE MAKINI SANA NA WATU WANAOANGALIA UDINI NA UKABILA NI WAKUOGOPWA.
 
jamani MIMI MTU WA HUKU KASKAZINI KIUKWELI DR MWAKYEMBE NI WA UKWELI HANA UTANI NA MTU NA UKWELI UNAJULIKANA JAMAA NI MCHAPA KAZI PROF MWANDOSYA AMEPOOZA SIYO KAMA SIKU ZA NYUMA SIJUI ANAUMWA BADO? ILA CCM WAKIMUWEKA DR MAENDELEO YATAONEKANA ANGALIA UCHUKUZI NDANI YA MIAKA MIWILI TU, NENDA EAST AFRICA RAIS KAGAME AMEKUWA NDUGU YETU BADALA YA ADUI HILI NI NDANI YA MIEZI MICHACHE TU MADAWA YA KULEVYA NDY USISEME WATU WALITAKA KUKIMBIA NCHI, USIMAMIZI WA MAZINGIRA WATU WALIKUWA WANAKOJOA NA KUJISAIDIA HOVYO NJIANI WAKISAFIRI HUYU BWANA ALIKOMAA MPAKA VYOO VIKANZA KUJENGWA HILI KWA SASA LIMEKUFA KAAA JAMANI PIGA UA DR MWAKYEMBE ANAFAA SANA KAMA KWELI TUNATAKA KUFIKIA KIPATO CHA KATI.

Zile pesa alizokwiba za mabehewa ya TRC na wewe umepata mgao?
 
masopakyindi

Mbona wote siyo presidential materials. Na hasa huyo unayempigia upatu ndiyo big ----
 
Last edited by a moderator:
masopakyindi

Kwa kweli sijaona hoja yako ndugu,
umetumia kigezo gani kumlinganisha mhe. Mwakyembe na mhe. Mwandosya
kwasababu kama ni political impact, mwakyembe yupo juu(nikimaanisha,he brought more change)
kama ni elimu, bado mwakyembe yupo juu
kama ni leadership skills, both ni viongozi but mwakyembe has been in various sectors and governmental positions and led in full effect.
and lastly kama ni kuhusu motive, i dont see whats the problem na kuchukua form mwishoni, kwasababu aliechukua mwanzo pia, sio guaranteed kwamba yeye yupo kimaslai ya jamii na sio binafsi, kwaiyo kwa wote ni kama bahati nasibu kwa mtanznia kutambua nani ndie kiongozi wa ukweli, na nani sie.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom