Mwakyembe na wenzake 'single' ya Lowassa ni fisadi imeishia kwa Rais Magufuli; Sasa tuanze 'single' mpya ya Makonda

stigajemwa

JF-Expert Member
Nov 12, 2016
449
430
Salaam,
Kwa waliosahau; Lowasa amekuwa akitajwa sana na wapinzani wake kuwa ni fisadi namba moja nchini.

Mwanzo kabisa alitajwa na kambi ya chadema kuwa ni fisadi kwa kigezo chake cha kujiuzulu kutokana na kashifa ya richimond. Hivyo chadema na kundi lake wakazunguka nchi nzima wakitangaza kuwa Lowasa ni fisadi namba moja nchini na wakamworodhesha kwenye orodha waliyoiita list of shame.

Ufisadi wa Lowasa kwa chadema na kundi lake uliishia pale Lowasa alipojiunga nao na kisha kumteua kuwa mgombea urais kwa tiketi ya UKAWA.Kilichofuata ni chadema hao hao kuzunguka nchi nzima wakisema kuwa Lowasa si fisadi na wanaosema ni fisadi waende mahakamani au walete ushahidi. Kiufupi single ya ufisadi wa Lowasa kwa chadema iliishia hapo.

Wimbo wa ufisadi wa Lowasa ukahamia kwa ccm na kundi lake. Wao walimpachika ufisadi mara tu baada ya kuihama ccm na kujiunga chadema kisha kuteuliwa kuwa mgombea urais kupitia mwanvulj wa UKAWA.Toka hapo ccm nao wakaanza kumnanga Lowasa kama fisadi.

Wimbo huu kwa upande wa ccm umekuwa ukichagizwa na Dk Mwakyembe kama mwenyekiti wa kamati ya richmond ambaye amekuwa akijinasibu kuwa ana ushahidi wa kutosha ambao ulikuwa bado kutolewa na kamati yake.
Lakini single ya ufisadi wa Lowasa kwa ccm nayo imeishia mikononi kwa mwenyekiti wa ccm Taifa. Aambaye msimamo wake ndani ya chama huwa ndio msimamo wa chama. Na ktk msimamo huo mwenyekiti wa ccm, rais Magufuli alisema kuwa Lowasa ni MTU safi yaani hana makandokando.

Hivyo kwa msimamo huo wa mwenyekiti wa ccm Taifa, maana yake ccm na kundi lake nao kwa sasa wanakiri kuwa Lowasa si fisadi. Kwa mantiki hiyo single ya Lowasa ni fisadi imekufa rasmi kwa pande zote mbili, yaani kambi ya upinzani na chama tawala.

Mwisho kabisa, baada ya single ya ufisadi wa Lowasa Kwisha sasa tuangalie single mpya ambayo imeasisiwa na Makonda.
Yenyewe inahusu ukatili wa Lowasa wa kutelekeza mtoto na mama yake. Tutarajie wapinzani wake kuanza kumtangaza Lowasa kuwa si mwadilifu kwa kutelekeza mama na mtoto.
Aksante.
 
Tujadili Tanzania ya viwanda...kwanini tunaimpott mpaka tooth pics jameni?? Jua linatukong'ori lkn hatuwezi kujitengenezea solar panel ama mitambo kadhaa itumiayo solar? Why ? Nipate majibu kabla sijakasirika tenaisifike tar. 26/04 asee
 
Fisadi ni Fisadi tu...!!! Sifa hiyo haisafishiki..hata mtu alie agalagae chini...au jiki itumike kumsafisha lakini bado atabaki na sifa yake ya UFISADI.Haya Mapya ya kutelekeza mtoto apambane na hali yake...mikashfa imezidi sasa...!.
 
Naona umesahau ile kitu ya kuvua gamba ndani ya CCM. Rostamu akasema ana achana na siasa za maji taka. Akabaki EL na Chenge. EL aka katwa wakati wa uchaguzi wa ndani-hii nafikiri ndo iliyokuwa hukumu ya EL ndani ya CCM. Chenge yeye amejikita bungeni na vyeo CCM wamempa. Kwa mawazo yangu naamini mafisadi wapo kinacho washinda ukipeleka mahakamani watanaswa hata wale ambao serikali imeamua kuwalinda kwa gharama yeyote hivyo wameamua waachane na hao wakina EL na Mzee wa Vijisenti. Na UKAWA hawawezi kuliamsha kwani EL ni mwenzao na kiongozi wao. Hivyo tusahau labda atokee mkichaa mmoja mwenye yake awashughulikie wahusika bila kujali wako upande gani.
 
Back
Top Bottom