Mwakyembe Na Usalama wa Taifa

Mwakyembe Na Usalama wa Taifa

fredito13

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2012
Posts
213
Reaction score
146
Wana JF,

Waziri wa uchukuzi Dr. Harrison Mwakyembe anafanya kazi za usalama wa taifa sasa hivi.

Ni Mwakyembe anayepambana na genge la wauza unga. Mwakyembe anapambana na wahamiaji haramu pale uwanja wa ndege wa JK Nyerere.

Sasa hivi Mwakyembe huyo huyo ameanzq kupambana na wezi wa mafuta ya serikali bandarini. Wezi hao wameunganisha mabomba kwenye matenki ya tipper na wanachukua mafuta watakavyo. Inashangaza kuona watu wa usalama wa taifa na polisi wapo na hayo yote bado yanatendeka.

Swali linalokuja hapa ni, usalama wa taifa wameshindwa kutimiza wajibu wao au Mwakyembe amewazidi ujanja kwenye kugundua na kufuatilia mambo?

Ni aibu kwa serikali yetu na vikosi vya usalqmq kushindwa kushughulikia mambo yenye athari kwa taifa, badala yake waziri wa uchukuzi ndio anafanya kazi za usalama.
 
Nadhani mwakyembe bado yupo sahihi kwani anafanya kazi hizo kwenye eneo lake la kazi. Tungeona kaenda kwenye shule za msingi na sekondari kukagua walimu waliopo maeneo yao ya kazi tungesema kaingilia wengine. Tuache majungu na kila mtu awajibike mahali pake pa kazi.
 
Hata km yeye ni TISS lakini walipaswa Ofisi ya Tiss ndo wagundue hizo habar, ila wao hawana kazi siku hiz Nchi imeoza kwa unga,wahamiaji, na matukio ya vioja.

Zaman walipokuwa wanasema Nyerere anamasikio hata ukitaja jina lake kibandani kwako anajua maana yake Tiss ilikuwa inafanyakazi vizuri
 
lakini pia inawezekana hao ndio wanaompa taarifa hizo nae anazifanyia kazi!
 
Mwakyembe anafanyia kazi taarifa anazopata na TISS.
 
lakini pia inawezekana hao ndio wanaompa taarifa hizo nae anazifanyia kazi!

Sure Mkuu,. Nasikia siku hizi TISS wameamua kuwasaidia moja kwa moja badala ya kushauri tu. Big Up sana TISS
 
Lazalaza, nqkubaliana na wewe. Kama usalama wa taifa wasingekua makini miaka ya nyuma, basi lile jaribio la mapinduzi (uhaini) wakati wa Nyerere lingefanikiwa. Sasa hivi usalama wa taifa wako makini kufuatilia vyama vya siasa a migomo ya wafanyakazi. Hawako makini kulinda usalama wa nchi kama vile wanavyopaswa kufanya. Unga, ujambazi kwenye mabenki, ofisi kubwa na matukio mengine ya ajabu yangepatiwa suluhisho mapema kama kweli tungekua na usalama wa taifa.
 
Wana JF,

Waziri wa uchukuzi Dr. Harrison Mwakyembe anafanya kazi za usalama wa taifa sasa hivi.

Ni Mwakyembe anayepambana na genge la wauza unga. Mwakyembe anapambana na wahamiaji haramu pale uwanja wa ndege wa JK Nyerere.

Sasa hivi Mwakyembe huyo huyo ameanzq kupambana na wezi wa mafuta ya serikali bandarini. Wezi hao wameunganisha mabomba kwenye matenki ya tipper na wanachukua mafuta watakavyo. Inashangaza kuona watu wa usalama wa taifa na polisi wapo na hayo yote bado yanatendeka.

Swali linalokuja hapa ni, usalama wa taifa wameshindwa kutimiza wajibu wao au Mwakyembe amewazidi ujanja kwenye kugundua na kufuatilia mambo?

Ni aibu kwa serikali yetu na vikosi vya usalqmq kushindwa kushughulikia mambo yenye athari kwa taifa, badala yake waziri wa uchukuzi ndio anafanya kazi za usalama.

mkuu unatumia akili za upande gani kufikiri unajua mwakyembe hizo tarifa anazipata wapi hizo tarifa,

mwakyembe anapewa tarifa na vyombo husika ndipo anafanyia kazi au wewe unadhani hizo tarifa anapewa na yesu,

Labda tusaidie mkuu usalama wa taifa ni nani,wepi,wapoje na wanafanyeje kazi zao ili tulinganishe na kazi za mwakyembe.
 
Fikiria, upanga wa dhahabu umeibiwa ofisini kwa IGP... Ofisini. Ofisi kubwa kama hiyo inaibiwa kitu chenye thamani kubwa kama hiyo, usalama wa taifa wako wapi?
 
Hata km yeye ni TISS lakini walipaswa Ofisi ya Tiss ndo wagundue hizo habar, ila wao hawana kazi siku hiz Nchi imeoza kwa unga,wahamiaji, na matukio ya vioja.

Zaman walipokuwa wanasema Nyerere anamasikio hata ukitaja jina lake kibandani kwako anajua maana yake Tiss ilikuwa inafanyakazi vizuri

unaushahidi kuwa tiss hawagundui mbona siku ile mwakyembe aliomba kufika leo apatiwe majina ya wahusika wa wezi wa mafuta kwa maoni yako alikuwa anawaagiza akina nani kama siyo vyombo husika.
 
Swali linalokuja hapa ni, usalama wa taifa wameshindwa kutimiza wajibu wao au Mwakyembe amewazidi ujanja kwenye kugundua na kufuatilia mambo?

Ni aibu kwa serikali yetu na vikosi vya usalqmq kushindwa kushughulikia mambo yenye athari kwa taifa, badala yake waziri wa uchukuzi ndio anafanya kazi za usalama.
kuna cha ajabu kwa serikali kushindwa, refer EPA, madawa ya kulevya na mengine unayoajua!
 
Mwakyembe ni mtu mwenye UWEZO mkubwa sana na amejaliwa kipaji hicho na Mungu, siyo siri.

Bahati mbaya huwa hataki tu kukitumia au kukitumia kwa nadra sana.

Wanaomfahamu kwa ukaribu wote wanakubaliana kwa hilo.
 
TISS wanapiga kazi sana, tofauti na watu mnavyo wachukulia, isipo kua hawa jamaa wamenyimwa meno...
 
Wana JF,

Waziri wa uchukuzi Dr. Harrison Mwakyembe anafanya kazi za usalama wa taifa sasa hivi.

Ni Mwakyembe anayepambana na genge la wauza unga. Mwakyembe anapambana na wahamiaji haramu pale uwanja wa ndege wa JK Nyerere.

Sasa hivi Mwakyembe huyo huyo ameanzq kupambana na wezi wa mafuta ya serikali bandarini. Wezi hao wameunganisha mabomba kwenye matenki ya tipper na wanachukua mafuta watakavyo. Inashangaza kuona watu wa usalama wa taifa na polisi wapo na hayo yote bado yanatendeka.

Swali linalokuja hapa ni, usalama wa taifa wameshindwa kutimiza wajibu wao au Mwakyembe amewazidi ujanja kwenye kugundua na kufuatilia mambo?

Ni aibu kwa serikali yetu na vikosi vya usalqmq kushindwa kushughulikia mambo yenye athari kwa taifa, badala yake waziri wa uchukuzi ndio anafanya kazi za usalama.

Usalama wapo kwa ajili ya kumlinda Rais na usalama wa taifa hayo mambo ya wezi sio wao watafute polisi ndio kazi yao
 
kwani nani hasa anajua kazi za usalama na mipaka yao?manake muweweseko mwingi hapa naona.
 
Fikiria, upanga wa dhahabu umeibiwa ofisini kwa IGP... Ofisini. Ofisi kubwa kama hiyo inaibiwa kitu chenye thamani kubwa kama hiyo, usalama wa taifa wako wapi?

Wewe huna taarifa sahihi! Upanga ule haukuibiwa ofisini kwake . Alikabidhiwa Zanzibar na akauweka kwenye gari la kamishna wa Zanzibar ndio walioupoteza na sio ofisini kwake

Taarifa hii mwambie na mwenzako hapo pembeni yako! Ajue
 
Usalama wapo kwa ajili ya kumlinda Rais na usalama wa taifa hayo mambo ya wezi sio wao watafute polisi ndio kazi yao

Unga sio suala la usalama wa taifa? Wageni kupewa vitengo nyeti kwenye ajira haliwahusu usalama wa taifa? Upanga kuibiwa ofisi ya Mkuu wa jeshi la polisi usalama hawahusiki? Na yanayowatokea viongozi wa dini usalama hawatakiwi kujua mhusika? What a shame!!!!
 
Back
Top Bottom