Wakuu,
TISS huwa hakamati mtuhumiwa yoyote yule, wao hutoa taarifa kwa chombo husika ili wachukue hatua na kutahadharisha.
TISS kitengo cha usalama wa viongozi, itokeapo aina ya uhaini au uasi...hapo jamaa huua pasipo mashauriano.
Inawezekana Mwakyembe amepora taarifa zinazoliendea jeshi la polisi au hupewa nakala ya taarifa za uhalifu zinazokwenda jeshi la polisi. Kwa kupitia taarifa hizo, na kwa jinsi muundo wa jeshi letu ulivyo, ndipo huamua kuchukua hatua mwenyewe.
Nchi hii, takriban 80% ya wanasiasa wote ni agents wa TISS hususan wale viongozi wakuu wa vyama vya siasa. Hata huu muungano wa CUF, NCCR na CDM utaparanganyika siku chache kabla ya uchaguzi na hawatoweza kujipanga kwa kuwa na nguvu ya kuhimili uchaguzi mkuu.
Pale TISS kuna vitengi vingi sana ambapo kila kitengo hutoa taarifa zao sahihi kabisa, tatizo ni kwamba TISS ni aghalabu kabisa kujitokeza kwenye vyombo vya habari na kuelezea jambo lolote isipokuwa kwa ulazima sana sana.
Hivyo, Mwakyembe kwa afanyayo ni kwa muongozo wa karibu kabisa aupatao toka TISS.
Cabinet ministers huwa takriban 50% ni TISS agents pasipo kujuana, TISS hutakiwa kujua kila kitu kinachoihusu nchi ndani ya mipaka na nje ya mipaka.