Mwakyembe msomi ovyo sana! Muziki ni zaidi ya Entertainment! acha uwongo!

TL. Marandu

JF-Expert Member
Jul 12, 2015
3,625
5,810
Mawaziri wengi walio na Taaluma na Uwezo, Ungelidhania sio Watu wababaishaji na wa Kupelekeshwa! Ila kwa kutokana na Sifa na Heshima anayokuwa nayo Mtu akiwa na Wadhifa wa Uwaziri basi wanakuwa njia panda pale Mambo yanavyoenda, Nimnukuu Rais Mwinyi Kama Gari lisilo na Usukani. Ila kwa Bahati mbaya Sana Wapo Wengine ambao ni Ovyo sana na Wababaishaji kama Harrison Mwakyembe. Hawa ndio waliouza nchi ndani ya Kikapu cha mkononi!

Ila Ninaona huko tuendako Mawaziri watakaobakia na watakaorukia Kuchaguliwa ni aina ya Mwakyembe ili aseme hakuna Mwanamziki aliyefanikiwa kwa Kuimba siasa! Kwake yeye Bob Marley, Alpha Blondy, Remmy Ongala, Sonny Okusun, Mbaraka Mwinshehe, Madona, Lucky Dube, Tupac Shakur, Kakai Kilonzo, Ivon Chaka Chaka, Miriam Makeba, Oliver Mutukudzi, etc Wote hawa hawajawahi kuwepo! Au kama walikuwepo hawajawahi kufanikiwa. Muziki ni Kielelezo cha Utamaduni, Kama ilivyo Tamthilia za Vitabuni, Senema na Mashairi, Na Lengo Lake ni a) KUONYA, B) KUFUNDISHA, C)KUBURUDISHA, D) KUREKEBISHA JAMII. Yeye Mwakyembe anaona Muziki kazi yake ni Entertainment Tu!

Mwakyembe unataka kusema hata Nyimbo za Mchakamchaka zilikuwa ni za Kijinga? Maana zilikuwa ni Zaidi ya Kuburudisha, Na za kukimbiza mwenge? Poor Weasel Mwakyembe!

Anachonishangaza Mwakyembe ni Mbwembwe anazotumia akiwa anajiongelesha Utumbo! Kuna wakati nawaza hata ningekuwa Sokwe! Huyu Jamaa nisingempa PHD ya nini? Si kuaibisha Taaluma na Wazimu wa ajabu!


Afriki (Ubaguzi wa Rangi ni Unazi) Alpha Blondy


Peace in Liberia Alpha Blondy


Zimbabwe Marley


Free Nelson Mandela Amy Winehouse


Sowetho by Ivon

Mama Land Ivon Chakachaka


Confession Maddona


Get up standup! Markey


Mrema Remmy Ongala


Wasakara ie Umezeeka Oliver Mutukudzi anamwambia Mugabe, Wasakara!


Tell them, power to the people, Soweto etc. Sonny Okusun



Miriam Makeba Akihutubia UN, 1963, Kama haya sio Mafanikio ni Lini UN watakaa na Kusikiliza Masokwe wenye PHD

Nina Uhakika Kama Nyimbo za sasa Tanzania Zingekuwa Kama hizi Mwakyembe angewahamasisha wengine waimbe mfano wa huyu! Maana Pamoja na Kuwa alikuwa Stooge wa Moi, bado alifanikiwa sana, Hivyo dhana kuwa Ukiimba siasa Huwezi fanikiwa Ni Upuuzi hadaa na Vitisho!



Kakai Kilonzo

Nakumbuka Nyimbo kama Zimbabwe na Namibia ni kwa Waafrika, Ondoka Ondoka Kaburu yoyoyooo! Mwakyembe alikwa wapi Enzi za Harakati za Nchi za Mstari wa Mbele au ukombozi wa SA? Miziki ilichangia kwa Kiasi gani?
 
Ni wa kusamehewa bure na mwishoni kabisa ni wa kupuuzwa tu ili mambo yaende
 
  • Thanks
Reactions: MTK
Halafu anapoongea kwa majigambo kujifanya yeye ndiye mjuaji kuliko wote kumbe ni bonge la ji.ga. Ndiyo maana nakubalina na Shivji kuwa kuna watu wana vyeti original lakini wanaelimu fake. Na hawa ndio hatari kuliko hao wenye vyeti fake lakini wengi wao walikuwa na uelewa wa hali ya juu sana kuliko hata hawa wanaoringia Phd zao wakati kichwani ni weupee na hekima na busara hawana kabisa
 
different colour same people, wa luck dube kupiga siasa za ubaguz Sauz Afrika. mzee tahra yule
 
May be mada yake Dr Mwakyembe haikueleweka kuhusu wanamuziki na siasa kwa Sasa nasema labda dhana yenyewe hawajaielewa!!
 
Mamoderator Wakifuta hii Wataniua kwa Pressure kwa Maana nilikuwa Nime mind Mwakyembe Kinoma ila Nikawa niko bussy! Hakuna wananichefua Kama wanajinadi kuwa ni Wasomi huku Kila wakifungua Mdomo wanajaza Mainzi
 
Mtoa mada una hoja ya msingi sana na yenye kujenga....lakini jazba zinakuweka mbali na ustaarabu wa wasomi

Tambua kuwa nje ya uwaziri au cheo chochote ni mwanadamu kama wewe na anaweza akakengeuka na ukamuweka sawa kama ambavyo wewe unavyolifahamu jambo hilo....na huo ndio ukomavu wa kiakili na kiutu uzima.....

Tofauti za kimitazamo ya kisiasa zisikufanye uonekane mjinga hali ya kuwa wewe ni msomi na mwerevu wa mambo.....

Nimependa andiko lako

Bravo....
 
Mtoa mada una hoja ya msingi sana na yenye kujenga....lakini jazba zinakuweka mbali na ustaarabu wa wasomi

Tambua kuwa nje ya uwaziri au cheo chochote ni mwanadamu kama wewe na anaweza akakengeuka na ukamuweka sawa kama ambavyo wewe unavyolifahamu jambo hilo....na huo ndio ukomavu wa kiakili na kiutu uzima.....

Tofauti za kimitazamo ya kisiasa zisikufanye uonekane mjinga hali ya kuwa wewe ni msomi na mwerevu wa mambo.....

Nimependa andiko lako

Bravo....
Usimwombee Po! Ustaarabu gani alionao Wa kumwambia Lowassa atamnyoa Kwa Chupa. Mimi wahuni wanafiki nawajibu kwa staili yao 10x over ndio Language wanaielewa!
Nikushauri Soma Bio au sikiliza Bio ya Martin Luther, sio yule sa US bali yule Aliyemaliza Uhuni wa Kuuzia watu Paradiso! Usinipangie Staili ya kuongea Nakuomba sana! Nimesha Reply post zako nyingi je nilisha kuvunjia heshima? Sina Jazba ninafanya kwa makusudi.
 
Usimwombee Po! Ustaarabu gani alionao Wa kumwambia Lowassa atamnyoa Kwa Chupa. Mimi wahuni wanafiki nawajibu kwa staili yao 10x over ndio Language wanaielewa!
Nikushauri Soma Bio au sikiliza Bio ya Martin Luther, sio yule sa US bali yule Aliyemaliza Uhuni wa Kuuzia watu Paradiso! Usinipangie Staili ya kuongea Nakuomba sana! Nimesha Reply post zako nyingi je nilisha kuvunjia heshima? Sina Jazba ninafanya kwa makusudi.

Sawa ndugu uwe na wakati mwema....
 
Inawezekana Mwakyembe hakueleweka....au uelewa wake juu ya masuala aliyokuwa akiyazungumzia ni mdogo......

Alifanya Makusudi. Mtu anayekunywa Dawa ya kuharisha na kisha anajipaka chemical ili nywele zinyonyoke na ajifanye kapewa sumu ili Aonewe huruma apate kiki ya kugombea Urais 2015. "Nimewekewa Polonium, The hell Polonium Tanzania? Na nani anaweza kutumia Sumu ya gharama namna hiyo kwa mtu kama huyu? Second if someone use Polonium on you huchomoki. Unanyanyuka in few hrs. Alizoea kudanganya huyu!
 

Alifanya Makudi. Mtu anayekunywa Dawa ya kuharisha na kisha anajipaka chemical ili nywele zinyonyoke na ajifanye kapewa sumu ili Aonewe huruma apate kiki ya kugombea Urais 2015. "Nimewekewa Polonium, The hell Polonium Tanzania? Na nani anaweza kutumia Sumu ya gharama namna hiyo kwa mtu kama huyu? Second if someone use Polonium on you huchomoki. Unanyanyuka in few hrs. Alizoea kudanganya huyu!


Nimekuelewa ndugu.....na nayaheshimu mawazo yako siku zote humu jamvini kwani huwa unajibu kwa weledi wa hali ya juu sana....watu wanaojitoa fahamu ilihali wana fahamu zao wasikutoe kwenye mstari ndugu yangu......
 
Back
Top Bottom