relis
JF-Expert Member
- May 24, 2015
- 3,187
- 4,762
Asumie neno msikitini afadhali kidogo aseme tu misikitini wanavaa kistaarabu ila kanisani Mungu wetu hajali hata tukienda uchi kabisa imani ni moyoni,ngoja tuache wafu mzikane.Waziri Harrison Mwakyembe amefanya mkutano na viongozi wa madhehebu ya dini wenye lengo la kujadili "Imani na Uzalendo Kuelekea Uchumi wa Viwanda"
Mwakyembe ameongea haya:-
Dk Harrison Mwakyembe: Tunapozungumzia uzalendo, tunazungumzia mtu na uchungu wa Taifa lake.
Maadili ya taifa yatazidi kumomonyoka kama viongozi wa dini hamtasimama kidete kukemea na kuwajenga watu wetu kimaadili. Leo hii watoto wetu wanaangalia picha chafu katika simu zao za mkononi halafu tunasingizia utandawazi, hili halikubaliki. Tushirikiane katika kukemea upotoshaji wa maadili kwa kusingizia utandawazi
Mavazi ya watu wetu siku hizi katika makanisa yanakuwa changamoto, ni afadhali kidogo katika misikiti ambako wanavaa kistaarabu. Mkutano huu ndo uwe kioo cha kurekebisha hali hiyo. Viongozi wetu tuwe mstari wambele katika kurekebisha mavazi ya waumini wetu ili kurudisha maadili ya taifa. Nawaomba msichoke kuimba kuhusu mavazi stahiki yanayoendana na maadili ya taifa.
Chanzo: Habari leo facebook