Tume ya kurekebisha sheria ni injini ya sekta ya sheria nchini

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,801
11,961
 LRCT ni taasisi ya Serikali, ni mali ya umma siyo mali yenu

 Tumieni nafasi zenu kutumikia wananchi

 Mtumishi wa umma hauna hati miliki na taasisi ya umma

 Tumikieni wananchi kwa kuzingatia maadili

Na Mwandishi Wetu,

LRCT Dar es Salaam Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania (Law Reforms Commission of Tanzania – LRCT) ni injini ya Sekta ya Sheria nchini ambayo imeundwa na Serikali na kukasimiwa majukumu ya kurekebisha sheria nchini ili kuhakikisha uwepo wa haki na maendeleo ya taifa kwa wananchi ambapo ni vema kutekeleza majukumu kwa kuzingatia maadili, sheria, taratibu na kanuni za utumishi wa umma.

Hayo yameelezwa na Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (Mb.), Waziri wa Katiba na Sheria wakati akifungua mkutano wa kikao kazi cha mafunzo baina ya viongozi wa Wizara na watumishi wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania yanayofanyika kwa siku tatu kuanzia leo kwenye ukumbi wa Ofisi za Bunge, Dar es Salaam.

Waziri Dkt. Ndumbaro amesema kuwa LRCT ni injini ya kurekebisha sheria nchini hivyo amewataka watumishi kutambua kuwa wamebahatika kupewa jukumu la kufanya kazi kwenye Tume na amewahimiza kuzingatia maadili, sheria, taratibu na kanuni za utumishi wa umma kwa vitendo, kwa kujitoa sadaka na kutumikia cheo alichopewa ili kuwapatia wananchi huduma stahiki.

“Hii ni taasisi ya umma, na siyo ya kwenu binafsi, lazima msimame kwenye sheria, taratibu na kanuni na siyo kutoka nje ya sheria, taratibu na kanuni kwa kuwa sisi wote ni watumishi wa umma na hakuna mwenye hati miliki ni muhimu mfanye kazi kwa kuzingatia uzalendo, tuchape kazi kwa bidii, tuheshimu mamlaka ili kuifanya Tume ing’ae, iendelee kuwa na thamani na kukubalika”, amesisitiza Dkt. Ndumbaro.

Naye Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Bi. Mary Makondo amesema kuwa viongozi na watumishi wa Tume watapatiwa mafunzo kuhusu maadili kwa watumishi wa umma; utawala bora; na kutokomeza rushwa katika utumishi wa umma; ambapo lengo la Wizara kutoa mafunzo hayo ni kuhakikisha mafunzo hayo yanawawezesha kutekeleza majukumu yao kisheria kwa ajili ya haki na maendeleo ya taifa letu ili kuwa na uwajibikaji kwa kuzingatia maadili ya watumishi wa umma na mafunzo hayo yanatolewa na Ofisi ya Rais – Ikulu; Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora; TAKUKURU; na Sekretariati ya Viongozi ya Maadili ya Umma.

Akitoa neno la shukrani kwa niaba ya Tume, Mwenyekiti wa Tume hiyo, Mhe. Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Januari Msofe amesema kuwa Tume imezingatia maelekezo ya Waziri Dkt. Ndumbaro hususani masuala ya maadili kwa kuwa maadili ni kila kitu, maadili ni popote iwe nyumbani, kazini na mbele ya jamii hivyo pamoja na mafunzo yaliyotolewa leo viongozi na watumishi wametambua kuwa ni muhimu kuendelea kujifunza ili kuweza kutekeleza vema majukumu na kuhudumia wananchi.

Naye Katibu Mtendaji wa Tume hiyo, Casmir Kyuki ameishukuru Wizara kwa kuendeleza utaratibu wa kusimamia Tume hiyo na anaamini kupitia mafunzo hayo watumishi watatoka na mwamko mpya wa kutekeleza majukumu.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania.
IMG_20221220_001630_997.jpg

Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Damas Ndumbaro akizungumza na viongozi wa Wizara na watumishi wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania wakati akifungua mafunzo ya siku tatu kwa watumishi hao kuhusu Sheria, Taratibu na Kanuni za Utumishi wa Umma yanayofanyika Jijini Dar es Saalam.

PICHA NA. 2 .JPG

Mwenyeketi wa Tume ya kurekebisha Sheria Tanzania, Mhe. Jaji Mstaafu January
Msofe, akizungumza wakati akichangia mada katika mafunzo ya siku tatu kuhusu
Sheria, Taratibu na Kanuni za Utumishi wa Umma yanayotolewa kwa watumishi wa
Tume hiyo yanayofanyika Jijini Dar es Saalam.

PICHA NA. 3 .JPG

Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Bi. Marry Makondo akizungumza na viongozi wa Wizara na watumishi wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania wakati akifungua mafunzo ya siku tatu kuhusu Sheria, Taratibu na Kanuni za Utumishi wa
Umma yanayofanyika Jijini Dar es Saalam.

PICHA NA. 4.JPG

Mkurugenzi wa Idara ya Huduma za Sheria kwa Umma wa Wizara ya Katiba na Sheria, Griffin Mwakapeje, akichangia mada kuhusu Maadili katika Utumishi wa Umma wakati wa mafunzo ya siku tatu kuhusu Sheria na Taratibu za Utumishi wa Umma yanayotolewa kwa watumishi wa Tume hiyo yanayoendelea Jijini Dar es Salaam.
 
Hiyo Tume ni kijiweni, bajeti ndogo, halafu wanaotakiwa kufanya hayo marekebisho most of them ni juniors. Ilitakiwa watoke katika taasisi mbalimbali waje na uzoefu.

Pia mshahara kiduchu.

Kuna wadada katika Ofisi hiyo ilifikia muda wakawa wanadanga kwa jamaa mmoja ambaye baadae alikuwa balozi. Full kununiana
 
Alidanga sababu ya mshahara au mapenzi tu
 
Alidanga sababu ya mshahara au mapenzi tu
Kuna mtu anadanga sababu ya mapenzi?

Ila jengo lao pale HAKI HOUSE no moja kati ya majengo bora kabisa.

Wana kazi ngumu sana kuandaa paper, ziende kwa full commission, zipite, waingie saiti.

That Tume, sometimes naiona kama Jack of trades, master of none.

Wanahitaji humo ndani wawe na specialisation ili wajue the minute details ya wanachotafiti.

Na pia kama wizara ikiona ni sawa, hao state attorney wawe wana rotate, kesho wako AG Chambers, baada ya muda Solicitor General, DPP, waende mawizara tofauti, itasaidia kuwapanua mawazo, na kuleta experience mpya.

Mtu akitoka wizara fulani, anajua changamoto za kisheria za wizara hiyo, anajenga wazo pale tume, and the like.

Na pia itaondoa hali ya tume kujiona mtoto wa kambo wa Wizara ya sheria.

Zamani walikuwa wanatembelea Law Reform Commission mbalimbali duniani. Pia nadhani waziombe zifanye audit ya kiutendaji ya Tume ili iendane na international best practice.
 
We ni mwana tume nini
 
Hebu waifanyie reform chap na waifute ikiwapendeza Ile Sheria ya jenister mhagama ya kikokotoo na ya fao la kujitoa kwani no kinyume na haki za binadamu!
 
Back
Top Bottom