Mwakyembe hali tete Jimboni kwake Kyela

Mwakyembe hali tete Jimboni kwake Kyela

ccm wana hali mbaya sana kuna uwezekano mkubwa sana wabunge wa kuzomewa na kupigwe na chupa majimboni mwao
 
Hata mseme nini,Mwakyembe amepaboresha bandarini, anaendelea kuifufua ATC na TRL.
Mtu ukiwa na nia njema basi angalau ungetaja hata treni ya dar kama ni sehemu ya mafanikio yake.
Mimi katika mawaziri ninaowakubali wa kwanza ni Mwakyembe.Anafanya maamuzi sahihi sana katika mazingira magumu.
 
Mwakyembe hafai kabisa. Sasa hivi ni Fisadi wa kutupwa: Kwenye taasisi zote zilizo Chini ya Wizara yake kaweka watu wake wote ili wale vizuri. Mapande (ambaye ni DG) wa Bandari ni mtu wake wakaribu sana pindi wakiwa Wizara ya ujenzi: DG wa Sumatra ni Class mate wake, DG wa TCAA ni rafiki yake wa Karibu sana. Na ufisadi anaofanya kila mwezi kuna fungu kutoka kwa taasisi zote zilizokuwa chini yake baadhi nimezitaja hapo juu. Anamtumia mama mmoja yuko pale wizarani anaitwa Tumpe Mwaijande kukusanya mafungu anayolipwa kifisadi (Tumpe wanatoka naye kijiji kimoja na Director of Maritime safety and security): Baada ya kupewa Uwaziri alitumia mbinu ya kutafuta popurality kwa kuwatimua wale jamaa ili aaminike kuwa ni mtu safi. Lakini siyo safi kabisa. Kwanza kipindi amepropose Jina la Mapande kuwa DG wa mamlaka ya bandari alipewa ushauri kutoka vyombo vinanvyomjua Mapande asivyo safi akakataa ushauri kalazimisha. Kumbe alikuwa na ajenda yake ya siri.

Jamaa hana chembe ya uadilifu kabisa...

Yeye na sitta ni wanafiki Sana wanaojipambanua wasafi kumbe wachafu Kama vyoo...

Huyo 6 kakimbia na mamilioni ya BMK bado anachekewa....

Huyo Tumpe Mwaijande mumewe ndo yule Mwaijande Wa Shirika la bima?
 
Nimeyapata matokeo ya jimbo la Kyela thibitisheni kama ni kweli au fix.

Matokeo ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wilayani
Kyela.Jumla ya Vijiji ni 90,CCM wamepata 79 na
CHADEMA 11.Jumla ya Vitongoji ni 401,CCM
wamepata 310 na CHADEMA 84 Vitongoji 5 bado
kufanyika Uchaguzi.
 
Vipi akitangaza nia ya Urais wa TZ? Huenda hii ikawa ndio dhamira yake!
 
Nimeyapata matokeo ya jimbo la Kyela thibitisheni kama ni kweli au fix.

Matokeo ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wilayani
Kyela.Jumla ya Vijiji ni 90,CCM wamepata 79 na
CHADEMA 11.Jumla ya Vitongoji ni 401,CCM
wamepata 310 na CHADEMA 84 Vitongoji 5 bado
kufanyika Uchaguzi.

ah ha ha ha ha mkuu tuthibitishe nini tena wakati wewe ndio umeyapata? Umenichekesha Sana.
 
Nimeyapata matokeo ya jimbo la Kyela thibitisheni kama ni kweli au fix.

Matokeo ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wilayani
Kyela.Jumla ya Vijiji ni 90,CCM wamepata 79 na
CHADEMA 11.Jumla ya Vitongoji ni 401,CCM
wamepata 310 na CHADEMA 84 Vitongoji 5 bado
kufanyika Uchaguzi.

kama ungethubutu kujisumbua kujua idadi ya kura ambazo UKAWA wamepata wala usingehangaika kutaja idadi ya mapori ambayo ccm wameshinda , labda kwa ufafanuzi tu ni kwamba UKAWA imechukua halmashauri ya mji wa kyela ! Kumbuka KWAMBA HAPO NDIO PENYE KILA KITU .
 
Mpaka sasa hivi sijaona point ya msingi kabisa kuhusu Dr Mwakyembe na kumsema na ku mkashifu hasa kipindi hiki kwani siku zote mlikuwa wapi?

Ati mnamwita fisadi sijui mmnamaanisha nini maana mtu akiwa fisadi huleta maendeleo ya kifisadi jimboni kwakwe mfano mzuri upo kwa mafisadi kama tunavyo jua nenda monduli nenda bilikana pale town utaona mafisadi.

Ukiangalia Tanzania sawa kuna maeneo yana vijimaendeleo na si maendele kama watu wanavyo taka kutuaminisha hii inatokana na watu wachache kuwa wanamiliki uchumi wetu nchi yetu inategemea sana misaada nayo ukikaa vibaya huwafikia watu wachache sana ukiangalia mmbunge hata kama yuko vizuri vipi huwa yeye kama yeye hawezi leta maendeleo ya sehemu husika isipokuwa wananchi wenyewe wanatakiwa kuchangamka na wawaelekeza viongozi wanataka nini uku wakionesha mifano leo hii mnakaa chini na kuaminishwa eti tumng'oe Mwakyembe ndiyo tutapata maendeleo wanakyela mnapotea kabisa

Mwiteni Mbunge mwambie tumekuchagua tunataka moja mbili tatu huku mkifutilia na kuanza kulishughulikia hilo jambo apo mtaona mambo yanakwenda bila hivyo mtaishia kulalamika na kubadili viongozi na vyama ambavyo havisaidii kitu

USHAURI WANGU KWA WANAKYELA
kubadili viongozi na vyama si suruhisho kama ni suruhisho nipeni mifano mitatu hai ya wilaya au mkoa wenye maendeleo kwa kufanya mabadiliko kila kukicha

la msingi ni kuitisha mkutano wa Kyela nzima kisha mwiteni mkuu wa mkoa mbunge DED na viongozi wote kujadili matatizo sugu ya Kyela wapi panaposumbua nanianaye sumbua suluhisho ni lipi hapo mtaona maendeleo makubwa vitu vingine vingi vipo ndani ya uwezo wa wanakyela na si kunywa pombe na kutukana tu.

PIA KUNAMAKUNDI MBALIMBALI YAMEVAMIA KYELA YAPASA KUWA MAKINI
sasa hivi kuna makundi ya Urais kupitia vyama yakipita huku na huko kuakikisha yanaendelea kualibu na kutufanya tuwe masikini.

Mkuu...naona KISU kimefika kwenye MFUPA povu zinamwagika sikidogo.....mnaogopa mabadiliko ingekuwaje ww kwa umri ulionao hadi sasa ungekuwa unanyonya ziwa la.MAMA acheni.woga mabadiliko ni LAZIMA
 
Jamaa hana chembe ya uadilifu kabisa...

Yeye na sitta ni wanafiki Sana wanaojipambanua wasafi kumbe wachafu Kama vyoo...

Huyo 6 kakimbia na mamilioni ya BMK bado anachekewa....

Huyo Tumpe Mwaijande mumewe ndo yule Mwaijande Wa Shirika la bima?

Mwakyembe na 6 walikuwa wanapiga mayowe kwaajili ya NJAA tu huyo Fisadi wa BMK imebidi apotee baada yakukwapua mabaki ya BMK anasubiri mwaka 2015 aibuke
 
Mwakyembe hafai kabisa. Sasa hivi ni Fisadi wa kutupwa: Kwenye taasisi zote zilizo Chini ya Wizara yake kaweka watu wake wote ili wale vizuri. Mapande (ambaye ni DG) wa Bandari ni mtu wake wakaribu sana pindi wakiwa Wizara ya ujenzi: DG wa Sumatra ni Class mate wake, DG wa TCAA ni rafiki yake wa Karibu sana. Na ufisadi anaofanya kila mwezi kuna fungu kutoka kwa taasisi zote zilizokuwa chini yake baadhi nimezitaja hapo juu. Anamtumia mama mmoja yuko pale wizarani anaitwa Tumpe Mwaijande kukusanya mafungu anayolipwa kifisadi (Tumpe wanatoka naye kijiji kimoja na Director of Maritime safety and security): Baada ya kupewa Uwaziri alitumia mbinu ya kutafuta popurality kwa kuwatimua wale jamaa ili aaminike kuwa ni mtu safi. Lakini siyo safi kabisa. Kwanza kipindi amepropose Jina la Mapande kuwa DG wa mamlaka ya bandari alipewa ushauri kutoka vyombo vinanvyomjua Mapande asivyo safi akakataa ushauri kalazimisha. Kumbe alikuwa na ajenda yake ya siri.

DUH ! EEE BHANA EEE ! Hii NI NOMA SANA !
 
Hata mwaka 2010 alipata kura za ulaghai. Ilikuwa akiwa kwenye mikutano yake ya kampeni, wananchi wakimwuliza mfano "Sisi hapa tunatatizo la maji...." anachojibu ni kwamba, tayari ameshaongea na waziri wat maji na mradi wao ni kipaumbele cha serikali. Halfu anaweka simu kwenye laud speaker, anawaambia wasikilize akiongea moja kwa moja na waziri mwenye dhamana. Anaanza kusema, "Hallo mheshimiwa, niko hapa nyumbani, wananchi wangu wanaomba kufahamu suala la maji limefikia wapi, naomba useme moja kwa moja waskisikia", . Sauti ya upande wapili inasema, "waambie wasiwe na wasiwasi, tayari nnimeshatoa maelekezo na mkandarasi.....blah blah..... atakuwa hapo kuanzia tarehe.....", . Mwakyembe angesema mmesikia wenyewe? Wapiga kura wake wangeitikia "Ndiyooooooooo!:.

Sehemu moja sauti ya pili ilijibu "Tayari vifaa vya ujenzi wa hilo daraja vimeshapakiwa kwenye magari vinakuja...".

Mara waziri wa ujenzi angejibu kwenye hiyo simu " Ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami uko katika budget yetu na mwezi wa kwanza unaanza rasmi huko".

Mwakyembe ni mafia. Safari hii atapanga mawaziri wa kwenye simu waseme nini tena? Mtaji wa uowongo wake umebuma kyela.
​Hii kiboko kama kweli alifanya hivyo.
 
Mbuge wa Kyela bwana Harrison Mwakyembe mambo yanamwendea kombo jimboni kwake. Juzi alizuiwa kwa Mawe na magogo na wanaichi wa Kyela na gari yake kumwagiwa pombe huku wakipiga kelele kuwa hawamtaki tena kwa kushindwa kutekeleza hata robo ya ahadi alizozihaidi siku za kampeni .

Alihaidi kiwanda cha juisi za embe na chungwa, meli ,kiwanda cha kugred mchele,barabara ya lami toka Kyela hadi Matema.

Chanzo mimi mwenyewe

Amelaaniwa amtumainiye mwanadamu na kumfanya kuwa kinga yake asema Bw wa majeshi.... Yeye na Six Mungu awasamehe lakini they shall rip what they sow!
 
Tulimtahadharisha mapema sana kwamba kyela tunataka uhamasishaji wa maendeleo wa kibunge , tulitaka mtu atakayekuwa kiongozi , atoe mawazo ya maendeleo ili sisi tuyafanyie kazi , tulijua kwamba yeye binafsi hana hela za kuleta maendeleo ya kyela bali ameshindwa kabisa kuchochea mzuka wa maendeleo , SASA NATANGAZA RASMI KWAMBA NITAMG'OLEA MBALI 2015 , SITAKI LAWAMA .

Kila la kheri mkuu mwenyezi Mungu akuongoze.
 
Hata mseme nini,Mwakyembe amepaboresha bandarini, anaendelea kuifufua ATC na TRL.
Mtu ukiwa na nia njema basi angalau ungetaja hata treni ya dar kama ni sehemu ya mafanikio yake.
Mimi katika mawaziri ninaowakubali wa kwanza ni Mwakyembe.Anafanya maamuzi sahihi sana katika mazingira magumu.

Hata sisi Kyela TUMEMUAMBIA AKAGOMBEE Ilala aliko wapa usafiri bora au Temeke anapo imarisha bandari yao!Hivi unajua kama Kyela na sisi tuna bandari na hajawahi igusa kwenye bajeti ya wizara yake?

Ni mbunge wa Kyela sio wa Dar kumbuka hii
 
tuliwaambia wananchi wanawachora hawakusikia wakashupaa tu. wote walokula posho za bunge la katiba hawarudi mjengoni mwakani. na waliochangia hoja hadharani wasijisumbue hata kurudi majimboni.
 
Tukiongelea utendaji, mie naona mwakyembe ni moja ya mawaziri wanaofaa sana na tunahitaji mawaziri wote wawe kama yeye. Ila tatizo la nchi yetu ni mfumo ndio maana hata mwakyembe kuna mambo anaogopa kuyafanya, kwahiyo dawa ni kuwang'oa ccm wote na najua tukifanya hivyo nchi itapiga hatua.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom