Risala ya wananchi wa Kyela Kwa Mbunge wao Dr. Harrison G. Mwakyembe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Risala ya wananchi wa Kyela Kwa Mbunge wao Dr. Harrison G. Mwakyembe

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by bakenyile, Apr 4, 2012.

 1. b

  bakenyile Member

  #1
  Apr 4, 2012
  Joined: Mar 30, 2012
  Messages: 20
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  RISALA YA MAPOKEZI YA MH. MBUNGE NA NAIBU WAZIRI WA UJENZI DR. HARRISON GEORGE MWAKYEMBE WILAYANI KYELA TAREHE 30 MWEZI WA 3 MWAKA 2012

  Mhe. Mbunge wetu na Naibu waziri wa Ujenzi, Dr. Harrison George Mwakyembe;
  Mama Linah Mwakyembe; na wasaidizi uliofuatana nao,
  Sisi wananchi wa Kyela bila kujali Tofauti zetu za kisiasa, za vyama, za Kidini na kikabila, tunakukaribisha nyumbani kwako Kyela kwa furaha tele huku tukimtukuza Mwenyezi Mungu kwa muujiza alioutenda wa kukuponya ugonjwa wa ajabu ambao mpaka sasa chanzo chake hakijathibitishwa ila sisi tunajua ni sumu ambayo Mungu kwa ukuu wake kaiyeyusha kutokana na maombi yetu kwake.
  Mhe. Dr. Mwakyembe kipindi chote ulichougua uliugua pamoja nasi wapiga kura wako ambaotumepitia kipindi kigumu sana chakuchanganywa akili na vyomba vya habari vya mafisadi kwa taarifa zao za kupotosha kuhusu hali yako ya afya. Leo tunaambiwa hali yako ni nafuu , kesho wanasema ni mbaya sana, keshokutwa wanasema (bila aibu wala huruma) umepoteza maisha. Tuliamua kuwapuuza na kuoma uponyaji kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Hatimaye Mungu ametenda MWAKYEMBE UMEPONA!!!
  Mhe. Mwakyembe tunapenda kuchukua fursa hii kumpongeza sana mama Linah Mwakyembe kwa ujasiri wake wa kukuhudumia bila kuvunjwa moyo na fisi waliokuwa wanasubiri mkono wa Dk. Mwakyembe udondoke. Tunasema AHSANTE sana. Vilevile tutakuwa ni wanyimi wafadhila tukisahau kumshukuru sana Jemedali wetu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dk. Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na serikali yake kwa kutambua haraka ukubwa na udharura wa tatizo lililokuwa limekupata na kukukimbiza India. Mwisho tunawashukuru madaktari wote Tanzania na India waliokuhangaikia na watu wote ndani na nje ya Kyela walioungana na wananchi wa Kyela katika kukuombea mbunge wetu.
  Mh. Dk. Mwakyembe wengi wetu tulifarijika sana tuliposikia mara ya kwanza ukiwaambia waandishi wa habari kwamba hukuenda India kumtafuta mchawi ila kutafuta tiba na kwamba kama ugonjwa wako ulikuwa wa mkomno wa mtu basi unamwachia Mungu. Hayo mheshimiwa Mbunge na Naibu Waziri wa ujenzi yalikuwa ni maneno mazito na ya busara yanayoendana na maandiko matakatifu kwamba kisasi si cha mwanadamu, ni chake mwenyewe Mungu!
  Lakini msimamo huu usichukuliwe na mafisadi kuwa udhaifu, hivyo kuendeleza vitimbi na njama zao za kumhujumu Mbunge wetu. Watakuwa wanafanya kosa kubwa la kujutia, maana sisi wananchi tutawashukia kwa nguvu zetu zote bila huruma kama Bunge la 9 lilivyoishukia Richmond.
  Tayari chokochoko zimeanza hata kabla vidonda vya Mbunge wetu havijakauka, sasahivi zipo harakati za chini chini za kumleta Edward Lowassa wilayani Kyela kuendesha harambee ya kanisa katoliki. Yote haya yanafanyika huku serikali ikiaangalia tu ili baadaye ije kuingia gharama kubwa ya kuleta FFU, kutibu majeruhi na kukarabati uharibifu wa Mali. Kyela hatuogopi kusema Ukweli na Serikali itusikilize. Ni Lowassa huyo huyo na best wake Rostam ambao kwa muda mrefu sana wameendesha kampeni ya magazeti kumtukana na kumzulia kila aina ya uongo Mbunge wetu; ni hawa wawili walioingiza mamilioni ya pesa kumg’oa Dk. Mwakyembe kwenye Ubunge; ni hawahawa waliotumia jeuri ya pesa kutaka kumg’oa Profesa Mwandosya kwenye u- NEC wa mkoa na Ubunge ; kwanini leo tusiamini kuwa ni hao hao waliosababisha viongozi wetu Mwakyembe na Mwandosya kupelekwa India kwa matibabu? Wasitake kuficha madhambi yao kwa kutoa michango kwenye makanisa yanayothamini pesa kuliko utu, kuliko udhaifu, kuliko usafi wa moyo na hata kuliko neno. HATUMZUII KUJA, ILA APIME MWENYEWE KAMA ALIVYOPIMA KWENYE RICHMOND.
  Mhe. Mbunge wetu, kuugua kwako kumesababisha kuwepo kwa viporo vingi vya matatizo katika jimbo lako; Ujenzi wa kiwango cha lami wa barabara ya Kikusya mpaka Matema, ununuzi wa Kivuko kipya katika ziwa Nyasa na Ulanguzi wa Mbolea na hata kushuka kwa bei ya zao la kokoa n.k. umerudi sasa tunakuomba anza kazi na haya, mengine utajionea mwenyewe.
  Nimalize kwa kukuombea afya njema. Afya yako iendelee kuimarika ziku hadi siku ili uendelee kuiongoza wilaya yetu kwa mafanikio. Kuugua kwako kusikufanye utetereke katika mapambano dhidi ya adui UFISADI, songambele tuko pamoja nawe.
  [FONT=&quot] [/FONT]
   
 2. Gwankaja Gwakilingo

  Gwankaja Gwakilingo JF-Expert Member

  #2
  Apr 4, 2012
  Joined: Jan 26, 2012
  Messages: 1,963
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Mwenye macho aone na asome kisha awahadithie wasio na macho na wasioweza kusoma,mod tunza kumbukumbu
  "usipoweza kupima utapimwa"
   
 3. MANGUNGO

  MANGUNGO JF-Expert Member

  #3
  Apr 4, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 1,538
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 133
  kwenye ofisi ile ndiko walikomwekea sumu na ndio huko amerudi tena.ningekua mimi nisengerudi magamba sio watu.sijui nja
   
 4. Osaka

  Osaka JF-Expert Member

  #4
  Apr 4, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 1,766
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Noted with thanks!
   
 5. Endeleaaa

  Endeleaaa JF-Expert Member

  #5
  Apr 4, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 1,223
  Likes Received: 314
  Trophy Points: 180
  Hiyo vita ya Tembo nyie Nyasi mnaitakia nini? au mna hamu ya kuumizwa?

  Lowassa akija huko hamuwezi kufanya lolote hizo ni kelele tu kama za Debe tupu. maana hakuna hata mmoja wenu wala Mwakyembe mwenyewe anaweza kuthibitisha kuwa amegongwa na Nyoka Lowasa.

  Hakufa this time basi Amshukuru Mungu wake atulie asubirie another strike. Ndani ya CCM kila mtu na Adui wa mwenzie msijidange kuwa adui wa Mwakyembe ni Lowasa na Rostam only.
   
 6. Osaka

  Osaka JF-Expert Member

  #6
  Apr 4, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 1,766
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Unahitaji maombi. Pole!
   
 7. Rogate

  Rogate JF-Expert Member

  #7
  Apr 4, 2012
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 215
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hawa wa Kyela nao!!! Mambo ya Ngoswe wamwachie Ngoswe mwenyewe. Hawajui hata kuwa mitambo ya Richmond imeuzwa na serikali imebariki uuzwaji wake!! Waache uzandeki Richmod nizaid ya wanavyoifahamu.
   
 8. M

  MSAUZI JF-Expert Member

  #8
  Apr 4, 2012
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 228
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Hakuna wana kyela hapo,nyie ni kakundi cha watu wenye njaa zenu.mmekalia kugawa wana kyela bila sababu.Wajinga nyie hamna kitu chochote.Lini mpokelewa anaandaa mapokezi na kujaza bodaboda mafuta.Kudadadek nyie,wapuzi kabisa,wilaya haina kitu nyie maugonvi tu.
   
 9. b

  bakenyile Member

  #9
  Apr 4, 2012
  Joined: Mar 30, 2012
  Messages: 20
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  You may crazy, kama ule umati niliouona mm uliletwa basi hicho kikundi kingekuwa tajiri sn, ninaamini ww ni mmoja wa wale wanaotumika kama condom, ndio maana unashindwa kuangalia vitu kwa uhalisia. Furthermore I m sure you are not from Kyela and if so then I regard you as blind minded. Kyela is not the way you think, they have their own power and they will never be driven by you people with such shallow minds.
   
 10. d

  dada jane JF-Expert Member

  #10
  Apr 4, 2012
  Joined: Dec 8, 2011
  Messages: 566
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hayo ni ya watu wa kyela na mafisadi tuwaachie wenyewe. Ila wanaweza kufanikiwa kama wakijiarumeru.
   
 11. b

  bakenyile Member

  #11
  Apr 4, 2012
  Joined: Mar 30, 2012
  Messages: 20
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Siamini kama hapo hakuna wana Kyela na kama umati ule uliokuwa unashangilia ile risala ni kakikundi basi hii dunia sielewi. Ila nakuonya kitu kimoja, kama wewe unatumika na mafisadi jihadhali sana na endelea kujificha kwenye mtandao huku. Kama wewe ni mkweli ebu penyeza pua yako hapa kwetu Ipinda na useme hayo maneno yako uone kitakacho kutokea.
   
 12. paty

  paty JF-Expert Member

  #12
  Apr 4, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 1,251
  Likes Received: 162
  Trophy Points: 160
  hamna kitu hapo, mwakyembe na kundi lake Vs Lowassa na kundi lake. kundi la mwakyembe lipo weak, linajidai ni kundi la uma, ila nao ni wale wale tu , wanazuga eti wananchi wote bila kujali itikadi za kisiasa, wapi wewe???? kimsingi huyu na mzee Sitta nawaona HATARI KULIKO HUYO LOWASA lowasa tunamjua ni ADUI , that is the point of winning, hawajamaa wanafiki sana, wanajidai wameweka maslai ya uma mbele ila still wana ajenda zao, mwakyembe akife mbali + sitta akafie mbali + lowassa akafie mbali hatuwaitaji woote ni walewale, WANA CONFLICT OF INTEREST , wanapambana kikundi cha akina mwakyembe ni WEAK na kinatumia WANANCHI KAMA SHIELD, WANAJAMVI, hawa jamaa wote tuwapige CHINIIII
   
 13. v

  vangiling'ombe Senior Member

  #13
  Apr 4, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 102
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  hv wana-jf huyu mtu anayeitwa lowasa ni nani katika nchi hii? Yaani kama tutakubali kuburuzwa na masaburi yake basi wazalendo wa ukweli wa nchi tutakuwa tumekufa wote.
  Swali:kwann anatumia nguvu nyingi kiasi hiki kujisafisha na hatimaye urahisi? Kama majirani zake tu (wana arumeru) wamemkata iweje tanzania nzima. Ashindwe na alegee.
   
 14. M

  MSAUZI JF-Expert Member

  #14
  Apr 4, 2012
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 228
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Kumshabikia Mwakyembe inatakiwa akili ya maiti au "IKHIGHUNE"maana yeye ni Gamba la Kinyonga,kila siku anakuja na mbinu za uongo,maendeleo Kyela hakuna,.Toka tumchague Mwakyembe,amefanya nini,zaidi ya lowasa lowasa,Mara Mwakipesile alikuwa ananikwamisha,sasa mwakipesile hayupo hamsemi tena.Mwakyembe ni gamba la kinyonga na bangi za Malawi.
   
 15. v

  vangiling'ombe Senior Member

  #15
  Apr 4, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 102
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ila nawe mwakyembe hueleweki vizuri. Huwezi kuichukia harufu ya choo ingali unang'ang'ania chooni. Jivue gamba na wewe.
   
 16. M

  MAKAH JF-Expert Member

  #16
  Apr 4, 2012
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 1,598
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mukenyile - chezea hangine sio watu wa kyl - ni wa wazi mno - nafikiri watu bado wana kumbukumbu ya mazishi ya Mpangala RIP.
   
 17. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #17
  Apr 4, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Risala imeleta ugomvi Jf kwa faida ya nani?
   
 18. Malafyale

  Malafyale JF-Expert Member

  #18
  Apr 4, 2012
  Joined: Aug 11, 2008
  Messages: 11,206
  Likes Received: 3,620
  Trophy Points: 280
  Mm kwetu ni Lufilyo-Ipinda!Dr Mwakyembe HANA NGUVU kwa sasa Kyela sijui mwipwa Banyekile unayatoa wapi maneno haya ya kutunga!Dr Mwakyembe anajua hata yeye kama 2015 anang'oka na hata mwaka 2010 akiwa KASUMULU alitangaza kuwa HATAGOMBEA tena kabla hajabadili uamuzi wake hivi juzi!

  Dr Mwakyembe sera zake kuhusu Kyela zimeshindwa na wapiga kura wanalijua hilo na yeye analijua hilo!Ana tu-diverge sasa kutumia vita vya ufisadi ambavyo havimletei faida yeyote mwana Kyela!Vita vya ufisadi vinatakiwa viwe collectively responsibilities ya wabunge wote na wala sio tu aachiwe Mbunge wa Kyela!Anapopayuka kuwa Lowasa ni fisadi ndiyo Kyela hospital inajaziwa madawa?Ndiyo bei ya kakao inaimarika?

  Dr Mwakyembe ni msanii tu na Banyakile ni mmoja wao wanaolipwa wajipange STAMICO wamsubiri ionekane kama anaungwa mkono!Kama HAJAJITOA mwaka 2015 ni aibu kwa Dr Mwakyembe!
   
 19. wwww

  wwww JF-Expert Member

  #19
  Apr 4, 2012
  Joined: Mar 20, 2012
  Messages: 350
  Likes Received: 204
  Trophy Points: 60
  Uzuri wa Kyela hawakopeshi, wakisema wamesema. ''UPIME MWENYEWE'' au Muulize Ridhiwani alifanywa nini kwenye harambee ya UVCCM.

  Kimsingi Kyela hawahitaji fedha za MAFISADI (FEDHA ZILIZOJAA DAMU NA JASHO LA WATANZANIA). Wanaohitaji pesa hizo ni KANISA KATOLIKI (Kanisa la kuwaibia walalahoi kupitia mikono iliyojaa damu ya Mafisadi).
   
 20. wwww

  wwww JF-Expert Member

  #20
  Apr 4, 2012
  Joined: Mar 20, 2012
  Messages: 350
  Likes Received: 204
  Trophy Points: 60
  Inawezekana wewe ndiye mpuuzi kuliko wote halafu hujielewi.
   
Loading...