Mwakyembe: Awamu iliyopita aliyetuwezesha kukamata 99% ya madawa ya kulevya aliishia jela

real G

JF-Expert Member
Feb 7, 2013
5,227
5,292
Amesema alipata taarifa za kichunguzi kuhusu jinsi dawa za kulevya zinavyopitishwa katika uwanja wa ndege wa Dar es Salaam, na akaamua kutangaza vita akisaidiana na mtu ambaye hajamuweka wazi, lakini mwisho mtu huyo aliyekuwa akiongoza vita hiyo, aliishia kufungwa gerezani mpaka leo.

Mwakyembe amesema hata baada ya yeye kutumia nguvu zake kumtoa gerezani ameshindwa, jambo ambalo linaonesha kuwa vita dhidi ya dawa za kulevya ni ngumu kuliko kawaida, huku akionesha matumaini kuwa katika awamu hii, serikali itashinda.

Dk. Mwakyembe amezungumza hayo leo jijini Dar es Salaam, alipokutana na wahadhiri na wanafunzi kutoka Shule Kuu ya Sheria ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, kwa lengo la kupokea mapendekezo ya kanuni ya kusimamia sheria mpya ya msaada wa kupata msaada wa kisheria iliyopitishwa na Bunge hivi karibuni.

Chanzo: EATV






Waziri Mwakyembe afichua kilichofanya azidiwe kete na Agnes Masogange katika sakata la dawa za kulevya, amtaja kijana wake ambaye yuko hatarini kuuawa gerezani


Waziri wa Sheria na Katiba Dkt. Harrison Mwakyembe ameendelea kufunguka jinsi alivyokwama kudhibiti upitishwaji wa dawa za kulevya katika Uwanja wa Ndege wa Dar es Salaam wakati alipokuwa Waziri wa Uchukuzi hadi kuzidiwa kete na Agnes Masogange

Waziri Mwakyembe akiwa kwenye kipindi cha East Africa Breakfast amesimulia kilichotokea wakati alipotaka kumdhibiti binti mmoja aliyedaiwa kupitisha masanduku matano ya 'materials' za kutengenezea dawa za kulevya aliyekamatwa nchini Afrika Kusini akitokea Tanzania.

Amesema baada ya kufuatilia sakata lile mbali na kuchukua hatua kwa watu waliomsaidia kupitisha mzigo uwanja wa ndege, aliamua kufanya jitihada za kumkamata binti huyo ili achukuliwe hatua, lakini muda mfupi baada ya binti huyo kurejea nchini, yeye alihamishwa wizara, hivyo kukosa nguvu ya kumshughulikia, hatua iliyofanya binti huyo kumfanyia "nyodo".

Kumbukumbu zinaonesha kuwa binti ambaye alikamatwa nchini Afrika Kusini wakati huo kwa madai hayo, na kisha Waziri Mwakyembe kumfuatilia hadi kutimua baadhi ya watumishi wa uwanja huo Mwezi Agost mwaka 2013 alikuwa ni 'video queen' maarufu nchini, Agnes Gerald 'Masogange'.

Vilevile Mwakyembe amesema kijana wake mmoja anayefahamika kwa jina la Jingu ambaye yuko gerezani, anapaswa kuongezewa ulinzi kwa kuwa yeye ndiye aliyekuwa jemedari wa kudhibiti dawa za kulevya uwanjani hapo, lakini baadaye aliundiwa kesi na sasa huko gerezani anakutana na watu ambao wanaweza kumdhuru kutokana na kwamba yeye ndiye aliyesababisha wafungwe.

======
Mfululizo wa kukamatwa, kesi, hukumu na kuachiwa huru kwa Agnes Masogange kwenye kesi ya Madawa ya kulevya

Masogange ajisalimisha mwenyewe Mahakama a Kisutu

Kupandishwa kizimbani na kusomewa shitaka

Yaliyojili wakati wa kesi ya Masogange

Masogange kupelekwa kwa Mkemia Mkuu

Kesi kusikilizwa

Tetesi za kuachiwa huru

Hukumu

 
huu ndio unafiki tusioutaka, Mwakyembe unalialia nini sasa siumwambie bosi wako tu hizi story??

Hili ni suala la kugonga hodi tu pale Jengo jeupe na kuongea na mkuu tena kizuri zaidi ni bosi wako na unaweza kumuona muda wowote ukitaka, mpelekee hizi taarifa maana yeye ndiye mwenye msaada sasa maajabu ya karne unakuja eti kuwaambia watanzania wa kawaida...
 
Kumkamata Masogange ilikuwa "kosa kubwa sana la kiufundi" kufanywa na Mwakyembe!
Masogange ni kati ya "Punda" maarufu dhidi ya "punda" wengine,maana yeye alikuwa anabeba mzigo wa "Drug Lords" ambao ni VIP.

Ukifuatilia "footnote" za watu waliomsindikiza Masogange hadi uwanja wa ndege,na namna begi zile zilivyopitishwa bila kuwa "scanned" utajua jinsi ambayo Dr Harissson alivyoingia choo cha kike kumkamata "Punda VIP"

Masogange alisindikizwa na Juma Pinto,kwa kadiri ya CCTV za JNIA.Aliondoka na ndege ya South Africa flight [HASHTAG]#SA189[/HASHTAG],ZS-SJF kupitia uwanja wa O.Thambo.

Mara ya mwisho alionekana kwenye mgahawa wa Pinto katikati ya jiji,na dada walioongozana na kukamatwa pamoja alikuwa mtumishi wa mgahawa wa kina Pinto.

Pinto mmiliki wa zamani wa Gazeti la Jambo Leo kabla hajamuuzia Manji.Aliyeingiza vifaa vya Radio ambayo Le Mutuz huwa anasema ni share holder bila kulipa kodi TRA ya Airport.Hajaanza kutajwa jana huyu Pingo,ndio alichukua tender ya kutangaza kupinga ujangiri kwa kubandika mabango kwenye viwanja vya ndege,na kampeni hiyo ilizinduliwa na mkuu wa nne.

Kama ameitwa Masogange,wanaotakiwa hata kuitwa tu na kuhojiwa,hata kama hawatamtia ndani,basi huyu Pinto na Kinje,kutowaita hawa ambao wapo ktk "kiwango bora" ni sawa na kumuacha Mbwana Samatha na Thomas Ulimwengu team ya Taifa na kocha akaamua kumuita Gaudence Mwaikimba ambaye hajaonekana uwanjani karibu msimu wa tatu sasa!

Mwakyembe aseme vizuri tu kina nani walimkwamisha alipokuwa anawataka kina Pinto.Tatizo huyu Dr ni mnafiki tu,aliikana Thesis yake juu ya Muungano na Serikali tatu,alikaa kimya juu ya katazo la mikutano ya siasa,si ajabu hata hili ataishia kukaa kimya
 
Amesema alipata taarifa za kichunguzi kuhusu jinsi dawa za kulevya zinavyopitishwa katika uwanja wa ndege wa Dar es Salaam, na akaamua kutangaza vita akisaidiana na mtu ambaye hajamuweka wazi, lakini mwisho mtu huyo aliyekuwa akiongoza vita hiyo, aliishia kufungwa gerezani mpaka leo.

Mwakyembe amesema hata baada ya yeye kutumia nguvu zake kumtoa gerezani ameshindwa, jambo ambalo linaonesha kuwa vita dhidi ya dawa za kulevya ni ngumu kuliko kawaida, huku akionesha matumaini kuwa katika awamu hii, serikali itashinda.

Dk. Mwakyembe amezungumza hayo leo jijini Dar es Salaam, alipokutana na wahadhiri na wanafunzi kutoka Shule Kuu ya Sheria ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, kwa lengo la kupokea mapendekezo ya kanuni ya kusimamia sheria mpya ya msaada wa kupata msaada wa kisheria iliyopitishwa na Bunge hivi karibuni.

Chanzo: EATV


Its disgusting msomi kuwa na vision ya namna hiyo. It doesn't add up mtu umesoma sheria, halafu kiongozi ktk system unasema vitu vya namna hiyo. Yaani anashindwa kwenda kwa rais am pardon huyo mtu kama ni kweli? I think these doctorate wanazopata something wrong.
 
Back
Top Bottom