Mwakyembe aunguruma | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwakyembe aunguruma

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Dec 21, 2011.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Dec 21, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,612
  Likes Received: 4,603
  Trophy Points: 280
  Ni kuhusu matokeo ya ugonjwa wake
  Ripoti nzito ya madaktari yatua serikalini
  Asema amerudi salama, hatalipiza kisasi  [​IMG]
  Naibu Waziri wa Miundombinu, Harison Mwakyembe, akizungumza na wandishi wa habari kutoka vyombo vya habari vya IPP nyumbani kwake Kunduchi, jijini Dar es Salaam jana, kuhusu afya yake baada ya kurejea nchini kutoka India kwenye matibabu. (picha na Omar Fungo)  Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk. Harisson Mwakyembe, ambaye alirejea nchini wiki iliyopita kutoka kwenye matibabu chini India, amezungumzia kuhusu ugonjwa wake na kusema serikali imeletewa ripoti nzima kuhusiana na kilichokuwa kinamsumbua.


  Dk. Mwakyembe, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kyela, mkoani Mbeya, alisema Madaktari Bingwa wa Hospitali ya Apollo nchini India alikokuwa anatibiwa, wametuma ripoti nzito yenye uzito wa kilo 10 kwa serikali ya Tanzania, kuelezea walichobaini baada ya kumfanyia uchunguzi.


  Dk. Harrison Mwakyembe alikuwa nchini India kuanzia Oktoba 9, mwaka huu akipatiWa matibabu ya ugonjwa wa mparaganyiko wa ngozi.

  Akizungumza na waandishi wa habari kutoka vyombo vya IPP nyumbani kwake, Kunduchi, jijini Dar es Salaam jana, Dk. Mwakyembe, alisema

  kuwa, licha ya ripoti hiyo kutumwa serikalini kwa ajili ya kufanyiwa kazi, pia madaktari walimueleza kila kitu, lakini kwa sasa hawezi kuzungumzia chochote kwa kuwa ni mapema kufanya hivyo.


  MUNGU AMENISAIDIA, NIMERUDI SALAMA  Alipoulizwa na waandishi wa habari kama ugonjwa wake unahusishwa na kunyweshwa sumu, Dk. Mwakyembe, alikataa kuweka bayana badala yake alisema hakwenda India kutafuta mchawi bali kupata matibabu.

  “Mimi sikwenda India kutafuta mchawi bali nilienda kutafuta matibabu na bahati nzuri Mwenyezi Mungu amenisaidia nimerudi salama,” alisema.


  Dk. Mwakyembe ambaye wakati wote wa mazungumzo, alionekana mwenye furaha, amani na kujiamini na wakati wote alimshukuru Mungu kwa kupata nafuu baada ya kupata matibabu.


  SITALIPIZA KISASI  Katika mazungumzo yake na waandishi wa habari wa IPP, aliweka mbele nguvu za Mungu, ambapo alisema kama kuna watu walitaka kumuangamiza anawasamehe na hana sababu ya kulipiza kisasi.

  “Sitalipiza kisasi hiyo sio kazi yangu bali Mungu anajua cha kufanya na watu wenye kulipiza visasi maisha yao sio marefu,” alisema.


  Dk. Mwakyembe huku akiwa amezungukwa na ujumbe wa viongozi wa Wilaya ya Kyela, waliofika nyumbani kwake kumjulia hali ya afya yake, alisema maombi ya Watanzania katika kipindi chote alichokuwa India yamesaidia kumponya.


  KUENDELEA KUPIGA VITA UFISADI  Mwanasiasa huyo anayejulikana kwa kupambana na vitendo vya ufisadi, aliahidi kuendeleza jitihada zake bila uwoga na kwa kasi kubwa na kwamba hatarudi nyuma.

  Alipoulizwa kama ugonjwa wake unahusisha chuki za kisiasa, alisema hilo anamuachia Mwenyezi Mungu na kwamba yeye hana cha kufanya.


  “Huu ugonjwa matibabu yake yalikuwa magumu kidogo, lakini madaktari walionitibu walijitahidi pamoja na maombi ya Watanzania nayo yamesaidia kunifikisha hapa nilipo leo,” alisema.


  NIKO TAYARI KUENDELEA NA KAZI  Kuhusu kurejea kazini, Dk. Mwakyembe, alisema yupo tayari kuendelea na kazi kama kawaida baada ya madaktari waliomtibu kuridhika kwamba anaweza kufanya hivyo.

  MWENYEKITI KYELA: MAFISADI WAMEHUSIKA


  Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyela Mkoani Mbeya, Gabriel Kapiji, akizungumza na waandishi wa habari, alidai mafisadi wamehusika katika ugonjwa unaomkabili mbunge wao.

  Kapiji na ujumbe wake walifika nyumbani kwa Dk. Mwakyembe kwa ajili kumjulia hali, baada ya kurejea nchini kutoka India alikokuwa amelazwa.


  Bila kumung'unya maneno, Kapiji, alisema watu wote wanaopingana na ufisadi ndiyo wanaotaka kuangamizwa na mafisadi na kwamba Dk. Mwakyembe ni mmoja wa watu wanaowindwa.

  “Endelea na kazi yako na sisi tupo nyuma yako kwa kuwa mafisadi hawataki kuona juhudi zenu zinafanikiwa hata siku moja,” alisema.


  KAULIYA KATIBU MKUU WIZARA YA AFYA  NIPASHE ilimtafuta Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Blandina Nyoni, kwa ajili ya kutoa ufafanuzi kama serikali imepata ripoti ya madaktari waliokuwa wanamtibu Dk. Mwakyembe, alijibu kwa kifupi kuwa ni mapema kuisemea na kisha akasema yupo kwenye kikao na kukata simu.  KAULI YA WAZIRI WA AFYA  Naye Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Hadji Mponda, alipoulizwa kuhusiana na taarifa hiyo iliyotumwa serikalini, alisema haijafika ofisini kwake.

  Waziri Mponda, alisema serikali inapokea taarifa nyingi kutoka Hospitali ya Apollo ambazo zinalenga kutoa ushauri, lakini ya Dk. Mwakyembe haijapokelewa na kusema kuwa labda bado ipo njiani.  CHANZO: NIPASHE

  Mwenyeezi Mungu akulinde Dr. Mwakyembe maaduwi zako wawe mbali na wewe uwe muangalifu sana Ameen.


   
 2. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #2
  Dec 21, 2011
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Duh!mwakiembe umenusulika,huna budi kumshukuru mungu!!
   
 3. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #3
  Dec 21, 2011
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,799
  Trophy Points: 280
  wakati fulani wana jf tulinong,onezwa kuwa mwakyembe angejaaliwa kurudi salama angefungu na kuweka kila kitu bayana, mbona anaonyesha dalili za kumdharau mungu kwa kushindwa kutoa ushuhuda mbele ya kusanyiko. anashindwa kusema ameponywa nini!!!!! nina mashaka!
   
 4. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #4
  Dec 21, 2011
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Yetu macho,

  Ingekuwa bora hawa CCM wakamalizana wenyewe kuliko wanavyotuua sote tena by slow killing dose....

  Dhambi waliyoiasisi ya kutafunana wenyewe kwa wenyewe lazima tu itawamaliza.....

  Namhurumia sana Mwakyembe ila pia namlaumu kwa kufanya mambo kizembe...Kama kweli anapiga vita ufisadi, inakuwaje anaendelea kubaki na mafisadi nadani ya magamba yao??

  Sitaki hata kumwamini mtu yeyote ndani ya hilo jidubwasha lao la ulaji kila mtu akikimbilia kuchukua chake mapema!!
   
 5. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #5
  Dec 21, 2011
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160

  Hawezi kusema lolote,

  Tangu lini mtu mwenye akili akaukata mkono unaomlisha??

  Kama dau niko tayari kuweka...I swear, he will never open his mouth...sana sana akiita press conference itaishia kuwa kama ya EL huko Monduli...Unaita watu wazima na kuanza kuwasimulia hadithi za kitoto!!
   
 6. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #6
  Dec 21, 2011
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,799
  Trophy Points: 280
  Kama anamuheshimu mungu ya nini kumtii shetani? eti namuachia mungu!
   
 7. rosemarie

  rosemarie JF-Expert Member

  #7
  Dec 21, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 6,767
  Likes Received: 1,023
  Trophy Points: 280
  kwa nini anaficha mambo na kudai kumwachia mungu kila kitu'siasa za miafrica ni ovyo kabisa'ameniudhi sana'analeta yale mambo yao ya kulindana'aende zake huko na liccm lake
   
 8. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #8
  Dec 21, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,612
  Likes Received: 4,603
  Trophy Points: 280
  Anaogopa wasije wakamuuwa kwa njia ingine ajali ya.........
   
 9. Manyanza

  Manyanza JF-Expert Member

  #9
  Dec 21, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,446
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Hawezi kumheshimu mungu hata siku lakini atamheshimu" Mungu" pekee
   
 10. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #10
  Dec 21, 2011
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160

  Mkuu,

  Huo ni utaratibu wa kawaida wanaotumia watu ambao wana utata kuzungumza na public. Hajafanya confession yoyote kwa hiyo hatuwezi kuamini kama kweli anamwamini Mungu,

  He just said so and there is no had proof of the content and intent!!
   
 11. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #11
  Dec 21, 2011
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160

  Hivi kuna ugumu gani kumwelewa huyu jamaa,

  Kwani mmesahau kauli yake kwamba ripoti ya Richmond iliyofikishwa bungeni ilikuwa nusu???

  He is still doing the same!!
   
 12. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #12
  Dec 21, 2011
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Woga tu na njaa,

  Yeye aligusa watu hawazidi 5 (RA, EL, Karamagi, Msabaha na wenginewachache) halafu anaogopa wasimuue...Kama tungetumia mfano huo, vipi Dr Slaa ambaye ameshataja zaidi ya 15 na bado yuko mzima???
   
 13. bakuza

  bakuza JF-Expert Member

  #13
  Dec 21, 2011
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 488
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Bila kueleza nini shida iliyomsibu kwa kutoa ushuhuda wa uponyaji wake na kumsingizia Mungu ni yale yale magamba yanaendelea.Hakuna jipya.Yeye ni mmoja wa wanaCCM na kila analolifanya ni kwa mjibu wa kautaratibu kao ka kujitafutia umaarufu,mali,n.k.Hata ktk ugonjwa anaingiza siasa.Kushney
   
 14. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #14
  Dec 21, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,612
  Likes Received: 4,603
  Trophy Points: 280
  hawezi kumuheshimu Mungu hata siku lakini atamuheshimu ''Mwenyeezi Mungu''
   
 15. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #15
  Dec 21, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,612
  Likes Received: 4,603
  Trophy Points: 280
  Dr Slaa ni Mzizi Mkavu hauchinbwi Dawa hawamuwezi Mafisadi Dr. Slaa ni chuma cha Pua.
   
 16. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #16
  Dec 21, 2011
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Sasa kama hawezi kujilinganisha na mtu kama Dr Slaa, kwa nini asibwage manyanga na kujisalimisha kwa mafisadi..After all, amepoteza pesa nyingi sana kwa kutokubali kuingia kwenye payroll ya akina RA na EL. Ona sasa anaishia kutishwa na sumu!!

  If you can't fight them, join them....Sijui kwa nini anashindwa kuelewa simple logic kama hiyo...Ama akae kimya au aende kwenye upande wa mashujaa wasiomwogopa mtu....Ningekuwa jirani naye ningepatia list of shame part 1 & 2!!
   
 17. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #17
  Dec 21, 2011
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,306
  Likes Received: 5,596
  Trophy Points: 280
  Sasa Mafisadi wanamlaumu kwa kuficha ukweli wa Richmond au?walitaka kuwe na serikali mpya sasa baada ya ile yote kujiuzulu!!!!aibu,,,,,,funguka Mwakyembe tujue ukweli!!!!!pole sana baba!!
   
 18. K

  Kwitukutila Member

  #18
  Dec 21, 2011
  Joined: Oct 30, 2011
  Messages: 43
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Sijaona ulichokisahihisha, usilazimishe udini hapa ni jukwaa la siasa ndugu.
   
 19. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #19
  Dec 21, 2011
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  At the most he has purred
   
 20. k

  kiyeyeu Member

  #20
  Dec 21, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 38
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mnafiki tu hata alipokuwa anatoa ripoti ya richmond kuna mengi aliyafichana leo riport ya ugonjwa wake kuna mengi kayaficha, hatuna muda wa kusikiliza upupu usio na mbele wala nyuma ni bora angekaa kimya kuliko kutoa mipasho ktk media
   
Loading...