Mwakyembe Arukiwa Na Wasomi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwakyembe Arukiwa Na Wasomi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Sumaku, Dec 21, 2009.

 1. S

  Sumaku Member

  #1
  Dec 21, 2009
  Joined: Feb 17, 2009
  Messages: 53
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  WASOMI WASEMA: Dk. Mwakyembe ni mpotoshaji

  MWANDISHI WETU

  Mbunge wa Jimbo la Kyela kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Dk. Harrison Mwakyembe, ametajwa kuwa ni miongoni mwa watu wapotoshaji nchini huku akijificha kwa kofia ya kubobea katika taaluma ya sheria.

  Hali hiyo imebainishwa na watu mbalimbali hivi karibuni kufuatia kitendo chake cha kusalimu amri na kuhojiwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupamba na Rushwa nchini (TAKUKURU) kutokana na kashfa ya kupokea posho mara mbili kwa kazi moja.

  Dk. Mwakyembe pamoja na baadhi ya wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , akiwemo Mbunge wa Kishapu, mkoani Shinyanga, Fred Mpendazoe ambaye naye awali aligoma kuhojiwa, hatimaye alikubali kuhojiwa na taasisi hiyo nyeti ya serikali.

  Baadhi ya wasomi ambao waliongea na mwandishi wetu kwa masharti ya kutotajwa majina yao gazetini walisema kuwa kusalimu amri kwa Dk. Mwakyembe na mwenzake na hatimaye kuhojiwa na Takukuru kumechukuliwa na baadhi ya watu kuwa ni hatua ya kiume na kukomaa kisiasa kwa wabunge hao ambayo ilikuwa ikitarajiwa na wengi nchini.

  Hata hivyo, baadhi yao wamemtaja msomi huyo wa sheria kuwa ni mpotoshaji kwani ameshindwa kuwa na msimamo katika mambo yake.

  “Awali alisema kuwa hawezi kuhojiwa kwa sakata la kupokea posho mara mbili kwa kazi moja kwa kuwa ana kinga ya kisheria, baadaye aliambiwa kuwa asipokubali angekamatwa na kuhojiwa kwa nguvu… anabadilika na kukubali, hii ina maana gani kama si upotoshaji,” alihoji mwanafunzi wa udaktari Chuo Kikuu cha Tiba cha Muhimbili, jijini Dar es Salaam.

  Alisema kuwa kujua sheria haina maana kuwa hawezi kufanya uhalifu, hivyo inavyoonekana ni kuwa alikuwa akifanya makusudi kuchukua posho mara mbili huku akijua kuwa kufanya hivyo ni kosa kisheria.

  Hata hivyo, daktari huyo mwanafunzi alisema kuwa kila shughuli anayofanya Dk. Mwakyembe anakuwa na lengo fulani, kwani sakata la Kampuni ya kufua umeme wa dharura ya Richmond ambayo yeye alikuwa mwenyekiti wa kamati ya kuchunguza mkataba wake, anaona kama inampa kinga asisemwe.

  Hata hivyo, mwalimu mmoja wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) cha jijini Dar es Salaam alisema kuwa, kukataa kuhojiwa kwa Dk. Mwakyembe kumemuondolea heshima yake mbele ya umma.

  ” Kama kuna rushwa mahakamani na polisi, basi wanaofanya makosa wakatae kukamatwa na polisi na wakatae kuhukumiwa na majaji?” alihoji msomi huyo na kuongeza kuwa huu ni upotoshaji mkubwa.

  Hata hivyo, baadhi ya watu wanashangaa kwanini alikubali kuhojiwa.

  “Ni kweli kuwa Dk. Mwakyembe angeendelea kugoma kuhojiwa, mwisho wa siku angejikuta akivunjiwa heshima yake kwa kuhojiwa kwa nguvu na hatimaye kupelekwa mahakamani kwa kukataa amri halali ya taasisi hiyo iliyopewa meno na Bunge lenyewe,” alisema mmoja wa watu waliohojiwa na mwandishi wetu.

  Akaongeza: “Baada ya hapo ndipo ushujaa wake ungemtokea puani kwani aibu ya kuhojiwa isingelingana na aibu ya kupelekwa mahakamani na kuhukumiwa kwa kukaidi amri ya halali ya serikali, kosa ambalo mwenyewe analitambua kisheria.”

  Hata hivyo, kukubali kuhojiwa kwa Dk. Mwakyembe ambaye aliapa kuwa asingehojiwa kamwe huku akidai kuwa kufanya hivyo ni kuwadhililisha wabunge, kumemwaibisha na heshima yake kuporomoka.

  Heshima yake imeshuka kwa vile anafahamika na mara kwa mara amekuwa akijitangaza kuwa ni mtu wa kanuni, hivyo swali hapa ni vipi alisimamia hoja ambayo asingeweza kuiendeleza.

  Wachunguzi wa mambo ya kisiasa wanasema kwamba, Dk. Mwakyembe ni mwanasheria, tena aliyebobea katika nyanja hiyo, hivyo anategemewa kuwa kila anachokisema anakuwa ameshakitafakari mara kadhaa kwa kuangalia madhara na athari zake mbele ya umma.

  Aidha, wamesema kauli ya mbunge huyo kuwa hawezi kuhojiwa kwa kuwa kufanya hivyo ni kukiuka sheria bila shaka ameitoa kwenye vitabu, kwa maana hiyo inaonekana kuwa vitabu vyake vya sheria alivyovisoma vilimdanganya au alikosea kuvisoma na kumwelekeza kuwa hapaswi kuhojiwa.

  Mbunge huyo wa Kyela, aliwahi kusema kuwa kuwahoji wabunge maana yake ni kukiuka sheria inayohusu kinga, madaraka na haki ya wabunge, bila shaka hoja hiyo ameijenga kupitia mtazamo wa kisheria zaidi.

  Si hivyo tu, Dk. Mwakyembe alidai kuwa taratibu hazikufuatwa kwani aliitwa kutaka kuhojiwa kwa simu badala ya wito maalum wa barua.

  Dk. Mwakyembe hakuishia hapo, alizidi kusema kuwa hatua hiyo ilichukuliwa kwa nia ya kufunika kashfa ya mkataba tata wa Kampuni ya kufua umeme ya Richmond .

  Kimsingi ni kuwa, wito ni wito tu, uitwe kwa kukonywezwa, kuitwa kwa barua, kwa mdomo, kwa simu au kupitia barua pepe, unabaki kuwa wito, kwani kinachotazamwa hapa ni taarifa ya kukutaka ufike sehemu fulani.

  Hata hivyo, hatua ya kutakiwa kuhojiwa na kashfa ya mkataba wa Kampuni ya Richmond , ni mambo mawili tofauti ambayo kimsingi yasingestahili kuwekwa pamoja kama alivyojaribu kufanya Dk. Mwakyembe.

  Hatimaye, sheria imechukua mkondo wake, Dk. Mwakyembe kahojiwa, japo kwa shingo upande, lakini kuhojiwa ni kuhojiwa tu. Ingekuwa ni jambo la aibu kwa serikali kushindwa kumchukulia hatua mvunjifu wa sheria.

  Hata hivyo, kitendo cha Dk. Mwakyembe kugeuka jiwe na kukubali kuhojiwa, kinaweza kuwashangaza wengi waliomuona mbunge huyo ni shujaa kutokana na hoja zake za kupinga asihojiwe huku akisema kuwa hatua hiyo ilikuwa na ajenda ya siri.

  Baada ya kuhojiwa sasa Dk. Mwakyembe ameibuka kwenye gazeti moja la Kiingereza na kutangaza kuwa alikubali kuhojiwa baada ya TAKUKURU kubadilisha taratibu za mahojiano ambayo awali yalikuwa yakienda kinyume na Katiba na Sheria za nchi.

  Wakati Dk. Mwakyembe anasema hivyo, Mpendazoe yeye akasema kuwa hayakuwa mahojiano, bali yalikuwa mazungumzo tu. Ni mazungumzo gani hayo na TAKUKURU?

  Hayo ni mambo ya kushangaza ambayo hayapaswi kujirudia kwa wabunge wetu, kwani wanapaswa kuwa mfano wa tabia na mwenendo mzuri unaozingatia weledi na si kukurupuka na kutoa matamshi mazito na yenye utata ambayo baadaye wanakuja kuyajutia.

  Hili la matamshi mazuri yenye kufurahisha watu linamkumba pia Spika wa Bunge Samwel Sitta, ambaye aliwahi kujitokeza na kuwakingia kifua wabunge kuwa kuwahoji ni kuwadhalilisha, wakati yeye ndiye aliyetaka waheshimiwa hao wahojiwe.

  Hii ina maana kuwa Spika Sitta hakuwa mkweli, aliwahadaa wabunge huku akijua kuwa yeye ndiye aliwasha moto huo bungeni baada ya kutakiwa kufanya hivyo na viongozi wa serikali.

  Tuhuma za wabunge kuwa wanapokea posho mara mbili kwa kazi moja zilifikishwa TAKUKURU na ofisi ya Bunge la Jamhuri ya Tanzania Aprili 26, mwaka huu.

  Kufuatia hali hiyo, Waziri Mkuu Mizengo Pinda alikaririwa akisema kuwa wabunge wanapaswa kuhojiwa kwani agizo hilo linatoka katika Ofisi ya Rais na si kwingineko.

  Hata hivyo, kila jambo halikosi mtibuaji, kwani suala hilo lilikuja kutibuliwa na Spika mwenyewe aliposema kuwa watu wanawaonea wivu wabunge ambapo aliwataka wajiandae kuingia katika ulingo wa siasa na kugombea ubunge mwakani.

  Hata hivyo, Spika Sitta alisema kuwa wabunge wataendelea kupokea fedha hizo mara mbili kwa kuwa ni takrima.

  Wabunge waliokwishahojiwa na kamati hiyo hadi sasa ni pamoja na James Lembeli (Kahama), Chrisant Mzindakaya (Kwela), Fred Mpendazoe (Kishapu), Aloyce Kimaro (Vunjo) na Anthony Diallo (Ilemela).

  Hakuna sababu hata moja ya Watanzania kujichanganya kwani TAKUKURU imekusudia kutekeleza wajibu wake na hakuna aliye juu ya sheria.

  Hata hivyo, sheria na kanuni za malipo ya posho zinasema mtumishi, mtu au asasi haiwezi kulipwa zaidi ya mara moja kwa ajili ya kazi hiyo hiyo.

  Sasa hawa wabunge wanalipwa posho za kujikimu (subsistence allowance) na Ofisi za Bunge, lakini wakienda kwenye taasisi au mashirika ya umma au serikali za mitaa wanalipwa tena posho za kujikimu kwa shughuli hiyo hiyo ambayo Bunge imeshawalipa.

  Inaelezwa kwamba, wabunge wanapotembelea asasi, taasisi na mashirika ya umma anapaswa kupewa chakula, maji ya kunywa, vinywaji baridi au baada ya kikao kufanyiwa hafla.

  Mchambuzi mmoja wa masuala ya kisiasa nchini aliwahi kusema kuwa Watanzania kila tunapotaka kufanya suala la maendeleo, huwa kuna urasimu unatokea, hivyo hadi unapokamilisha taratibu zake kunakuwa hakuna maana tena.

  Dk. Mwakyembe alikataa kuhojiwa na TAKUKURU kama baadhi ya wabuge wengine walivyohojiwa na taasisi hiyo kwa madai kuwa hizo ni mbinu za kutaka kuwaziba midomo wabunge.

  Katika mahojiano yake na vyombo vya habari hivi karibuni Dk. Mwakyembe alikaririwa akisema kuwa, TAKUKURU inawapigia simu wabunge mmoja mmoja na kuwahoji kwa takriban zaidi ya saa tatu.

  Alisema kuwa hilo ni kosa na ni kinyume cha sheria kwani mahojiano hayo hayawekwi kwenye maandishi.


  CHANZO: TAIFA Tanzania, Desemba 18, 2009
  Nimeinasa kwenye mtandao wa kwanzajamii.com
   
 2. D

  DOMINGO BASO Member

  #2
  Dec 21, 2009
  Joined: Dec 21, 2009
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Upuuzi uleule,ni akina nani hao.Hili gazeti lilianza vizurri but I see linaelekea kufa sasa.Linatumiwa.
   
 3. b

  bambumbile Senior Member

  #3
  Dec 21, 2009
  Joined: Aug 30, 2009
  Messages: 109
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tafsiri za sheria za Dr. Mwakyembe zimemponza aliyekuwa mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya Kyela. Alimpa ushauri ambao baadaye umekuja kuonekana ni kinyume na sheria na mzee wa watu kaishia kupoteza cheo.

  Kama kuna mtu anajua vitabu vya sheria alivyotunga Dr. Mwakyembe ninaomba majina yake na wapi vinapatikana?
   
 4. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #4
  Dec 21, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,470
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Bua ha ha ha..aah mie sitii neno..Kuna waandishi wana matuthi ya rejareja.
   
 5. TingTing

  TingTing Member

  #5
  Dec 21, 2009
  Joined: Dec 20, 2009
  Messages: 93
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Sasa ni gazeti ndilo lina makosa ama ni mbunge mwenyewe ndio ana makosa ya kuvunja sheria kwa kupokea posho twice. Duh.....
   
 6. b

  bigilankana Senior Member

  #6
  Dec 21, 2009
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 143
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  tanzania ina mambo. mbunge anakataa kuhojiwa na chombo cha dola. Anatamba hahojiwi. Chombo kinasema kitamhoji atake asitake. kasalimu amri. utakuta watu wanamtetea hapa. Huyu anatoa mfano mbaya sana kwa wananchi
   
 7. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #7
  Dec 21, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,470
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Mwenye makosa aliyechukua posho mara mbili. Hili halina mjadala.
   
 8. M

  Mafuchila JF-Expert Member

  #8
  Dec 21, 2009
  Joined: Apr 29, 2006
  Messages: 752
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Interesting!!!
   
 9. Nyuki

  Nyuki JF-Expert Member

  #9
  Dec 21, 2009
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 371
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hata mimi nilimshangaa,PCCB imekuwepo kuptia sheria iliyotungwa na bunge,na wakakipa meno chombo hiko cha dola akiwepo yeye mwenyewe DR.Harrison isitoshe yeye ni mwanasheria aliyebobea katika fani hiyo.

  Anatoa picha mbaya sana kwa jamii nzima ingali yeye ni mwakilishi wa jamii.it is very unproffessional to act like that.thats why politics is a dirty game
   
 10. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #10
  Dec 21, 2009
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,033
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Gazeti lenyewe ni la nazir karamagi!!!!!!!!! Give me a break, msomi analyst wake ni mwanafunzi, what nonsense is this!!!!!!!!!!

  I wonder wapi prince bagenda alipoharibikia, nilimuadmire sana enzi zake. Lakini sasa tangu aajiriwa na karamagi anaysis zake ni za hovyo bora hata za aliyefeli darasa la nne.
   
 11. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #11
  Dec 21, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 135
  Mwakyembe mwizi
  Waandishi wazushi
  Twafwa!
   
 12. K

  Kicheruka JF-Expert Member

  #12
  Dec 21, 2009
  Joined: Feb 2, 2009
  Messages: 792
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  no sense
   
 13. B

  Boramaisha JF-Expert Member

  #13
  Dec 21, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 820
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Habari hii imedhamiriwa kumdhalilisha Mwakyembe kwa makusudi kabisa. Kwanza inategemea ni katika mazingira gani yaliyosababisha Mwakyembe atamke kwamba hayuko tayari kuhojiwa na PCCB. Pili, hivi ni Mwakyembe peke yake ambaye amekuwa akipokea posho mbili na si Wabunge wote? Why pick on him alone katika suala hilo la posho mbili.

  Magazeti yanayopenda kuandama watu badala ya hoja yanatia aibu taaluma ya uandishi. Gone are the days when we had waandishi kama akina Reginald Muhango, Adam Lusekelo na wengine wengi waandishi waliokuwa wakijua na kuitumikia kwa uadilifu taaluma yao ambapo mtu ulikuwa ukipenda kununua gazeti na kupenda kulisoma toka ukurasa wa kwanza hadi wa mwisho kwa sababu zilikuwa zinachambuliwa hoja na si kuchamba watu!
   
 14. b

  bambumbile Senior Member

  #14
  Dec 21, 2009
  Joined: Aug 30, 2009
  Messages: 109
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Lakini yeye mwenyewe si ndiye aliitisha mkutano na waandishi wa habari na kuwaambia amekataa kuhojiwa? Alipohojiwa, angeitisha mkutano pia na kuwaambia kakubali kuhojiwa.

  Wabunge wengine hawakusema lolote kuhusu kujua sheria na kukataa kuhojiwa ndio maana hata sasa waandishi hawana cha kuandika juu yao.

  Magazeti yanakukuza na siku wakiona unaanza kuwa dhaifu, yanasaidia kukumaliza. Waandishi sasa wanamtumia Mwakyembe kuuza magazeti yao.
   
 15. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #15
  Dec 21, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,275
  Likes Received: 352
  Trophy Points: 180
  Unajua JF tuepuke kupayuka mambo jamani nakumbuka yeye alisema wao kuhojiwa kwa kipindi kile ilikuwa kama undue influence kisheria bse walikuwa wanataka kudiscuss richmond iyo iyo amabayo Hosea amekomaa kustep down.
  Basically walitaka kuwaziba midomo wabunge.
  Alafu taratibu hazikufuatwa bse ata speaker alikuwa hana taarifa kama bosi wao.
  Je wewe PCB wakija kwa ofisi yako watakuja kukuhoji bila bosi wako kujua.
  Last year mimi walikuja nkawaambia warudi then waandike barua ya kuomba appointment kwanza na kuandika wanataka taarifa zipi na walitii
   
 16. M

  Magezi JF-Expert Member

  #16
  Dec 21, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,813
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 145
  mijadala mingine haina mashiko
   
 17. M

  Magezi JF-Expert Member

  #17
  Dec 21, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,813
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 145
  Yeye alikataa kwa sababu taratibu hazikufuatwa, lakini baadaye kama mnakumbuka Hosea ilibidi aende bungeni kuwa na mazungumzona spika na hapo aliwasilisha barua ya kuitaarifu ofisi ya spika juu ya suala hilo na baada ya hapo spika alitoa waraka kwa wabunge walio takiwa kuhojiwa.

  Kwa mujibu wa kanuni za bunge mbunge hawezi kupingana na waraka uliotolewa na spika, kwa mh. mwakyembe ilibidi ahojiwe ktk mazingira hayo na si vinginevyo.
   
 18. KILITIME

  KILITIME JF-Expert Member

  #18
  Dec 21, 2009
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 267
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Unakumbuka kwamba Dkt Mwakyembe alisema kwamba yeye pamoja na wabunge wengine kuhojiwa ni kukiuka Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge? Sasa hizo haki, kinga na Madaraka ya Bunge vimeenda wapi mpaka anakubali ahojiwe? Kwa nini usikubali tu kwamba Dkt Mwakyembe aligundua kwamba alichemka kwa kukataa kuhojiwa na ndio maana hajaitisha tena mkutano na waandishi wa habari ili kuwaambia kwamba alishakubali kuhojiwa! Halafu Spika 6 kudai kuwa hakuwa na taarifa za kuhojiwa kwa Wabunge si kweli, alitaka asionekane mbaya kwa "wapiganaji" wenzake ndio maana hajasema lolote baada ya wao kuhojiwa!
   
 19. KILITIME

  KILITIME JF-Expert Member

  #19
  Dec 21, 2009
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 267
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Kanuni ya ngapi?
   
 20. b

  bambumbile Senior Member

  #20
  Dec 21, 2009
  Joined: Aug 30, 2009
  Messages: 109
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mazungumzo ya Mwakyembe mbona yako humu humu JF? Naona sasa mmeanza kupotosha ukweli. Alichosema Mwakyembe na mnachosema sasa ni tofauti kabisa.

  Kuhusu Hosea kwenda bungeni, wote wawili, yaani Sitta na Hosea walikataa kwamba Hosea hakwenda pale bungeni kwa ajili ya suala la posho mbili. Kama nakumbuka vizuri Hosea aliitwa na PM na akasema aliona isingekuwa heshima kuondoka bila kumsalimia spika.

  Vipi ile kanuni ya 100 na 101 aliyosema inamlinda? Pia alisema atakutana na TAKUKURU mahakamani na huko atawabwaga? Mbona kakunja mkia kuwafuata ofisini kwao tena kimya kimya?
   
Loading...