Mwakyembe anawashukuru nyote

Tunamshukuru Mungu kwamba amepata nafuu na kurudi nyumbani. Tunamwombea aendelee kupona na kuungana nasi katika mapambano ya kulikomboa taifa letu toka mikononi mwa mafisadi, ambao ni chama chake - ccm!
 
Ambacho sikubaliani na wengi kuhusu Dr. Mwakyembe ni kuhusu ugonjwa wake. Kwanini watu hawakiri maradhi waliyo nayo na wanatafuta sympathy ya wananchi kwa kusema mara kalogwa, mara kategeshewa ajali, mara kawekewa sumu na mafisadi....kwa lipi? Karne ya 21 bado watu wanaamini kwenye tunguli! Watu na maradhi yao lkn wanaficha nyuma ya pazia la mkono wa mtu! Type ya viongozi kama akina Mwakyembe, Sitta, Membe, Nape ambao ni Ma-opportunists siwafagilii sana. Wana udhaifu mkubwa nyuma ya pazia! Ila Kama binadamu nimefurahi afya yake imeimarika na namuombea maisha marefu ili asahihishe pale alipojikwaa!
 
Maelezo yako hayajitoshelezi!fafanua
Nadhani unakumbuka wakati mwakyembe anasoma ripot ya richmond; mwishoni alisema kuna baadhi ya mambo wameyafunika ili kuilinda serikali. Hatukujua wakati huo lakini baadae tuliona swala la richmond limemalizwa kihuni na waziri mkuu mbele ya sita na sita akafunga mjadala bila kuruhusu hoja za wabunge bado hatukuelewa. Mwisho tumesikia juzi Lowasa anamwambia kikwete ukweli lakini lowasa huyuhuyu ndio alikuwa ameficha ukweli huo kwa nia ya kumlinda rafiki yake, na mambo aliyosema lowassa ndiyo waliyoficha akina mwakyembe na sita.
 
jamani ngoja niwakumbusheni zamani wakati anafundishwa alijitoa kwenye board ya nbc baada ya kuzikataa milioni hamsini ambazo board member wote walipewa ili wapitishe mambo ya makaburu mwenzie wote wasiokuwa wazalendo walizichukua na wakati huu ndio alikuwa akianza msingi wa ghorofa lake mliloliona kwenye tv (itv) ndio ujue watu walivyo wazalendo mtu anashida ya hela ila hawezi uza utu wake huyo ndiyo dr mwakyembe! mwita 25 unamzungumzia uwaziri wa juzi tu hapa!!

na alipokuwa usalama wa taifa wakati mwandishi wa habari kamuulize kwa nini alitoka (mwita research first before you speak)

hilo ndio jembe na limerudi, na tunalitaka chadema kama ccm hamtomchagua kuwa mgombea wenu!!

Kumbe ni mtu wa usalama wa Taifa; hiyo kazi nasikia huwa hawatoki ni ya maisha!!
 
mwakyembe anawashukuru wote mlio muombea. kapata nafuu kubwa na anasema ataendelea na kasi ileile. kwamba matatizo yake yamesababishwa na mafisadi.source itv. Mia

mwambie tulimwombea sana. Ila mwabie pia asiwe na kasi kama ya mkubwa wake ambaye kasifiwa mbio hadi kapitiliza kwao
 
Hamna kitu hapo; Mwakyembe, Lowassa na Sita ndio waliolea sana ufisadi. Wanatakiwa hata kuchomwa moto. Hawa ndio walioficha ufisadi eti wanakipigania ccm, ujinga gani huu wanawezaje kuwa na uchungu na chama badala ya taifa?
Kaka Kibona
ingekuwa better kuanza kuwachoma moto mafisadi ndio wafuate waliolea. Unajua hata unapotakakumwadhibu mtoto mkaidi unaanza na adhabu ndogo au karipio na sio adhabu kubwa kama ya kumnyonga. Ndivyo walivyofanya uliowataja hapo juu. Walichokifanya walitoa onyo hivyo tusiwahukumu kuwa wanafiki. Wakulaumiwa ni mafisadi ambao hawakutaka kusikia na kuanza kulipiza visasi kwa kutaka kuwadhurumu pumzi yao(wapambanaji) wakati hata gharama yake hawaijui. Mungu aishie milele mwenye hukumu ya haki atawahukumu tu. I believe it. After low muda ulikuwa bado kwa huko nyuma kidogo wananchi hatukuwa aware kihivyo. Lkn kwa sasa hao mafisadi wafanye la kufanya we know each and every thing.
 
Huyu mwakyembe hatumuelewi! Kama anatambua maombi yatu, inampasa atueleze alikua anaumwa nini au sumu gani alipewa, kuendelea kukaa kimya au ku ficha ni u snitch. Bora wamuongezee doz ya kutosha, akafie mbali!
 
Watakucheka watu MD24. Shauri yako.
 
Kinachotakiwa Mwakyembe aeleze ni akina nani walimwekea sumu au wanaotaka kuua kuliko kuficha matokeo yake akifa ndio yatoke oh fulani ndie aliemuua. Sema ukweli hili hao wanaokutafuta wajulikane na utakuwa huru. Usiogope kunyanganywa unaibu waziri ww bado ni mbunge tena wa kuchaguliwa na wananchi ina maana wananchi wako nyuma yako hata wakikuvua uanachama unaouwezo wa kuingia katika chama na wananchi wako wakakupa ubunge. Ivyo waeleze wana kyela nini hasa kimekutokea achana na kulinda ambavyo avilindiki kama ni dowans, richmond tayari wananchi wameshawajua ivyo hakuna jipya.
 
Ambacho sikubaliani na wengi kuhusu Dr. Mwakyembe ni kuhusu ugonjwa wake. Kwanini watu hawakiri maradhi waliyo nayo na wanatafuta sympathy ya wananchi kwa kusema mara kalogwa, mara kategeshewa ajali, mara kawekewa sumu na mafisadi....kwa lipi? Karne ya 21 bado watu wanaamini kwenye tunguli! Watu na maradhi yao lkn wanaficha nyuma ya pazia la mkono wa mtu! Type ya viongozi kama akina Mwakyembe, Sitta, Membe, Nape ambao ni Ma-opportunists siwafagilii sana. Wana udhaifu mkubwa nyuma ya pazia! Ila Kama binadamu nimefurahi afya yake imeimarika na namuombea maisha marefu ili asahihishe pale alipojikwaa!

Siri ya ugonjwa wake anaijua yeye,familia yake na madaktari wanaomtibu. Tetesi nyingine nadhani ni mambo ya kutafuta ushawishi na umaarufu wa kisiasa!
 
Nadhani unakumbuka wakati mwakyembe anasoma ripot ya richmond; mwishoni alisema kuna baadhi ya mambo wameyafunika ili kuilinda serikali. Hatukujua wakati huo lakini baadae tuliona swala la richmond limemalizwa kihuni na waziri mkuu mbele ya sita na sita akafunga mjadala bila kuruhusu hoja za wabunge bado hatukuelewa. Mwisho tumesikia juzi Lowasa anamwambia kikwete ukweli lakini lowasa huyuhuyu ndio alikuwa ameficha ukweli huo kwa nia ya kumlinda rafiki yake, na mambo aliyosema lowassa ndiyo waliyoficha akina mwakyembe na sita.

Mkuu nimekupata...hii siasa ya Tz,kazi kweli kweli
 
ameiweka serekali mtegoni kwamba 'ripoti ya ugonjwa wake imekabidhiwa serikali", sasa tusubiri kama serikali hii ya jk wataitoa kwa wananchi...
 
Kwa jinsi alivyoeleza japo hakumtuhumu mtu yeyote lakini pia alionyesha ujasiri wa kutoogopa mtu yeyote katika kuwatumikia watanzania. Na mwenyekiti wa halmashauri ya kyela alipasua jipu kwa kuhusisha ugonjwa wa mwakyembe na mafisadi ambao wanatka kupunguza kasi yake katika kuwakabili. Sasa najiuliza kuwa kama kuna tuhuma hizo uslama wa taifa wanafanya nini? mimi nilitegemea kuwa usalama wa taifa watachukua maelezo hayo kama kianzio cha kusaka genge hilo hatari kwa taifa letu. Ni jambo lisilokubalika popote kunapokuwa na tuhuma nzito kama hizo halafu hatuoni kinachofanyika tunataka kuona uchunguzi wa kina unafanyika na kama kweli kuna watu wanahusika kutishia maisha ya watu wengine wachukuliwe hatua mara moja.
 
Jamani hodi humu ndani..,
Mimi kuna kitu kinanishangaza sana,kama nakumbuka vizuri Dr.Mwakyembe aliwahi kuripoti kuwa kuna njama za

kumuua,sasa kama aliweza kutambua hilo na akavitaarifu vyombo husika(serikali) na bado majaribio ya kumuua

yakaendelea inamaana serikali ya TZ teyari imegeuka kuwa ya kimafya na hata raisi mwenyewe kutokemea au kuhoji

hadharani inakuwaje mambo kama hayo yanatokea basi inawezekana hata yeye ni muhusika .
 
jamaa ana bonge la jumba la ghorofa!nilidhania wanamapinduzi sio matajiri.
 
jamaa ana bonge la jumba la ghorofa!nilidhania wanamapinduzi sio matajiri.

Kumbe na yeye ana Libugando, Mwanza enzi hizo ghorofa ilipokuwa ni Bugando Hospital tu. Fisadi anatakiwa kuwa na mali kuanzia kiasi gani wajameni?. Maana naona watu huwa hawaangalii mtu kazipataje mali alizonazo. Kama aliweza kujenga ghorofa zamani hizo, nafikiri atakuwa na mabugando kibao, kwa hiyo nayeye ni wale wale tu. Azimio la Arusha lingerudi kutaifisha maghorofa yote ya watu ambao wapo kwenye uongozi nafikiri vita kubwa sana ingeaza, maana wenzetu wanamiliki mpaka AK47. Mimi kumiliki shortgun napata wakati mgumu kweli kujieleza.
 
Back
Top Bottom