Jaji Mfawidhi
JF-Expert Member
- Feb 20, 2016
- 15,514
- 23,256
Hapo Picha inajieleza, maneno mengi sitaki
wakati serikali inayo ongozwa na ma-profesa na ma phd holders ikiprove failure, na huku vituko vikizidi kila uchao, Harisson Mwakyembe ambaye wakati mmoja aliwahi kumshauri JIWE kwamba waifanye TLS (Chama Cha Wanasheria Wa Tanganyika) iwe SACCOS na viongozi wake wateuliwe na Mwakyembe, hii ilibuma.
Sasa huyu bwana sijui ni ile sumu aliyonyweshwa kipindi ama la lakini kaibuka na Roma Mkatoliki.
"Kama msanii unang'ang'ana kuimba siasa na kukosoa serikali basi amua kuachana na muziki uanzishe chama cha siasa. Lakini kama unataka kupata maslahi kwenye muziki, basi nyimbo hizo hazilipi. Haiingii akilini nina shahada nne halafu msanii ambaye hajaenda hata shule anatunga nyimbo za kunikosoa. Wewe na darasa la nne lako sijui la 7 utanionya mimi mwenye degree nne na nimefundisha vyuo vikuu mbalimbali?" - Dr.Harisson Mwakyembe (PhD), Waziri wa Habari, Sanaa na Michezo.
Na Malisa GJ - Albert Einstein aliwahi kuulizwa akili ni nini? What is intellect? Akasema akili ni kile kinachobakia baada ya kuondoa yote uliyofundishwa darasani.
Yani kwa mujibu wa Einstein kuna watu wakiondoa yale waliyofundishwa shuleni, vichwa vyao vinabaki vitupu. Vinakuwa wazi kama mzinga wa nyuki.
Kitu pekee walichojaza kichwani ni yale waliyofundishwa darasani. Hawa ndio hujisifia vyeti, au idadi ya "digrii" walizonazo. Hawana akili, japo wana elimu.
Einstein alisema hakuna uhusiano kati ya elimu na akili. Kuna watu wana elimu lakini hawana akili, na wengine wana akili lakini hawana elimu. Ni bora uwe na akili ukose elimu, kuliko uwe na elimu ukose akili.
Manguli wa Sayansi duniani kama kina Isaac Newton, Galileo Galilei na Archimedes of Syracuse hawakuwa na elimu yoyote ya cheti diploma wala degree, lakini walikua na akili. Ugunduzi wao mpaka leo unaiongoza dunia. Akili.
Akili siku zote ni "superior" kuliko elimu kwa sababu akili ndio ilibuni elimu. Yani watu wenye akili walikaa wakakubaliana waanzishe utaratibu ambao utamuwezesha mtu kukaa darasani na kujifunza kwa kipindi fulani, kisha mtu huyo apimwe kwa mitihani na kisha atunukiwe cheti. Ubunifu huo ulifanywa na akili. Jiulize mtu wa kwanza kutunukiwa degree duniani alifundishwa na nani?
Kwahiyo mtu mwenye akili lakini akakosa elimu, anaweza kuwa msaada mkubwa kwa jamii kuliko mtu mwenye elimu lakini akakosa akili. Mark Zuckerberg hakumaliza shule lakini kwa kutumia akili amebuni mifumo rahisi ya mawasiliano kupitia mtandao.
Yeye ndiye mmiliki wa Facebook, Whatsapp na Instagram. Wale maprofesa waliomuona "kilaza" darasani leo wanatumia ubunifu wake kuendesha maisha yao. Kama sio Facebook basi wanatumia Instagram au Whatsapp. Maprofesa wenye elimu kubwa wamezidiwa ujanja na "kilaza" mwenye Akili.
Kumbuka Einstein alisema akili ni kile kinachobakia baada ya kuondoa yote uliyofundishwa darasani. Jiulize wewe ukiondoa yale uliyofundishwa darasani unabaki na nini? Yani ukiondoa hiyo diploma, degree, PhD au 'digrii 4' unazojivunia, kichwa chako kinabaki na nini?
Kama kuna kitu kinabakia basi hicho kinachobakia kinaitwa "AKILI". Na kama hamna kinachobakia basi hilo bichwa halina tofauti na mtungi wa gesi. Nothing more, nothing less!
kama aliomba ama hakuomba namba kwa huyu dada mimi sijui
#Akili #Elimu #NinaDegree4