Mwakilishi wa Jimbo la Jang'ombe, Abdallah Diwani avuliwa uanachama wa CCM. Fancy Nkuhi,Mariam Ussi wapewa karipio kali

Papaa Mobimba

JF-Expert Member
Jan 27, 2018
754
3,097
Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (NEC),amemvua uanachama wa CCM kwa kosa la kukiuka maadili ya chama cha Mapinduzi Mwakilishi wa Jimbo la Jang’ombe visiwani Zanzibar, Abdallah Maulid Diwani

Pamoja na mambo mengine, Mwakilishi wa Jimbo la Jang’ombe, Abdallah Maulid Diwani amefukuzwa uanachama kwa kwenda kinyume na maadili na miiko ya viongozi wa CCM.

“Kikao pia kimetoa karipio kwa Wajumbe wa Bunge la Afrika Mashariki, Fancy Nkuhi na Mariam Ussi Yahya kwa mwenendo usioridhisha, usiolinda maslahi ya nchi na unaokinzana na misingi na miiko ya uongozi na wamewekwa chini ya uangalizi wa kimaadili kwa miezi 18,” imesema taarifa hiyo ya Polepole.

Sababu ya kuvuliwa yasemekana

'Abdalla Diwani aliwaambia CCM ndani ya ukumbi wa baraza la wawakilishi kama wapo hapo kwa hisani ya Jecha lakini hawakushinda uchaguzi.
Alisema kwenye baraza la wawakilishi kwamba CCM ilifanyiwa favour na Jecha mwenyekiti wa tume ya uchaguzi lakini ukweli CCM haikushinda.
Walimbana pale pale aombe radhi, akawauliza kwani Jecha hakufuta uchaguzi?

DeYXLaBWAAApp-F.jpg
 
Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (NEC),amemvua uanachama wa CCM kwa kosa la kukiuka maadili ya chama cha Mapinduzi Mwakilishi wa Jimbo la Jang’ombe visiwani Zanzibar, Abdallah Maulid Diwani

Pamoja na mambo mengine, Mwakilishi wa Jimbo la Jang’ombe, Abdallah Maulid Diwani amefukuzwa uanachama kwa kwenda kinyume na maadili na miiko ya viongozi wa CCM.

“Kikao pia kimetoa karipio kwa Wajumbe wa Bunge la Afrika Mashariki, Fancy Nkuhi na Mariam Ussi Yahya kwa mwenendo usioridhisha, usiolinda maslahi ya nchi na unaokinzana na misingi na miiko ya uongozi na wamewekwa chini ya uangalizi wa kimaadili kwa miezi 18,” imesema taarifa hiyo ya Polepole.

Huyu atakuwa Mpemba tu!
 
Pamoja na kuwa sababu hazijawekwa wazi lakini watu tayari wana sababu zao......

Kweli wabongo wape picha tu habari watajazia wenyewe....
 
Back
Top Bottom