Zee la shamba
Member
- Oct 17, 2007
- 55
- 3
Kweli kifo cha mende, yaani sasa mpaka Mwakawago naye, je na yeye anaweza akajibu yanayomuhusu kule ubalzoi wetu NY?
Anyways, mkuu alimaliza muda wake ubalozini kwetu NY, akapewa kazi na Kofi Annan, kuwa msaidizi wake Sierra Leone, ambako hakuelewana kabisa na baadhi ya seniors wa UN, huko hivyo alihamishiwa kwa muda visiwani Cape-Verde, mpaka alipomaliza mkataba wake na UN, alirudi nyumbani, ambako mpaka leo hajapewa chochote, ingawa amekuwa akijaribu sana lakini Mkapa, alikataa kabisa kuonana naye toka alipotoka ubalizini kwetu, Muungwana, ndio kabisaaa maana huyo mzee aliwahi kuwa bosi wa Muungwana zamani Dodoma CCM, alikuwa akimchukia sana Muungwana mpaka akamuhamishia Tunduru, kwa hiyo uwezekano wa hata Bodi hakuna,
Sasa najua yuko benchi, ila haya yamenishitua kutoka kwake, maana ya kwake ni aibu hata kusema, lakini ndio hivyo tena kifo cha mende!
Mzee mwenzangu, ukweli wa hoja haujalishi nani anautoa. Hata akitokea jambazi aliyeko kifungoni akisema "walioiba na wenyewe washitakie" hatuwezi kumuambia "wewe jambazi na uko kifungoni kwa hiyo hoja yako haina maana". Hoja iangaliwe kwa uzito wake wenyewe bila kujali nani anaitoa. Hadi hivi sasa hatujasikia hoja za ufisadi kuhusu Mwakawago, Butiku, Warioba n.k isipokuwa kwa wale wachache waliobahatika "kuzifahamu". Hilo hata hivyo haliondoi ukweli kuwa Mwakawago anayo hoja au hana hoja.
Unafikiri kuwataka waliohusika wajibu hoja amekosea bila kuangalia kama yeye amewahi kutuhumiwa hoja na akakataa kujibu; na kama kuna hoja dhidi yake itolewe na yeye aambiwe ajibu. Lakini kujibu hoja kwa kukataa kujibu hoja kwa sababu aliyetoa hoja ana makosa fulani ni mbinu ambayo chama chetu kimejaribu sana na ninafikiri watu wameanza kutuelewa vizuri..
Mkuu so far ninaheshimu sana wito kama huu ulipotolewa na Mwinyi, na Malecela, na ndipo hasa Mtandao waliposhituka, maana by then walikuwa wameowaomba wote wawili wawasaidie kwenye hilo lakini wote wakagoma,
lakini Butiku na huyu Mwakawago, I am not sure, kwa sababu wote wawili hawana rekodi nzuri kuhusiana na rushwa, na ninajua kuwa wamekuwa wakijaribu kila njia kupewa kazi ya ulaji na Mtandao lakini wameshindwa, ndio maana nina wasi wasi na kauli zao kama ni genuine!
Nafikiri na wewe unafahamu kuwa viongozi wetu wa juu sio wajinga kiasi hicho!
Exactly what I am saying mkuuu!ila inanishangaza kuona ni kwa nini imemchukua muda mrefu kusema hadharani kama kweli yeye anauzalendo na nchi hii.
Mkuu Bubu,
Viongozi wenye uchungu na nchi husema pale pale tu kabla moto haujapungua, huwa hawasubiri mpaka moto umesiha ndio wanajitokeza,
Huyu angekuwa mzalendo kweli basi angekemea Zitto, kusimamishwa bungeni kwanza, kabla hajaopngelea mafisadi, tunashukur kuwa amesema something, lakini no thank you too!