Zee la shamba
Member
- Oct 17, 2007
- 55
- 4
MWASISI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na aliyekuwa Katibu Mtendaji wa pili wa chama hicho, Balozi Daudi Mwakawago amewashauri viongozi wa serikali wanaotuhumiwa kwa ufisadi wajiondoe katika nafasi wanazoshikilia kwa sasa ili kupisha uchunguzi huru kuhusu madai hayo.
Akizungumza na Mwananchi katika mahojiano maalum nyumbani kwake jijini Dar es Salaam, Balozi Mwakawago alisema wale wote ambao wanatuhumiwa kwa ufisadi kwanza wanapaswa kujibu tuhuma zinazowakabili na baada ya hapo wajiondoe katika nyadhifa zao ili uchunguzi huru ufanyike.
"Yule anayetuhumiwa jamii ingetegemea aseme kitu, ukinyamaza na kudhani tuhuma hizi zitaishia hewani, unajidanganya, zitaendelea kuwako, kwa maoni yangu naona tuhuma za kisiasa bora zingejibiwa kisiasa," alisema Balozi Mwakawago.
Alisema ili kuimarisha utawala bora nchini, ni wakati muafaka sasa wale ambao wametuhumiwa kwenda kwa Rais ambaye amewateua na kumueleza haja yao ya kujiondoa katika nafasi wanazoshikilia.
"Tujenge utamaduni wa uwajibikaji, wanatakiwa waende kwa aliyewateua, wamweleze kwamba wametuhumiwa na wameamua kukaa kando ili uchunguzi huru ufanyike. Wananchi wanawaangalia, wananchi sasa wanajua haki zao kuliko huko nyuma, viongozi lazima wafahamu hilo, pia wanafahamu dhana ya uwajibikaji kuliko hapo zamani," alisema.
Alisema kwa wale ambao wana dhana kwamba Mahakama itawasafisha wanajidanganya kwani katika siasa hakuna ushahidi wa Mahakama, na hata wakisafishwa na vyombo vya sheria bado wananchi wataendelea kuamini tuhuma hizo ni za kweli kwa kuwa bado wamekalia nyadhifa ambazo wametuhumiwa wakiziongoza.
"Ni kweli Mahakama inaweza kukusafisha, lakini pia ni vema kuwa makini maana ukienda Mahakamani, unaweza kuvuliwa nguo zaidi, tuhuma nyingi zaidi zinaweza kuibuka. Mahakama si mchezo itaenda kila eneo na mambo mengi yanaweza kuibuliwa," alisema.
Balozi Mwakawago ambaye ameshika nyadhifa za Katibu Mwenezi wa TANU, Katibu Mtendaji wa CCM, Waziri wa Habari katika Serikali ya Awamu ya Kwanza, na Waziri wa Viwanda na Biashara katika serikali ya Awamu ya Pili, alisema katika siasa tuhuma hujitokeza pale ambapo wadau wanagundua kuwa kiongozi fulani ametoka katika mstari.
Akizungumzia kusainiwa kwa mkataba wa mgodi wa dhahabu huko Uingereza, Balozi Mwakawago alisema haoni tatizo kwa mkataba kusainiwa nje ya nchi, ila tatizo ni kule kusainiwa katika hali ya usiri pasipo wananchi kupewa taarifa.
"Tatizo ambalo limejitokeza ni ile hali ya mkataba kusainiwa katika hali ya usiri, hakuna sababu ya mkataba kusainiwa kwa usiri na viongozi.
Viongozi wanasaini mikataba kwa niaba ya wananchi, hivyo wananchi wana haki kabisa ya kupata habari za mikataba ya maliasili zao," alisema.
Pia Balozi Mwakawago ambaye alikuwa Balozi wa Kudumu wa Tanzania Umoja wa Mataifa miaka ya 90, alisema baada ya Rais Kikwete kuwaambia Watanzania kwamba kulikuwa na haja ya kuangalia upya mikataba ya madini kwani ilikuwa haiwanufaishi Watanzania wakati akihutubia Bunge, wananchi wengi waliingiwa na furaha kwa hiyo hatua ya kusaini mkataba mwingine katika kipindi kifupi kuliibua maswali mengi.
"Rais Kikwete aligusa hisia za watu, hivyo walishangaa pale walipoambiwa kwamba kuna mkataba mwingine ambao umesainiwa katika kipindi kifupi, ilibidi wajiulize kulikoni? alisema Balozi Mwakawago.
Tuhuma za ufisadi zilitolewa na Mbunge wa Karatu, Dk Willibrod Slaa dhidi ya viongozi wa serikali na chama. Tokea tuhuma hizo zitolewe, baadhi ya waliotuhumiwa wamekana kuhusika nazo, na wengine wametishia kwenda Mahakamani.
source Mwananchi news paper