Mwakalebela aigaragaza Takukuru mahakamani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwakalebela aigaragaza Takukuru mahakamani

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mallaba, Feb 26, 2011.

 1. Mallaba

  Mallaba JF-Expert Member

  #1
  Feb 26, 2011
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 2,560
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  KESI ya pili ya kupokea rushwa kwenye mchakato wa kura ya maoni ndani ya CCM iliyokuwa ikimkabili Frederick Mwakalebela (41), imeondolewa mahakamani na mshtakiwa kuachiwa huru.

  Kuondolewa kwa kesi hiyo kunafuatia pingamizi la awali lililowekwa na wakili wa Mwakalebela, Basil Mkwata.

  Mwakalebela alikuwa mshindi wa kwanza kura za maoni za CCM nafasi ya ubunge wa Iringa Mjini mwaka jana, lakini jina lake liliondolewa na nafasi yake kupewa Monica Mbega, ambaye alishindwa na mpinzani wake, Mchungaji Peter Msigwa wa Chadema.

  Upande wa utetezi ukiongozwa na Wakili Mkwata, uliwasilisha pingimizi la awali la kisheria ukiomba kesi hiyo iondolewe mahakamani kutokana na upungufu wa kisheria uliofanywa na upande wa mashtaka, Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa nchini (Takukuru).

  Upungufu huo ni mtuhumiwa kushtakiwa kwa kutumia sheria mbili tofauti kwenye hati moja ya mashtaka, jambo ambalo ni kinyume cha sheria.
  Akiondoa shauri hilo mahakamani, Hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Iringa, Festo Lwila, aliyekuwa anasikiliza shauri hilo alisema mahakama imeridhia pingamizi hilo.

  Hakimu Lwila alisema mshtakiwa alishtakiwa kwa kutumia sheria mbili tofauti kwenye hati moja ya mashtaka, suala ambalo ni kinyume cha sheria na kinaweza kumsababisha ashindwe kuandaa utetezi wake ipasavyo.

  Pia, Lwila alisema hapakuwa na sababu ya kuweka sheria mbili tofauti kwenye hati moja na kwamba, usahihi wa hati ya mashtaka unapaswa kuwa makini tangu awali inapoandaliwa, tofauti na hivyo ndio umemfanya Mwakalebela kuwa huru.

  “Kutokana na sababu hii, mshtakiwa anakuwa huru na upande wa mashtaka mna hiari ya kuleta tena kesi hii ikiwa haina 'duplicate',” alisema.

  Katika pingamizi hilo, Mkwata alisema tayari mshtakiwa ameshaadhibiwa baada ya Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) kumwengua kwenye uchaguzi, hivyo kuomba shtaka hilo liondolewe mahakamani.

  Awali, akisoma shtaka hilo Mwendesha Mashtaka wa Takukuru, Imani Mizizi, alidai kuwa Juni 20, mwaka jana, Mwakalebela alidaiwa kutoa hongo ya Sh100,000 kwa Hamis Luhanga ambaye ni Mwenyekiti wa Kijiji cha Mkoga, ili awagawie wajumbe 30 wa CCM walioitwa kwenye kikao.

  Mizizi alidai kuwa, Mwakalebela anadaiwa kutoa rushwa kinyume cha sheria ya kupambana na rushwa namba 11 ya mwaka 2007 kifungu cha 15(1)(b) kinachokwenda sambamba na sheria ya gharama za uchaguzi namba 6 ya mwaka 2010, kifungu cha 21 (1) (a) na kifungu cha 24(8).

  Pia, Mahakama ya Mkoa wa Iringa Jumatatu ijayo inatarajia kutoa uamuzi iwapo kesi ya kwanza inayomkabili Mwakalebela (41) na mkewe Selina, iendelee kusikilizwa au iondolewe.
   
 2. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #2
  Feb 26, 2011
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 6,174
  Likes Received: 2,175
  Trophy Points: 280
  Napenda kusikiliza hadithi za kibongo, kwa mfano unamuita mtu siyo raia wa Tanzania hivyo hastahili kugombea ubunge(Bashe) na kweli anazuiwa kugombea mwisho wa siku hakuna hatua zinazo chukuliwa kwa mtu kuishi nchini kinyemela na kuthubutu kugombea uongozi na hadithi inaishia hapo. Siku nyingine utasikia mtu ametoa rushwa katika mchakato wa uchaguzi hivyo anafanywa hana sifa za kugombea na hagombei, mwisho wa siku inagundulika ulikuwa ni mchezo wa kisiasa na hakuna hatua zinazochukuliwa kwa aliyeanzisha uongo huo na hadithi inaishia hapo. Utasikia watu wamejipatia mapesa kibao ya serikali kupitia njia za udanganyifu na ukweli unathibitika alafu unamsikia Rais wa nchi anawaagiza wezi wakipata hizo pesa wazirudishe haraka iwezekanavyo na hadithi inaishia hapo. Hizi hadithi mungu akinipa uhai ninaamini nikiwaadithia wajukuu zangu watacheka sana na kuniuliza hizo hadithi zinatufundisha nini?
   
 3. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #3
  Feb 26, 2011
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,909
  Likes Received: 12,066
  Trophy Points: 280
  Tanzania ina mahakama? hiyo ni michezo ya kuigiza tu. Mimi si hakimu wala mwanasheria lakini naweza ku-predict matokeo hata kabla ya kesi kusikilizwa. Niulize kesi yeyote unayoijua ya kisiasa nikusomee matokeo, kesi ya Mramba,EPA, Dowans, Rada ya Chenge kama hadi leo hujui matokeo yake unamatatizo.
   
 4. Maishamapya

  Maishamapya JF-Expert Member

  #4
  Feb 26, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,280
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
   
 5. Pukudu

  Pukudu JF-Expert Member

  #5
  Feb 26, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 2,970
  Likes Received: 735
  Trophy Points: 280
  takukuru a.k.a 'tume ya kupamba na kusafisha rushwa' is a big joke haifanyi kazi yake bali inalinda na kutekeleza majukumu ya baadhi ya watu tena ndani ya CCM, though inaendeshwa kwa kodi zetu mifano ni mingi tu inayoenyesha udhaifu wao kama wkt wa uchaguzi wa jumuiya za ccm kuna wagombea mkoa wa ars walishikwa na takukuru wakazuiwa kugombea then wakashinda kesi mahakamani. Sidhani kama taasisi hii haina wataalamu bali wamezibwa macho na midomo kwa posho na marurupu makubwa wanatumika kama madog we need to change
   
Loading...