Beatrice Kamugisha
JF-Expert Member
- May 18, 2019
- 762
- 6,980
Taifa la Mungu elimu si Mali ya serikali Bali ni Mali yetu. Wanaosoma si watoto wa serikali bali Ni watoto na ndugu zetu. Wanaoshindwa kusoma kwa kukosa madarasa na madawati si watoto wa serikali bali ni wanetu. Serikali imepewa dhamana yakutuonyesha njia na vipaombele. Sisi tunadhamana ya kusaidia serikali ifikie malengo yaliyowekwa. Kwa mwaka 2021 tukubaliane kama Taifa kwenda na kauli mbiu "TOKOMEZA UHABA WA MADARASA NA MADAWATI TANZANIA."
Waziri wa elimu tusaidie kuyafanya haya;
1. Tuambie kwa Sasa tunahitaji madarasa mangapi ya shule za chekechea/ msingi na sekondari kwa nchi nzima ukituainishia mahitaji kwa kila shule na kata,tarafa,wilaya na mkoa kwa kila shule. List iwe in pdf ili kila mwananchi aipate kwa njia ya WhatsApp lengo nikuwaeleza wananchi huko walipotoka Kuna tatizo na wanapaswa kuwa sehemu ya kulitatua. Wapo watu hawajui kijiji chao kina tatizo gani. (Wekeni na gharama ya darasa moja shs ngapi kwa kila eneo)
2. Kwa mtiririko hapo juu tuambieni kila shule ina hitaji madawati kiasi gani na ikiwezekana price per dawati kwa kila eneo.
3. Kulingana na mchanganuo hapo juu, tuambieni serikali imejikita kufanya nn kwa mwaka 2021 ( calendar year not financial year) ili tujue sehemu iliyobaki.
4. Tuelekezeni utaratibu mzuri wa kuchangia huduma hii, ningependekeza fedha ziingizwe kwenye akaunti ya shule kulingana na mchangaji anataka kutatua tatizo la shule gani.
5. Kwa wale wanaotaka kutoa madawati yaliyokamilika waandaliwe daftari maalum ofisi na daftari hizo ziwe kwa mkuu wa shule. Hivyo hivyo kwa matofali na zitolewe risiti zakuthibisha mali hizo kupokelewa.
6. Kila Tarehe 01 ya mwezi mpya serikali itupe updates za michango kwa kila eneo.
7. Vyombo vya habari viombwe kuitangaza kampeni hii angalau kila siku bila gharama yoyote.
8. Kwa wale ambao watataka kuchangia bila kueleza wangependa msaada uende shule gani basi msaada wao utakapopokelewa eneo la kipaombele liwe ni eneo la kijijini ambapo uwezo wa kuchanga ni mdogo.
9. Projection ya Government iwe ya kutatua tatizo for ten to twenty years siyo tunafunga kampeni desemba 2021 tunaanza Tena kusikia uhaba wa madawati.
Huu ni mchango wangu wa mawazo kwa mwaka ujao, unaweza ukachukuliwa kitaifa au ukachukuliwa kiwilaya au shule mojamoja inaweza kuutumia kutatua tatizo la madarasa na madawati.
Siku zote lazima tatizo lifahamike ndipo litatuliwe. Tufahamu vijiji vyetu vinatatizo gani?
Nikiripoti kutoka Kanyigo ni Beatrice Kamugisha- mwalimu mstaafu.