Mwaka 2020 ulikuwa ni msiba mkubwa wa demokrasia

Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
37,619
46,258
Tafakari kama leo kungekuwa na wabunge wa upinzani angalau 40 wa kuchaguliwa katika bunge kutoka Tanzania bara wakishindana kwa hoja.

Tafakari maswali ambayo angekuwa anaulizwa Waziri mkuu kuhusu masuala mbalimbali na KUB bungeni kwa sasa

Tafakari bajeti za mawaziri vivuli ambazo zinakosekana bungeni kwa sasa ambazo zingeleta mawazo mbadala kwa serikali.

Kwa yeyote aliyefikiria au anayefikri ni sawa kukosekana kwa kambi ya upinzani bungeni alilikosea sana na analikosea sana taifa hili na vizazi vyake vingi mbeleni. Historia itamhukumu na kumsema vibaya siku zote.

Hakuna Tanzania bora itakayopatikana bila ushindani wa vyama vya siasa bungeni

Kujenga nchi huchukua muda mrefu sana ila kubomoa inahitaji muda mfupi sana.
 
Sasa inategemea ushindani upi? Hata madume ya panzi yakigombea jike ni upinzani pia.

Tanzania bado hatujawa na upinzani. Ni upinzani maslahi ambao ukiuendekeza kama kiongozi hutoboi. Hakuna rais aliyebezwa na upinzani kama JK. Alionekana kituko si tu kwa wananchi bali hadi kwa watoto wake.

Leo hii mama alivyoingia walianza kasi ya katiba mpya, wameitwa ikulu.

Kila kitu kimezima labda wakanyagiwe waya tena ndio utawasikia wakipinzani na serikali.
 
Back
Top Bottom