BUSARA ZANGU
JF-Expert Member
- May 5, 2013
- 778
- 1,269
Habari ya muda huu
Wakati tumebaki na siku 33 kabla ya kufunga mwaka nina imani kila mmoja wetu anatafakari mwaka kesho afanye jambo gani ili aweze kupiga hatua hususani za kiuchumi katika Maisha yake. Mimi ni mmoja kati yenu.
Pamoja na mipango tuliyonayo, ni ukweli usiopingika kwamba kwa kuwa tunaishi kwenye nchi yenye serikali (kinyume na anarchism) basi serikali ina mkono wake katika ku shape mipango yetu. LAKINI HAPA NITAKIRI, SERIKALI YA SASA INA MKONO MKUBWA UNAOFIKA KILA KONA YA MAISHA YETU. Rejea maamuzi ya Mwakyembe na Jafo kuhusu ndoa. Pia Rejea uamuzi wa Makonda kisha JPM kuhusu Fiesta. Tena rejea maamuzi ya JPM kuhusu wale vijana waliokuwa wanalima kwenye vyanzo vya maji kule Mwanza. Niishie hapo kutoa mifano kwani leo nimelenga kuliongelea hili swala katika angle ya uchumi.
Serikali isiyotabirika siku zote imekuwa si rafiki kwa muwekezaji ama mtu yoyote anayetaka kufanya jambo la Kimaendeleo. Tazama kwenye mambo yafuatayo:-
Mfano mimi nina kibanda Dar ambacho hakijamalizika. Nilipanga mwakani Mungu akijalia nikimalizie ama nikisogeze kwenye kukikamilisha. Lakini nitaendeleaje na ujenzi kama sijui bomoa bomoa baada ya kumaliza kimara, kisha zile nyumba 1200 itahamia kwenye mtaa gani?
Kuna rafiki yangu anataka anunue hisa katika bank flani ili walau awe na investment huko. Lakini anawaza kesho chochote kinaweza kuibuliwa na serikali. Sote tunajua hasara waliyopata mabenki baada ya mambo ya vyeti feki, watumishi waliotumbuliwa lakini wakiwa na mkopo bank waliacha hasara kubwa huko. Vipi kesho serikali ikiamua kufunga benki kwasababu yoyote ile, kuna jambo kuhusu mifuko ya jamii linatokota kwa vyovyote vile kuna athari itakayoumiza watu.
Wamiliki wa nyumba juzi wameambiwa wanatungiwa sheria ili wawe wanapokea kodi ya mwezi mmoja mmoja badala ya miezi 3,6 ama mwaka. Nyumba nimejenga mimi, serikali inajua sementi, nondo, misumari sikununua kwa rejareja (kwa serikali kupangia wauzaji wa vifaa vya ujenzi) Lakin inataka kodi nichukue kwa rejareja. Kwa wanaotaka kufanya biashara kwenye eneo la real Estates wataendelea na mipango yao? Vipi serikali ikianza kupanga na bei za kodi? Watu wanahofu ya kufanya maendeleo.
Naogopa kununua Ardhi, naogopa kuanzisha biashara ya mazao, naogopa kuanzisha duka la nguo (maana unaweza kushangaa kesho mitumba imezuiwa), naogopa kulima mbaazi maana sijui kesho ya zao hilo.
Sio mfanyabiashara au mkulima tu hata mtumishi anaogopa sababu hajui kesho yake. Hajui lini utaanza uhakiki labda watumishi wasio na vyeti vilivyo na picha hawatahitajika tena, ya nini aende chuo kujiendeleza? Naogopa kuanzisha shamba la miti, je mwakani serikali ikitaifisha misitu ya asili na isiyo ya asili kwa fidia watakayopanga wao?
Mashaka, Mashaka, Mashaka. Ogopa sana utawala wa Maagizo.