Mwaka 2017 Edward Lowassa Kapotea Kabisa, 2018 Atafufuka Au Ndiyo Mwisho Wake Kwenye Medani Ya Siasa?

JINOME

JF-Expert Member
May 29, 2017
958
1,424
images-20.jpg

Alhamisi njema Wadau,
Tofauti na ilivyozoeleka kwa Waziri Mkuu aliyejiuzulu kwa kashfa ya Rushwa na Mbunge wa zamani wa Monduli, Edward Ngoyayi Lowassa kuonekana kwenye kwenye matukio mbalimbali (Makanisani, Misikitini na hata, misiba, birthday, harusi, majukwaa ya kisiasa n.k) , mwaka 2017 umekuwa ni mgumu sana kwa mwanasiasa huyu Nguli. Mzee amekuwa baridi sana. Tatizo nini? Umuhimu wake katika maeneo haya haupo? Au muda wa kuhitajika haujafika? Au thamani yake maeneo haya imekwisha?
Nakumbuka miaka ya kuanzia 2012 hadi uchaguzi wa 2015 mzee alikuwa ni kimbilio:

MICHUZI BLOG: Mh. Lowassa atoa msaada wa sh. mil. 5 kwa Baraza la Misikiti Tanzania
Matukio: EDWARD LOWASA ATOA MSAADA MWINGINE, SOMA HAPA
Viwanjani (nini kimejiri leo Maximo?): Lowassa Atoa Mil. 10 ujenzi wa kanisa Mbeya.

Mwaka 2015 mtu mmoja mmoja , kikundi cha watu ama taasisi zilimtembelea Mhe,Lowassa nyumbani kwake kumtaka agombee urais kwa madai ya yeye kuwa chaguo lao. Mzee aliwaandalia chakula, vinywaji na kila aina ya burudani. 2017 Mzee amepoa sana, ametembelea wamasai wenzake tena wa kutoka Kenya.

Daily Mitikasi Blog: LOWASSA: MASHEKHE WA BAGAMOYO MMENISHAWISHI KUGOMBEA URAIS 2015
WANANCHI KUTOKA MARA WAWASILI KWA WAZIRI MKUU MSTAAFU NA MBUNGE WA MONDULI EDWARD LOWASSA MONDULI,WAMKOSA WAELEZEA... | Magazeti ya leo| Tanzania News |Tanzania Today

Nini tafsiri ya Lowassa kuhamishia siasa zake nchi jirani ya Kenya? Ni kujaribu bahati yake tena ya kutafuta ushawishi wa kisiasa nje ya nchi? Inasaidia nini katika kufanya siasa za Tanzania? Au ndo ule msemo wa kufa kwa Nyani?

Lowassa: Ninamuunga Mkono Kenyatta na nipo tayari kutoa msaada wakati wowote
Lowassa ahudhuria sherehe ya kuapishwa kwa Kenyatta
MICHUZI BLOG: Wakongwe wa siasa nchini Kenya wamtembelea Mh. Lowassa Monduli

Licha ya Wapinzani wenzake kupinga Kupigwa Marufuku kwa mikutano ya hadhara ya kisiasa, yeye alipongeza hatua hiyo na kusema kuwa mikutano ya ndani ni mitamu sana na inawaimarisha wapinzani, je kwanini Lowassa amepotea mwaka 2017 badala ya kuimarika kama alivyodai? Tatizo nini?
Lowassa Apongeza Mikutano ya Hadhara ya Kisiasa Kuzuiwa.....Asema Mikutano Yandani imekuwa Mitamu Zaidi na Imewaimarisha | MPEKUZI

Je mwaka 2018 Mzee atafufuka kisiasa au ndo atazidi kupotoea na ahadi yake ya kwenda kuchunga Ng'ombe Monduli itatimia?

Nini maoni yako kama mdau na shabiki mkubwa wa Mzee Lowassa? Unampa ushauri gani?
 
Wanaosema nihame CCM, watahama wao-Edward Lowassa. Hakuna kitu kilimuuma huyu mzee kama kulazimishwa kuondoka CCM.
 
View attachment 661514

Tuko busy tunatafakari maneno ya busara ya Kakobe.

Hatutoki kwenye reli.
 
Huyo ndo basi tena, malipo ni hapahapa duniani, figisu zake kwa wenzie zimemrudia mwenyewe
 
Back
Top Bottom