Mwaka 2015 ulivyokuwa kwangu

BILGERT

JF-Expert Member
Feb 27, 2015
6,534
11,001
Habarin wana MMU,natumai mnaendelea vyema na shamrashamra za kuukaribisha mwaka mpya 2016..


Wadau,binafsi namshukuru mwenyez Mungu kwa mema mengi,alonijalia kwa mwaka huu unaoisha leo usiku sa sita....kuna mengi mema na pia kama mjuavyo changamoto hazikosekani.nataka kushare nanyi jinsi nilivyo upokea mwaka huu 2015 na jinsi unavoisha huu mwaka 2015 hasa yale makuu ambayo yaweza kuwa mabaya ama mema yaliweza kunitokea,lkn cha muhimu nahitaji kila mmoja wetu atushirikishe yake, kwa namna hii ambayo ntawashirikisha.


Ndugu zangu,binafsi niliweza kumaliza masomo yangu ya kozi ya Medical Laboratory Sciences,ktk chuo fulani mkoani IRINGA mwaka 2014 mwez wa saba...nilikuwa nyumbani mpaka ule mwaka 2014 ukaisha,maana sikujihusisha na masuala ya Tempo works.Hivo mwaka 2015 niliupokea kama ilivo ada,mwez wa pili nlipata post yangu ya kazi nkipangwa huku halmashauri ya mpwapwa dodoma.Hivo kwa upande wangu,nlimshukuru sana Mungu kwa kuanza mwaka vyema pamoja na baraka alonijalia ya kupata kazi.Hapo katikati kuna changamoto kadhaa ambazo nimezipitia,lakin nliweza kuzitatua na hatimaye kusonga mbele.

Ndugu zangu,Naumaliza mwaka huu wa 2015 nikiwa na majeraha makubwa sana moyoni,ambapo mwenzang niliye kuwa nampenda na kumthamin kama mpenz wang,kanifanyia unyama mkubwa sana ambao sito kuja niusahau katika maisha yangu.ni mwanamke ambaye nilikuwa namthamin,namuheshimu na kumfanyia lolote lile,yaan mambo nilo mfanyia ni zaid ya yale ambayo nilikuwa nawafanyia wazazi wangu na ndugu zangu.Kanifanya niuone mwaka 2015 mbaya kwangu,ingawa ulianza vyema.Jinsi alivonitendea,nmehisi kuna jini limemuingia maana sitaki kuamin kama yeye ndo kanifanyia...nawashukuru sana ndungu zangu wa MMU kwa kunitia moyo,hakika naendelea vyema na ninaamin nitaanza vyema huu mwaka mpya wa 2016 na kuendelea vyema na kazi zangu za kulijenga taifa letu. maana lile tukio lilitokea tar 20/12/2015 siku ya jumapili sa mbili na nusu asubuh.nlikuja kuwashirikisha.rejea hiz mada https://www.google.com/url?sa=t&rct...6Xwk5hdWLCMoM3fyA&sig2=wrpQmnG1cJZlP7ZjFlDg1Q


Ambapo nilileta mada inayosomeka....NIPO NJIA PANDA na pia nkaleta MREJESHO wake.



karibuni sana,natanguliza shukrani zangu za dhati kwenu nyote.
 
Back
Top Bottom