Mwajiri wangu hapeleki Michango yangu NSSF, nifanyeje?

Ndibalema

JF-Expert Member
Apr 26, 2008
10,956
4,649
Jamani naombeni msaada wa mawazo.

Nimefanya kazi kwa muda mrefu na mwajiri wangu huyu wa sasa.
Hivi karibuni nikapata wazo la kwenda nssf kuangalia michango ambayo kwa mujibu wa salary slip ninazopewa na mwajiri wangu kila mwisho wa mwezi huonyesha kiasi flani kimekatwa kwenda NSSF.
Jibu nililopewa na NSSF, bado kidogo nizimie.

Nimemwuliza boss wangu hanipi jibu la kueleweka inaonyesha ni dhairi kuwa anafahamu huu mchezo wa hii kampuni.

nifanyeje ili nipate haki zangu?
Nikiendelea kuwa king'ang'anizi si nitakosa hata kibarua chenyewe?
 
Back
Top Bottom