Mwai Kibaki Road Hiyooooo

Mwai Kibaki Road Hiyooooo

Haya ni matusi kwa mashujaa kama SAMORA, KWAME, na MANDELA.
 
Wajameni naomba mnisaidie maana sielewi hapo. Hivi Barabara ya Bagamoyo kubadilishwa jina na kuitwa Jina hilo la Rais wa nch jirani kunaleta maaana gani? Huyo Rais wa Jirani katufanyia nini kikubwa hadi tumpe jina kwenye barabara zetu? Vigezo gani vinahusika kutoa majina ya Barabara zetu? nielimisheni wandugu.
Huu ujinga cjui tutaacha lini? Tunafuta history zetu kumfurahisha jirani?!
 
hatujifunzi sisi watz na ndio maana hako kaheshima kidogo kalikokuwepo nako kanapotea, na hata Mzee Kibaki mwenyewe alisema mbele ya JK kuwa "hatutembei" lakini hata huyo anayetembe inaonekana hana analojifunza labda.
maeneo mengi duniani njia/barabara/highways za kutoka nje ya miji huwa wanajitahidi kuziita maendeo ya huko zinakoelekea. Na hapa tulikuwa hivyo wakati nchi bado ina maono lakini sasa tunaacha hata mambo ya msingi, ni ajabu kabisa!
Mbona Nairobi imejengwa hiyo Thika super highway wameiacha na jina lake hilo hilo la zamani? Au hakuna watu wanaostahili hizo 'heshima'??? (Pia angalia, Mombasa Rd, Nakuru Rd)
 
hata ukiangali kwa hao waliotufundisha huu ustaarabu wa kuita majina barabara zao sehemu nyingi zinabakia na majina ya ziendako. Mfano Brooklyn Bridge, Williamsburg bridge (NY), na miji kama London ni madaraja machache yenye majina ya watu na hao ni mashujaa wa kweli kama Lambert Bridge, Aklbert Bridge.
tufuatilie zaidi labda tunaweza kujua ni vipi Mzee Mwai Kibaki amepewa ushujuu huu.
tunavyoambiwa Deni la taifa lafikia Sh.22 Trilion usije kukuta kuwa Kenya ndio wametoa pesa za ujenzi wa hiyo barabara au wameweka mortgage ya mkopo. Hakuna lisilowezekana nchi hii
 
Tanzania ilikotoka, siko inakoenda.
Hili swali sidhani kama lina majibu.
JK kulipwa fadhila ya Phd yake.
Mhhhhhhh...!!!
 
10996_10151327365208581_543735236_n.jpg

JK una mapungufu!!!!!, sasa hilo nalo la kushangilia. Kweli, Chaguo la Mungu!
 
Hari mpya ,kasi mpya ,nguvu mpya ,me ndo rais mtanifanya nini ccm oyeeeeeeeeee,mbulula mbulula kiazi.
 
Nikiangalia uchochoro wa nyerere road hapa nairobi napata hasira sana! Tz tumekuwa wanyongevsana kwa w K!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom