Kumekuwapo na tabia inayokera sana katika barabara ya Mwai Kibaki zamani Old Bagamoyo. Watumiaji wa barabara wanaotoka Kawe kwa sababu wanazozijua wao wanahisi wao ndio wana haraka zaidi na may be ndio wenye umuhimu zaidi kuliko wale tunaoelekea Kawe. Pasipo aibu wamekuwa wakitumia lane ya wale wanaoenda Kawe na kusababisha usumbufu na pengine ajali ambazo zingeweza kuzuilika. Kadri siku zinavyoenda ndivyo tabia hii imekuwa ikiota mizizi, infact kuna maeneo mengi tu mida hii ya asubuhi ni kama vile lane ya kwenda Kawe inakuwa imekufa kwani lanes zote zinakuwa zinatumiwa na wanaoenda mjini. Kama nilivyosema nimeshuhudia ajali kadhaa ambazo zingine zimesababisha vifo kutokana na upuuzi huu.
Nimeamua kuliweka hili kwani nimeona hakuna juhudi zozote zinazochukuliwa kukomesha tabia hii mbaya ya ubinafsi isiyokuwa na tija yeyote kwani yeyote mwenye akili timamu atakubaliana na mimi kwamba mwisho wa siku hasara ya jambo hili ni kubwa kuliko faida ambayo pia si halisi. I know hiki ni kilio cha watumiaji wa barabara nyingi jijini so Kamanda Kenyela ambaye najua ni member humu na wenzako wa mikoa ya kipolisi ya Dar tafadhali tunaomba mchukue hatua haraka inavyowezekena.