Mwafrika (mweusi) asiyejua Kiingereza!

Barbarosa

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
22,584
27,786
Mwafrika mweusi asiyejua Kiingereza anadharauliwa sana na Mwafrika Mweusi TU lkn siyo na Mzungu, Mchina, Mwarabu, Muhindi n.k hivi ni kwanini?

Ninachomaanisha kwa mfano kama haujui Kiingereza ukamwambia Mmarekani haujui Kiingereza haitakuwa ishu siyo ishu, lkn ukimwambia Mwafrika (mweusi) haujui Kiingereza atakudharau kama kiatu na si ajabu hata kama ulitaka huduma ofisini kwake ukawa ndiyo mwisho wako, sasa kwa nini?


Kwa mfano leo hii Waziri Mkuu au Waziri (Mwafrika Mweusi) yoyote yule aseme hawezi kuongea Kiingereza vizuri hapa JF ita crash kwa jinsi watu (sisi Waafrika weusi) watakavyokuwa wanamshambulia na wengine kumtaka ajiuzulu na hii itasambaa Afrika Nyeusi (Mzungu wa AK wala haitakuwa ishu) yote na kuwa ndiyo hoja ya mwaka, lkn hali kama hii haiwezi kutokea sehemu nyingine yoyote ile Duniani isipokuwa Afrika nyeusi kwetu hata Afrika Kaskazini haiwezekani hata tu Somalia haitakuwa ishu, sasa ni kwa nini tuko tofauti na Dunia nzima?

Je hili linahalisha sisi kubaguliwa na karibu kila kiumbe wa Dunia hii, mpaka hata Mungu?
 
Unachekwa kwa kutojua kiingereza na waafrika/wtz wenzako, ila hatumcheki mzungu kwa kutojua kiswahili.Wakati wenye kiingereza chao hawatucheki kwa kutokukijua, ndipo utakapojua ngozi nyeusi kuna kitu kibaya imekifanya kwa mungu maana kama ni laana hii sasa imezidi.
 
Mimi nadhani ndivyo tulivyo. hatupendi vyetu, tunavidharau na hatuviheshimu. tunaona vya wengine kuwa ndio bora na vya maana zaidi kuliko vyetu. Pia kupenda kujifanya vile tusivyo ndio kunatufanya tuwe hivi. NAHISI SISI WATANZANIA TUNAONGOZA KWA KUWA LIMBUKENI DUNIA NZIMA (JAPO SI WOTE)
 
Sababu kubwa ni moja, hiyo ndio lugha ambayo imetumika kama nyenzo ya kukufundishia, tunajiuliza imekuwaje umemaliza chuo kikuu na haujui kiingeleza? Kiingeleza kwetu na kwa nchi nyingi za Afrika kimepewa kipaumbele na kinatumika kama official language, hivyo kutokujua kiingeleza kuna ambatana na kutokuwa na elimu, kwa Afrika sijaona jinsi ya kumtenganisha mtu aliyeelimika na kujua kiingeleza
 
Sababu kubwa ni moja, hiyo ndio lugha ambayo imetumika kama nyenzo ya kukufundishia, tunajiuliza imekuwaje umemaliza chuo kikuu na haujui kiingeleza? Kiingeleza kwetu na kwa nchi nyingi za Afrika kimepewa kipaumbele na kinatumika kama official language, hivyo kutokujua kiingeleza kuna ambatana na kutokuwa na elimu, kwa Afrika sijaona jinsi ya kumtenganisha mtu aliyeelimika na kujua kiingeleza



Wazungu wa Afrika Kusini (Waafrikaans) pia wanatumia Kiingereza kufundishia, lkn kama Muafrikaans akisema hajui Kiingereza vizuri hakuna Mzungu mwenzake atakaye mcheka, yaani kwa mfano leo hii Zuma akiongea kiingereza kibovu Afrika yetu nyeusi yote itakuwa imepata kinyago cha kumcheka lkn kama Raisi angekuwa Mzungu (Muafrikaans) na akaongea kiingereza kibovu isingekuwa ishu kwa Wazungu wenzake wala hata kwetu, sasa ni kwa nini?
 
Umenikumbusha wasomi wengi wa Kitanzania hawapendi kusoma hadithi za Kiswahili. Wanapenda novels. Wanapenda magazeti ya Kizungu. Waafrika Weusi, hususani Watanzania tunaamini Kingereza ndo weledi.
 
Sio kikristo tu, wabongo maboya sana unakuta mtu kapigiwa simu na ndugu yake kutoka kijiji, anapokea halafu anaenda kuongelea pembeni kikabila lakini simu hiyo hiyo ipigwe na mfanyakazi mwenzie anabaki hapo hapo na kuongea kiswanglish yaani tunajiradhau wenyewe.
 
Emancipate yourselves from mantal of slavery none but ourselves can free our minds have not fear for the atomic energy cos none of them can stop the time. Bob marley.
 
Kingereza kibovu kwenye nchi zetu ni dhihirisho hukuenda shule ama ulilala shuleni wakati wenzio wanapata elimu, ndicho kinatumika kwenye mifumo ya elimu yetu. Wacheni uvivu mjifunze kuongea lugha kwa ufasaha. Mbona nyie Wabongo mnaogopa sana kuongea lugha zenu za asili wakati hapa mnataka kutuaminisha eti mnapenda chenu. Kabla uonge Kiswahili au Kingereza, kwanza penda lugha yako.

Binafsi napenda lugha yangu ya asili, Kikikuyu, na pia nina uwezo wa kuongea lugha kadhaa za Kiafrika, hata huko Bongo nilijaribu sana kujifunza Kinyakyusa na kihaya. Tatizo sikupata waongeaji. Watu hawataki kusikika wakiongea lugha zao, eti wataonekana kuwa washamba.
 
Kingereza kibovu kwenye nchi zetu ni dhihirisho hukuenda shule ama ulilala shuleni wakati wenzio wanapata elimu, ndicho kinatumika kwenye mifumo ya elimu yetu. Wacheni uvivu mjifunze kuongea lugha kwa ufasaha. Mbona nyie Wabongo mnaogopa sana kuongea lugha zenu za asili wakati hapa mnataka kutuaminisha eti mnapenda chenu. Kabla uonge Kiswahili au Kingereza, kwanza penda lugha yako.

Binafsi napenda lugha yangu ya asili, Kikikuyu, na pia nina uwezo wa kuongea lugha kadhaa za Kiafrika, hata huko Bongo nilijaribu sana kujifunza Kinyakyusa na kihaya. Tatizo sikupata waongeaji. Watu hawataki kusikika wakiongea lugha zao, eti wataonekana kuwa washamba.
Umeongea vizuri.MTU akiongea lugha yake ya asili eti mkabila....why?
 
Mleta mada naona hata wewe ni wale wasiojua kiingereza na ambao wanastahili kuchekwa. Ina maanisha uwezo wako wa kuelewa ni mdogo sana.


Anayedharauliwa ni kama wwe mleta mada kwa mantiki hujasoma huna elimu!. Elimu ya Tanzania inatolewa kwa kiingereza. Kama hata kugha ya kusomea shule wwe huijui ina maana wewe ni mbumbumbu,, hujasoma na huna elimu na ndiyo maana unadharauliwa.

Huwezi kumdharau mhindi, mchina ama mfaransa kwa kutokujua kiingereza kwa kuwa elimu yak haitolewi kwa kiingereza na hivyo kutokujua kiingerea kwake hakuna muunganiko na IQ yake. Lakini kama raia wa nchi inayozungumza na kusomesha kifaransa ana kireno awe hakijui, la zima atadharauilika kwamba yeye alipishana na kengele za shule. Kwa maana nyingine ni juha!

Kama wewe vile ambavho hudharauliki kwa kutokujua kireno, kiitaliano ama ki Danish,ni kwa sababu elimu yako haina uwiano na lugha hizo na hivyo huwezi kupimwa kwa hizo. Lakini kama wewe umesoma kwa kiingereza halau hukijui wwe ni juha kwamba ni sawa na ile mijitu inakaaga darasani ksogeza miaka lakini kichwani hakuna kitu.

Ukitaka kuonyesha makali, onyesha uwezo wako katika fani nyingine uanze kujenga heshima la sivyo kulalamikahapa hakukuongezei sifa badala ya ke utadharaulika zaidi kwamba pamoja na kuogopa umande, bado hujitambui na unaishia kulazimisha kuwa pull down wenzako ili ujuha wako uonekane ndicho kiwango cha nchi.

HILO HALIPO. HOPE UMEELEWA.
 
You know me and you fotocopy tugeza yani tunafanana

Don't follow follow me without because yani usinifuate bila sababu.

Andika hapa ze dogi yani ticha akimfundisha dogo English course the dog

Mzungu akiwaaga wabongo byee byee mtafsiri wake mbongo anawatafsiria nunua nunua
 
Mimi nadhani tatizo huwa sio kutojua kingereza, tatizo la watz kukosa fluency ni lack of practise kwenye kuongea, tumesomea kingereza ila hakuna anaetumia kingereza katika maisha out of school,
Ndio maana katika uandishi utakuta wanaandika vizuri ila kuongea wanastrugle,
wakienda kusoma abroad wanafanya vizuri sana,
Then Mimi sioni ulazima wa kujua kingereza that much. maana lugha ni lugha tu what matters ni mawasiliano.
I wish siku moja tubadilishe mitaala mashuleni watu wasome kwa kiswahili from kindergarten mpaka college.
 
Back
Top Bottom