Mwafrika apigiwa debe kuwa Papa

Mwafrika apigiwa debe kuwa Papa

Sumasuma

JF-Expert Member
Joined
Jun 23, 2011
Posts
342
Reaction score
110
Imeandikwa tarehe 03 Machi 2013
By ROMA, Italia
Imesomwa mara: 48
Kadinali Peter Turksonhttps://www.jamiiforums.com/images/kardinali-peterson.jpg
KADINALI Peter Turkson wa Ghana hawanii upapa, lakini ni dhahiri ana wanaomwunga mkono ambao wanaamini anatosha na wamebandika mabango yenye picha yake sehemu mbalimbali za jiji hili.

“Chagua Peter Kodwo Appiah Turkson kwenye Baraza la Makadinali!,” imeandikwa kwa herufi nzito katika mabango juu ya picha ya Kadinali huyo, ambaye ni maarufu miongoni mwa makadinali wanaofikiriwa kumrithi Benedict, ambaye Alhamisi alikuwa papa wa kwanza baada ya karne sita, kujiuzulu.
Mabango hayo yamebandikwa katika mbao ambazo zilitumiwa na wagombea wa uongozi nchini mapema wiki hii.
Tofauti na uchaguzi wa Bunge, wagombea wa upapa kwa kawaida hawatakiwi kuzindua kampeni, hali inayoonesha kuwa mabango hayo yanatoka kwa wafuasi wa Turkson au yawezekana yanabandikwa na wafanya mzaha.
Makadinali wanatarajia kukutana faragha katika kanisa dogo la Sistine kwa siku 10, mkutano ambao chaguo lao litakuwa limebarikiwa na Roho Mtakatifu na si siasa za kidunia.
Turkson anaweza kuwa mtu wa kwanza asiyetoka Ulaya kuongoza Kanisa Katoliki baada ya kipindi cha zaidi ya miaka 1,000 kupita kama atachaguliwa.
Lakini usemi wa zamani wa Kiroma unaonya dhidi ya kukampeni, hata kama ni kwa siri, ili mtu kuwa papa au hata kujaribu kubashiri matokeo ya Baraza la Makadinali.
Unasema: “Anayeingia kwenye Baraza kama papa, anatoka kama kadinali”. Wakati hayo yakiendelea, Papa mstaafu alikuwa akiendelea kusoma ujumbe kutoka kwa wanaomtakia heri huku akivinjari katika bustani za kasri lake.
Papa huyo wa zamani mwenye umri wa miaka 85 alikuwa pia akiangalia televisheni ikirusha matangazo ya kuondoka kwake Vatican Alhamisi jioni, na kulala fofofo katika makazi yake hayo ya upapa katika kasri la Gandolfo, ambako atakaa kwa miezi miwili, msemaji wa Vatican alisema jana.
“Alilala vizuri. Hali ya hewa ilikuwa mwanana yenye utulivu,” Padri Federico Lombardi aliwaambia waandishi wa habari, akikariri alichoambiwa na Katibu Myeka wa papa mstaafu, Askofu Mkuu Georg Gaenswein kupitia simu kutoka makazi hayo yaliyoko Kusini mwa Roma.
Benedict alichukua CD zake za muziki anaoupenda sana na vitabu vingi vya Theolojia, Historia na Falsafa, Lombardi alisema na kuongeza kuwa hivi karibuni ataanza kupiga kinanda chake usiku.
Kuhusu lini Baraza la kumchagua Papa mpya litaanza, makadinali ndio watakaoamua, lakini hilo halitafanyika mpaka idadi ya makadinali 115 kutoka sehemu mbalimbali duniani watakapokuwa wamewasili.
Haijulikani ni wangapi mpaka jana walikuwa wamewasili.
Hakuna kilichokuwa kimeshaandaliwa hadi jana, lakini Vatican inaonekana kujipanga kwa uchaguzi ifikapo katikati ya mwezi huu, hivyo Papa mpya anaweza kusimikwa kabla ya Jumapili ya Matawi Machi 24 na hivyo kuongoza Wiki Takatifu kujiandaa na Pasaka.
· Source: Habari leo
 
I wish they will finally select a black pope this time around. Good luck cardinal Turkson
 
Kabla Papa mpya hajapatikana nani anakuwa in charge?
Nadhani kabla papa mpya hajapatikana, kanisa linakuwa linaongozwa na College of Cardinals chini ya Dean of the College of Cardinals. Dean mwenyewe hana mamlaka ya kufanya maamuzi kama ya papa, lakini iwapo kuna maamuzi mazito yatakayotakiwa kufanyika wakati huo, basi itabidi College yote ikutane ili kufanya maamuzi hayo.
 
Huyu Cardinal mwafrika wa Ghana anastahili, an sifa zote na uwezekano ni mkubwa wa yeye kufika raundi ya mwisho ya kura lakini hatakuwa PAPA.

Atakayekuwa Papa ni yule mwenye jina la PETER, au ubini wake, parokia yake ama jimbo, mtaa, mji atokako ndani kuna Peter.
Huyu mghana ana Peter ila kwa safari hii lazima Papa atoke ITALY. Nawasilisha
 
Mkuu Mooney, hapa umeniacha njia ya panda. Kwanini unadhani jina la Peter ndio litatoa Papa?
 
Huyu Cardinal mwafrika wa Ghana anastahili, an sifa zote na uwezekano ni mkubwa wa yeye kufika raundi ya mwisho ya kura lakini hatakuwa PAPA.

Atakayekuwa Papa ni yule mwenye jina la PETER, au ubini wake, parokia yake ama jimbo, mtaa, mji atokako ndani kuna Peter.
Huyu mghana ana Peter ila kwa safari hii lazima Papa atoke ITALY. Nawasilisha

We umejuaje anastahili?

Watanzania bwana, tumeshindwa kuchagua Rais kabla hata hatujamaliza kujutia makosa yetu tayari tumeshaanza ujuzi wa kuchagua Pope. Eti ana sifa zote, sifa gani? Hovyoo!!

Uongozi wa kiroho hauangaliwi kwa macho ya mwili. Mambo hayo yangefanyika kwa akili kama zako, usingekuta tuna mtu anaitwa Mtume Paulo, ambaye alikuwa Saulo muuaji wa Wakristo
 
Mi nasubiri moshi mweupe!! nakumbuka nilikuwa Form six nilipoujua msamiati wa moshi mweupe!!
 
Hata akitoka ulaya ilimradi mising ya kanisa inafuatwa kama ilivyo.na tena awe kijana sio mzee sana
 
We umejuaje anastahili?

Watanzania bwana, tumeshindwa kuchagua Rais kabla hata hatujamaliza kujutia makosa yetu tayari tumeshaanza ujuzi wa kuchagua Pope. Eti ana sifa zote, sifa gani? Hovyoo!!

Uongozi wa kiroho hauangaliwi kwa macho ya mwili. Mambo hayo yangefanyika kwa akili kama zako, usingekuta tuna mtu anaitwa Mtume Paulo, ambaye alikuwa Saulo muuaji wa Wakristo

Tusubiri, tusiandikie mate
 
Kwa mtu mweusi kuwa pope ni big issue! Misingi ya kanisa katoliki ni mikubwa na kuna usiri mkubwa kuongoza jumuiya hyo hasa top position ya u pope!

nakumbuka mwalimu wangu mmoja alikuwa ni frate aliniambia ukatoliki si dini ya kueleweka kiarahisi, yapo mambo mengi ya misingi, imani na uongoz kwenye hiyo ngazi ya juu. Kwa mwafrika kuwa pale juu ni ngumu sana! Bado mda kufika huko..lets wait n see!
 
Je, ni ngumu kwa mwafrika tu au hata kwa wanaotoka mabara mengine nje ya Europe? Kwa sababu kama sikosei mapope wote wametoka Europe so far.
 
Kwa mtu mweusi kuwa pope ni big issue! Misingi ya kanisa katoliki ni mikubwa na kuna usiri mkubwa kuongoza jumuiya hyo hasa top position ya u pope!

nakumbuka mwalimu wangu mmoja alikuwa ni frate aliniambia ukatoliki si dini ya kueleweka kiarahisi, yapo mambo mengi ya misingi, imani na uongoz kwenye hiyo ngazi ya juu. Kwa mwafrika kuwa pale juu ni ngumu sana! Bado mda kufika huko..lets wait n see!

Hata Mwafrica anaweza sana na kanisa Katoliki liliwahi kuwa na papa wawil au zaidi toka Africa, sina uhakika na idadi
 
Back
Top Bottom