Mkuu nakumbuka, naona the guess imeenda pembeni kidogo...
Ni kweli ukiangalia kijuujuu.
1. Papa Francisco ni muitaliano bila kuchanganya damu. Wazazi wake wote wawili walitoka Turin (Torino) Italy. Kama ulivyoishasikia, babake alikuwa mhamiaji na mfanyakazi wa reli huko Argentina. Cardinal Jorge alizaliwa na kukulia Buenos Aires, Argentina.
2A. Nilisema yeyote atakayekuwa Papa lazima jina PETER LAZIMA liwepo kwenye bio yake.
Maana ya Peter- Petro- Pietro maana yake ni jiwe - MWAMBA na ubini wake ni BERGOGLIO na Bergo ni Rock.
B. Baba Mtakatifu amechagua jina la FRANCIS - Francisco - Franciscus kwa kufuata nyayo za Mt. Francis wa ASSISI.
C. Awali Mt. Francis wa Assisi aliitwa GIOVANI PETRO BERNADONE. Huyu alipenda sana kutunza mazingira na aliwapenda sana wanyama na ndege walikula kutoka kiganjani mwake bila woga.
Babake alikuwa tajiri sana lakini Francis baada ya kuwaona ombaomba na kushinda nao aliamua kuacha maisha ya kitajiri na kuwa mtawa na fukara akitangaza na kueneza injili.