Mwadhamu Polycarp Pengo: Serikali mbili zinatosha

Mwadhamu Polycarp Pengo: Serikali mbili zinatosha

MwanaDiwani

JF-Expert Member
Joined
Mar 22, 2013
Posts
5,536
Reaction score
2,268
pengo+px.jpg

Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Muadhama Polycarp Kardinali Pengo akiwaonesha waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, nakala ya gazeti la Mwanachi lililoandika habari kuhusu msimamo wa Kanisa juu ya suala la serikali tatu.

KANISA Katoliki limekanusha taarifa iliyotolewa na vyombo vya habari kuwa msimamo wa kanisa hilo ni kuwepo kwa serikali tatu katika katiba mpya.
Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo, amesema taarifa hiyo si sahihi bali ilitolewa na Tume ya Haki ya Baraza la Maaskofu pasipo kumshirikisha.

"Wao kama Watanzania wanayo haki ya kutoa maoni, hivyo si kosa wakiwa kama Watanzania maoni yao kuwa ni kuwepo serikali tatu, ilichokosea tume hiyo ni kusema kwamba huo ni msimamo wa Kanisa Katoliki jambo ambalo si kweli," alisema.

Pengo alisema anakanusha vikali taaifa hiyo iliyotolewa juzi na vyombo mbalimbali vya habari hususan magazeti na kuwa Kanisa Katoliki lina wajibu wa kutoa msimamo wake katika mambo mawili tu yanayohusu imani na maadili.

"Kwa mfano ikitokea hoja kwamba kuwepo na vipengele kwenye katiba vinavyosema hakuna Mungu, kuwepo kwa ndoa za jinsia moja au kuhalalisha utoaji mimba hapo kanisa lina haki ya kusimama na kutoa msimamo wake kwani masuala hayo yanagusa imani na maadili,"alisema.

Aliongeza kuwa anatumia nafasi hiyo katika mkutano na waandishi wa habari kutoa msimamo wake kama Mtanzania wa kawaida kuwa mapendekezo yake ni kuendelea kuwepo kwa serikali mbili yaani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ile ya Mapinduzi ya Zanzibar.

"Kama kuna dosari zozote zilizojitokeza wakati wa kuasisi Muungano zinazotishia umoja wa kitaifa ni heri zikarekebishwa ili uendelee mfumo wa serikali mbili kwani serikali tatu ni mzigo," alisema.

Mwishoni mwa wiki iliyopita, Tume ya Haki na Amani ya Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) ilitoa tamko ikitaka Bunge Maalumu la Katiba kuepuka kukashifu mapendekezo ya muundo wa serikali tatu.
Chanzo:Habarileo.
 
Kuna baadhi ya watu wanatumia njia zote hata zile za kilaghai ili kupitisha ajenda zao. Wanashindwa kusimama wao wenyewe ili wahesabiwe kwa kutoa maoni yao kwa sababu pamoja na mambo mengine, wanasumbuliwa na inferiority complex. Hawajiamini kama kauli zao zinakubaliwa/zitakubaliwa na wanachi.

Huwezi kulitumia kanisa Katoliki kwa mambo ya kilaghai hasa ikichukuliwa kuwa kanisa ni kioo katika jamii kwenye maswala ya ubinadamu.

Kuelekea upatikanaji wa Katiba mpya, tutawasikia wengi wakija na matamko huku wakidai yametolewa na taasisi zinazo heshimika katika jamii.

Tunashukuru Baba Askofu kwa kutoa ufafanuzi mzuri kulingana na tamko la Tume ya Haki na Amani.
 
mkuu MwanaDiwani inaonekana wewe masaa 24uko macho! tehe maana mijadala yako unaanzisha usiku kati, au unakuwa unaamini watukanaji wengi watakua washa lala angalau! tehe maana....!
 
Last edited by a moderator:
mkuu MwanaDiwani inaonekana wewe masaa 24uko macho! tehe maana mijadala yako unaanzisha usiku kati, au unakuwa unaamini watukanaji wengi watakua washa lala angalau! tehe maana....!
FYI dunia mviringo...ukilala, wengine wako macho. betlehem, wewe ungependelea serikali ngapi? Mimi, serikali moja lakini kama haiwezekani, serikali tatu. Kuhusu kura? Katika kuamua hatma ya taifa na kwa kuzingatia hali halisi nchini, kura ya wazi ni sawa na kubariki usukule/utumwa, je wewe?
 
Last edited by a moderator:
Kama tunataka muungano wa kweli na imara basi serikali moja inatosha sana. Zanzibar na Pemba ziwe mikoa kama vile Tanga, Iringa nk
 
KANISA Katoliki limekanusha taarifa iliyotolewa na vyombo vya habari kuwa msimamo wa kanisa hilo ni kuwepo kwa serikali tatu katika katiba mpya.
Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo, amesema taarifa hiyo si sahihi bali ilitolewa na Tume ya Haki ya Baraza la Maaskofu pasipo kumshirikisha.

"Wao kama Watanzania wanayo haki ya kutoa maoni, hivyo si kosa wakiwa kama Watanzania maoni yao kuwa ni kuwepo serikali tatu, ilichokosea tume hiyo ni kusema kwamba huo ni msimamo wa Kanisa Katoliki jambo ambalo si kweli," alisema.

Pengo alisema anakanusha vikali taaifa hiyo iliyotolewa juzi na vyombo mbalimbali vya habari hususan magazeti na kuwa Kanisa Katoliki lina wajibu wa kutoa msimamo wake katika mambo mawili tu yanayohusu imani na maadili.

"Kwa mfano ikitokea hoja kwamba kuwepo na vipengele kwenye katiba vinavyosema hakuna Mungu, kuwepo kwa ndoa za jinsia moja au kuhalalisha utoaji mimba hapo kanisa lina haki ya kusimama na kutoa msimamo wake kwani masuala hayo yanagusa imani na maadili,"alisema.

Aliongeza kuwa anatumia nafasi hiyo katika mkutano na waandishi wa habari kutoa msimamo wake kama Mtanzania wa kawaida kuwa mapendekezo yake ni kuendelea kuwepo kwa serikali mbili yaani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ile ya Mapinduzi ya Zanzibar.

"Kama kuna dosari zozote zilizojitokeza wakati wa kuasisi Muungano zinazotishia umoja wa kitaifa ni heri zikarekebishwa ili uendelee mfumo wa serikali mbili kwani serikali tatu ni mzigo," alisema.

Mwishoni mwa wiki iliyopita, Tume ya Haki na Amani ya Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) ilitoa tamko ikitaka Bunge Maalumu la Katiba kuepuka kukashifu mapendekezo ya muundo wa serikali tatu.
Chanzo:Habarileo.
Waandishi wa habari wengi wanakosea sana wanapofikiri kuwa Cardinal Pengo ndiye msemaji wa kanisa katoliki Tanzania. Kwa wale wanaojua vizuri siasa za kanisa, Cardinal Pengo ni Askofu wa Dar es salaam tu; sio mkuu wa kanisa la Tanzania. Msemaji wa kanisa katoliki Tanzania ni Mwenyekiti wa baraza la maaskofu. Sasa huyu mwandishi anapoanza kuwa Kanisa katoliki limekanusha wakati Pengo mwenyewe anasema hayo ni mapendekezo yake kama mtanzania, unaweza kuona kuna contradiction.
 
sasa hii ni nini!!???

Tulishawaachia akina warioba kazi, wakamaliza... na sasa tumewapa watu mia sita ukumbi wafanye upuuzi na maigizo, then huyu jamaa nae anakuja kivyake

where is the authorization matrix in the country, na Pengo anazungumziaje mamilioni ya wakatoliki ambao hawaungi mkono kauli yake??

HE LOST CREDIBILITY LONG AGO, AND HE SHOULD TRY TO KEEP THE SMALL RESPECT HE HAS TO HIMSELF, THIS IS A SILLY MISTAKE TO MAKE AND HE HAD NO REASON WHATSOEVER

SOMETIMES UKISHINDWA KUELEWA NAFASI YAKO, UNAISHIA KUWA KANJANJA TU KAMA KANJANJA WENGINE.... PENGO COULD AHVE MADE SOME ONE ELSE MAKE THOSE REMARKS
 
...inaelekea kuwa hali si shwari ndani ya Kanisa.
 
Hili Levi Mwadiwani Hakuna haja ya kusoma thread zake nikumpa za USO tu
 
Last edited by a moderator:
Hata mimi naamini serikali mbili zinatosha kabisa kama moja imeshindikana.
 
Pengo amedhihirisha ukereketwa wake kwa CCM na ku-confirm dhana inayolalamikiwa na Waislamu kuwa Serikali ya ccm inafuata sera ya mfumo Kristo.
Rasimu ya Katiba imetokana na mawazo ya wananchi yeye ni nani mpaka adharau matakwa yao? Mamlaka ya kuwasemea wananchi ameyatoa wapi?

Wakatoliki watanisamehe kwa hili, ila Mkuu wenu wa Kiroho amepotoka kuingilia na kutoa msimamo wa kisiasa!

Kufikia hapa naweza nikasema bila shaka yoyote kuwa Pengo ni mfuasi wa kambi ya Lowassa.
Kumbuka kipindi kile Lowassa amefukuzwa kazi kwa sababu ya ufisadi, baada ya muda Cardinal Pengo alimtembelea Lowassa nyumbani kwake na kuzindua kitabu cha mke wa Lowassa, Regina!!
 
Yaani huyu hana hata aibu, anaonyesha msimamo wake wa kisiasa kabisa.
 
msimamo wa wakatoliki ni serikali tatu.umesikia juzi.sema lingine acha kulia lia.
 
Mtoa mada una ukurutu kwenye ubongo,sidhani kama mtu mwenye akili timamu anaweza kuandika ujinga huo,liondoe tope zito kwenye akili zako,pengo sii saizi yako kumuingiza katika huo ujinga wako,shame on you.
 
msimamo wa wakatoliki ni serikali tatu.umesikia juzi.sema lingine acha kulia lia.
Amesema kuhusu Pengo na kichwa cha habari kinamhusu Pengo!

Tafadhali elewa mada kwanza kabla ya kuchangia.
 
Back
Top Bottom