GE2025 MWABUKUSI: Kesi ya uhaini ya Lissu iwe LIVE Mahakamani

GE2025 MWABUKUSI: Kesi ya uhaini ya Lissu iwe LIVE Mahakamani

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

tonicimmobility

JF-Expert Member
Joined
Jun 17, 2025
Posts
493
Reaction score
1,038
Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) Wakili Boniface Mwabukusi ametoa wito kwa Mahakama kuona namna ya kurejesha matangazo mubashara ya mwenendo wa kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Tundu Lissu ili kutoa nafasi kwa umma kufuatilia kile kinachoendelea Mahakamani

Soma pia: Tundu Lissu: Sasa ile hofu yangu inatimia, kesi ya uhaini ambayo adhabu yake ni kifo inafanyika gizani ili watu wasijue

Akizungumza na wanahabari kwenye viunga vya Mahakama Kuu ya Tanzania, Masijala ndogo ya Dar es Salaam leo, Jumatano Septemba 10.2025, Mwabukusi amesema wakati kesi hiyo inarushwa mubashara kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ilipunguzo malalamiko ya wanna kwa kiasi kikubwa

Kauli ya Mwabukusi inakuja wakati ambao viongozi na makada wa CHADEMA wakilalamikia kuanyiwa 'hila' na wengine kuzuiliwa kuingia Mahakamani kufuatilia mwenendo wa kesi ya kiongozi wao.

Chanzo: Jambo Tv
 
Kizimkazi anavyopenda mambo ya siri kuficho uozo atakubali??
 
Mbona sioni vyombo vya habari vikiripoti proceedings za kesi ya uhaini inayomsibu shujaa Lissu

Kimya. Waandishi wa habari wapo kimya.

Tatizo nini?
 
Mbona sioni vyombo vya habari vikiripoti proceedings za kesi ya uhaini inayomsibu shujaa Lissu

Kimya. Waandishi wa habari wapo kimya.

Tatizo nini?
tatizo wanahofia watashughulikiwa
 
Ni kesi yetu yaani TAL vs Jamhuri - ila Jamhuri mwenyewe hatakiwi kujua kinachoendelea mahakamani.
 
Mbona sioni vyombo vya habari vikiripoti proceedings za kesi ya uhaini inayomsibu shujaa Lissu

Kimya. Waandishi wa habari wapo kimya.

Tatizo nini?
ukimya wao ni kwa usalama wa vyombo vyao na maisha yao msiwalaumu sana
 
Kufungiwa kwa JF katika. wakati huo huo wa kesi ni sehemu ndogo ya juhudi hizo hizo, za kubana habari zinazo husu kesi hiyo.
 

Conversation​


ENGLISH and SWAHILI

Developments in the Treason Case Against Tundu Lissu: Report from the High Court, Dar es Salaam - September 8, 2025

Criminal Case No. 19605/2025: Republic vs Tundu Lissu.

On September 8, 2025, the High Court of Tanzania in Dar es Salaam was the scene of significant activity in the treason case against Tundu Lissu, a prominent politician and lawyer. The court session began with extensive preparations, attended by CHADEMA party leaders, diplomats, and a large crowd of supporters.

This case, the third of its kind in Tanzania’s history, started with preliminary discussions on legal representation, the court’s jurisdiction, and lower court records.

Preparations were intense, with repeated orders to turn off phones and refrain from recording, which raised concerns about transparency.

Over 200 officers from a special prisons unit were present, and behind-the-scenes discussions caused delays in the case’s commencement.

Case Commencement and Introduction of PartiesThe case officially began in Courtroom No. 1, presided over by a panel of three judges led by Justice Dunstan Ndunguru. Tundu Lissu entered the courtroom with significant presence, followed by the judges.

The court clerk announced the case as Criminal Case No. 19605/2025: Republic vs. Tundu Lissu. The prosecution was represented by a team of seven lawyers led by Nassoro Katuga, alongside Job Mrema, Thawabu Issa, Mossie Kahima, Harrison Lukosi, Cathbert Mbiringi, and Winiwa Kasala.The defense initially included lawyer Neema Saruni, who introduced herself as Lissu’s pro bono counsel.

However, Lissu insisted on representing himself, thanking the court for appointing counsel but emphasizing his 23 years of legal experience. He described the case as the “ultimate test” for Tanzania’s legal system and took full responsibility for his defense.

Tundu Lissu noted that since the Kisutu court, he had a team of over 50 learned lawyers and requested their continued assistance with research, as the prison lacked internet or library access.

Rashid Katuga objected to including this team in the official record, arguing it could complicate a two-party case. The judges allowed Lissu to represent himself, released Saruni, but left room for the research team to assist without being formally recorded.

Discussions on Court Jurisdiction and Charge Sheet, Katuga stated that the prosecution received a “Notice of Motion” from Lissu under CPA Sections 294(1) and 295, challenging the charge sheet’s validity and the High Court’s jurisdiction to hear the case.

He stressed that jurisdiction should be resolved first, citing appellate court decisions like Thabiti Ramadhani Maziku vs. Amina Hamisi Tyeira. Lissu agreed but slightly modified his objection, arguing the court lacked jurisdiction due to significant errors in the Kisutu court’s records.

He noted that treason cases are rare, this being the third after those in 1970 and 1983, requiring a legal precedent.Lissu explained the legal basis for committal proceedings under CPA Sections 261, 184, and 262, stating the charge should have been read in the court of the arrest location (Mbinga), not Kisutu.

He referenced Republic vs. Dodoli Kapufi, emphasizing proper investigation and committal procedures. The judges agreed to address jurisdiction first.Review of Lower Court Records and AdjournmentLissu continued his objections, stating that Kisutu’s records contained significant errors, including over 10 adjournments without explanation under CPA Section 265(1).

He described his journey from Mbinga to Dar es Salaam and repeated adjournments due to incomplete investigations, with records only starting from August 18, 2025, omitting those from April 10.


Katuga admitted Lissu received incomplete records, and the judges ordered complete records to be provided, adjourning the case for one hour for Lissu to review them. Lissu requested 30 minutes, but the judges granted an hour, with Katuga agreeing to ensure a “fair hearing.”After the break, Lissu returned, stating he received two different sets of records—one in prison and another in court—providing evidence of “criminality” and “doctoring” of documents. He pointed out discrepancies in page counts and missing court orders in one set.


Lissu requested an adjournment until the next day to thoroughly review the records and expose the “mischief” involved. Katuga attempted to respond, but the judges stopped him, promising a later opportunity.

The judges granted the adjournment until September 9, 2025, at 10:00 A.M.Conclusion of the DayThe day showcased significant tension between the two sides, with Lissu leading in-depth legal discussions on procedure and records. The courtroom saw moments of laughter and tension, with the crowd expressing opposition to Katuga. The case will continue tomorrow, with further updates expected. This report is based on updates from Hilda Newton, providing a real-time picture of courtroom proceedings.
Source :: X @changeTanzania
 
KISWAHILI

Maendeleo ya Kesi ya Uhaini Dhidi ya Tundu Lissu: Ripoti Kutoka Mahakama Kuu, Dar es Salaam - Septemba 8, 2025

Criminal Case No. 19605/2025: Jamhuri dhidi ya Tundu Lissu.

Kwenye mahakama kuu ya Tanzania mjini Dar es Salaam, siku ya Septemba 8, 2025 ilikuwa na shughuli nyingi katika kesi ya uhaini dhidi ya Tundu Lissu, mwanasiasa na wakili maarufu.

Mahakama ilianza na maandalizi makubwa, ikihudhuriwa na viongozi wa chama cha CHADEMA, mabalozi, na umati mkubwa wa wafuasi.


Kesi hii, ambayo ni ya tatu ya aina yake katika historia ya Tanzania, ilianza na maelezo ya awali na majadiliano kuhusu uwakilishi wa kisheria, mamlaka ya mahakama, na rekodi za mahakama ya chini.

Maandalizi yalikuwa makubwa, na maagizo ya kuzima simu na kutochukua rekodi yalitolewa mara kwa mara, na hivyo kuibua masuala ya uwazi.


Askari zaidi ya 200 kutoka kikosi maalumu cha magereza walikuwepo, na majadiliano ya nyuma ya pazia yalisababisha kuchelewa kwa kuanza kwa kesi.

Kuanza kwa Kesi na Utambulisho wa PandeKesi ilianza rasmi katika Ukumbi Na. 1 wa mahakama kuu, chini ya jopo la majaji watatu wakiongozwa na Jaji Dunstan Ndunguru. Tundu Lissu aliingia mahakamani akiwa na "vibe kubwa sana," na majaji waliingia baadaye.

Karani wa mahakama alitangaza kesi hiyo kama Criminal Case No. 19605/2025: Jamhuri dhidi ya Tundu Lissu. Upande wa jamhuri uliwakilishwa na timu ya mawakili saba wakiongozwa na Nassoro Katuga, pamoja na Job Mrema, Thawabu Issa, Mossie Kahima, Harrison Lukosi, Cathbert Mbiringi, na Winiwa Kasala.

Upande wa utetezi ulianza na wakili Neema Saruni, ambaye alijitambulisha kama wakili wa Lissu chini ya mpango wa probono. Hata hivyo, Lissu alisisitiza kwamba atajitetea mwenyewe, akishukuru mahakama kwa kumteua wakili lakini akisisitiza uwezo wake wa kujitetea kama wakili mwenye uzoefu wa miaka 23. Alieleza kwamba hii ni "ultimate test" kwa mfumo wa kisheria wa Tanzania, na kwamba atachukua jukumu kamili kwa maisha yake.

Lissu alitaja kwamba toka Kisutu, alikuwa na timu ya mawakili zaidi ya 50, na aliomba waendelee kumsaidia katika utafiti, kwani gerezani hakuna mtandao au maktaba.

Mwanasheria wa serikali Rashid Katuga alipinga utambulisho wa timu hiyo kwenye rekodi rasmi, akisema inaweza kusababisha utata katika kesi ya pande mbili.


Majaji walikubali Lissu ajitetea mwenyewe na wakamwachilia Saruni, lakini waliacha mlango wazi kwa timu ya utafiti kuwepo bila kuingia kwenye rekodi.

Majadiliano Kuhusu Mamlaka ya Mahakama na Hati ya MashitakaKatuga alitaja kwamba jamhuri ilipokea "Notice of Motion" kutoka Lissu chini ya vifungu 294(1) na 295 vya CPA, ambapo Lissu alipinga uhalali wa hati ya mashitaka na mamlaka (jurisdiction) ya mahakama kuu kusikiliza kesi. Alisisitiza kwamba suala la jurisdiction linapaswa kuamuliwa kwanza, akirejelea maamuzi ya mahakama ya rufaa kama Thabiti Ramadhani Maziku vs. Amina Hamisi Tyeira. Lissu alikubali na alibadilisha pingamizi lake kidogo, akisema mahakama haina mamlaka kutokana na makosa makubwa kwenye rekodi za mahakama ya Kisutu (committal court). Alieleza kwamba kesi za uhaini ni nadra, na hii ni ya tatu baada ya zile za 1970 na 1983, hivyo inahitaji kuweka precedent ya kisheria.

Tundu Lissu alieleza msingi wa kisheria wa committal proceedings chini ya vifungu 261, 184, na 262 vya CPA, akisema shitaka lilipaswa kusomwa mahakama ya eneo la kukamatwa (Mbinga), sio Kisutu. Alirejelea kesi ya Jamhuri vs. Dodoli Kapufi, akisisitiza kwamba upelelezi na committal lazima zifuatwe vizuri.


Majaji walikubali kuanza na suala la jurisdiction.Uchambuzi wa Rekodi za Mahakama ya Chini na KuahirishwaLissu aliendelea kutoa pingamizi, akisema rekodi za Kisutu zina makosa makubwa, ikiwemo kuahirishwa kwa kesi zaidi ya mara 10 bila maelezo chini ya kifungu 265(1) vya CPA. Alieleza safari yake kutoka Mbinga hadi Dar es Salaam na kuahirishwa mara kwa mara kutokana na upelelezi usiokamilika, na rekodi zinazoanzia tu Agosti 18, 2025, bila yale ya Aprili 10, 2025.

Rashid Katuga alikiri kuwa Lissu alipewa rekodi fupi, na majaji waliagiza rekodi kamili ziwekewe, hivyo kuahirisha kesi kwa saa moja ili Lissu azisome.

Tundu Lissu aliomba dakika 30, lakini majaji walimpa saa moja, na Katuga alikubali ili kuhakikisha "fair hearing."Baada ya mapumziko, Lissu alirudi akisema alipewa rekodi mbili tofauti, moja gerezani na nyingine mahakamani, na hivyo kutoa ushahidi wa "criminality" na "doctoring" ya nyaraka. Alitaja tofauti katika kurasa na maagizo ya mahakama (court orders) yaliyokosekana katika rekodi moja.

Tundu Lissu aliomba kuahirishwa hadi kesho ili asome rekodi vizuri na kuonyesha "uchafu" uliofanyika. Katuga alijaribu kujibu, lakini majaji walimzuia, wakimuahidi nafasi baadaye.


Majaji walikubali kuahirisha kesi hadi Septemba 9, 2025, saa nne asubuhi.Hitimisho la SikuSiku hii ilionyesha mvutano mkubwa kati ya pande mbili, na Lissu akiongoza majadiliano kwa kina kuhusu sheria na rekodi.

Mahakama ilikuwa na vicheko na mvutano, na umati ulionyesha upinzani dhidi ya Katuga. Kesi itaendelea kesho, na masasisho zaidi yanategemewa.

Ripoti hii imetokana na masasisho ya Hilda Newton, ambayo yanatoa picha ya moja kwa moja ya majadiliano mahakamani.
Source : : X @changeTanza
 
Back
Top Bottom